WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezitaka Kamati za Ushauri wa Stadi (Training Advisory Committees–TACs) za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuwa chachu ya kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji halisi ya soko la ajira na uzalishaji nchini. Prof. Mkenda amesema kamati hizo zinapaswa kuwa kiungo madhubuti kati ya VETA, Serikali, waajiri na sekta binafsi, ili kuhakikisha vijana wanaohitimu wanakuwa na ujuzi, umahiri, ubunifu na uwezo wa kutumia teknolojia unaohitajika katika maeneo ya kazi. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda Ameyasema hayo leo, Agosti 13, 2026, jijini Dodoma, wakati akizindua rasmi Kamati za Ushauri wa Stadi za VETA, ambapo amesisitiza kuwa mfumo wa mafunzo ya ufundi stadi haupaswi kuishia katika kutoa vyeti pekee, bali unapaswa kuwaandaa wahitimu kwa ajira, kujiajiri na kuanzisha shughuli za uzalishaji. “Hatupaswi kuwa na mfumo wa mafunzo unaoishia katika kutoa vyeti pekee. Tunataka...
Marato tv - Sauti ya Jamii