Skip to main content

Posts

Showing posts from June 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dodoma Kuandika Historia Mpya ya Usafishaji wa Shaba

_Kiwanda cha Shengde chakaribia kuanza uzalishaji rasmi mwezi Julai_ *Juni 26, 2025- Dodoma* Mkoa wa Dodoma unajiandaa kuandika historia mpya katika sekta ya usafishaji wa madini, kufuatia hatua za mwisho za ujenzi wa kiwanda kipya cha Shengde Precious Metal Resources Company Ltd, kilichopo eneo la Nala, ambacho kinatarajiwa kuanza rasmi uzalishaji wa copper cathode mwezi Julai, 2025. Katika ziara maalum ya ukaguzi, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Menard Msengi, amesema ujenzi wa kiwanda hicho ni hatua kubwa kuelekea utekelezaji wa agizo la Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, la kuhakikisha kuwa hadi kufikia Julai 30, 2025, usafishaji wa shaba yote inayochimbwa nchini unafanyika ndani ya mipaka ya Tanzania. “Ujio wa kiwanda hiki ni kichocheo muhimu katika maendeleo ya Sekta ya Madini mkoani Dodoma na nchini kwa ujumla,” amesema Mhandisi Msengi, na kuongeza kuwa, “mradi huu utawanufaisha wachimbaji wadogo kwa kuwapatia soko la uhakika, kuongeza thamani ya madini...

Tarura Dar es Salaam Yaendelea na Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara iliyosimama Kutokana na Mvua

Dar es Salaam Imeelezwa kwamba uwepo wa mvua nyingi jijijini Dar es Salaam imepelekea ujenzi wa barabara katika maeneo yenye zabuni kusimama kufanya kazi katika kipindi cha miezi miwili. Hayo yameelezwa na Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Geofrey Mkinga wakati akikagua maeneo ambayo yapo chini ya wazabuni. Akikagua barabara ya Tabata-Mazda (mita 500), Tabata-Kinyerezi kuelekea Sokoni (kiwango cha zege) pamoja na barabara ya Kivule-Msongola (km 9) na barabara kuelekea hospitali ya wilaya na Majohe (Km. 2.7). “Kama tulivyotoa taarifa mwanzo kwamba kazi nyingi zilikuwa zimesimama kutokana na uwepo wa mvua nyingi zilizonyesha hivyo kwasasa tumeshawaagiza wakandarasi warudi ‘site’ na kuanza kazi mara moja”. “Wakati wa mvua nyingi wakandarasi hawakuweza kukusanya malighafi na hata kuingia kwenye machimbo, pia huwezi kuweka ‘material’ ya udongo kipindi hicho’ aliongeza kusema. Hata hivyo, Mhandisi huyo aliwataka wakandarasi wote walio...

Dkt. Biteko Azipongeza Ssf na Total Energies Kufikia Viwango vya Juu Vya Usalama vya Usafirishaji

📌 Asema Serikali inaweka sera za kulinda na kuvutia wawekezaji 📌 Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama 📌 Rais Samia apongezwa kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji nchini 📌 Wasafirishaji watakiwa kuzingatia usalama barabarani Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezipongeza Kampuni za Total Ernergies na Super Star Fowarders – SSF  kwa kuweza kufikia viwango vya juu vya usalama vya usafirishaji huku akiwataka wasafirishaji wengine kufuata  nyayo zao kwa kuwa kampuni hizo ni mfano mzuri wa kuigwa. Dkt. Biteko amesema hayo Juni 25, 2025 jijini Dar es salaam wakati akishiriki katika maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya Super Star Fowarders (SSF) na Total Energies.   “ Leo tumekusanyika hapa kusherehekea hafla ya miaka 30 ya ushirikiano baina ya Kampuni zetu hizi mbili za Total Ernergies na Super Star Fowarders. Katika kipindi hicho chote, mmekuwa washirika wakubw...

Rais Samia aipongeza Yanga kwa Ubingwa

Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa 31 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ikiwa ni ubingwa wa nne mfululizo. Kwa zaidi ya miaka 85, upinzani wa Yanga na Simba umeendelea kuwa burudani kwa mamilioni ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Endeleeni kutupa burudani.

Tanzania Itaendelea Kuweka Kipumbele Kwenye Madini Mkakati - Mbibo

*Dar es Salaam* Tanzania imeweka mkakati thabiti wa kuipa kipaumbele Sekta ya Madini , hasa madini yenye thamani ya kimkakati kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi , kuongeza ajira na kuongeza thamani ya Pato la Taifa. Hayo yalisemwa Juni 24, 2025 na Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo wakati akifungua mkutano wa Jiolojia Barani Afrika (PanAfGeo). Mbibo alieleza kuwa, Tanzania imepanga kuendeleza utafiti wa Jiosayansi ambapo imepanga ifikapo mwaka 2030 kufikia asilimia 50 kwa utafiti wa jiofizikia. Akielezea kuhusu uongezaji thamani madini , Mbibo alieleza kuwa, mkakati mwingine ni kujenga viwanda vya kuchakata madini ya kimkakati yakiwemo madini ya Kinywe, nikeli, lithium pamoja na madini ya shaba. Kuhusu ushirikiano wa kimataifa kwenye Sekta ya Madini, Mbibo alifafanua kuwa,Tanzania inaendelea kuongeza ushirikiano na taasisi mbalimbali za kimatsaifa  ikiwemo Umoja wa Ulaya hususani kwenye Sekta ya Madini kwa lengo la kuongeza na ujuzi kwa watalaam wa jiolojia nchini. Mbibo ali...

Masauni ataka wananchi wasichukulie poa suala la mazingira

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Masauni amewataka watanzania kutochukulia poa suala la utunzaji wa Mazingira badala yake wayatunze ili Tanzania iendelee kuwa sehemu salama. Waziri Masauni aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwenye Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Baraza. Masauni alisema katika kuhakikisha suala la utunzaji wa mazingira linakuwa endelevu Baraza linatakiwa kuwekeza nguvu zaidi katika eneo la utoaji wa huduma na elimu kwa umma. Alisema NEC ikifanya hivyo itasaidia watanzania waielewe Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kuona wana wajibu wa kuyatunza Mazingira. Alisema Baraza lina jukumu kubwa la kuhakikisha mazingira yanatunzwa na ili suala hilo lifanikiwe ni lazima kila mmoja kutimiza majukumu yake katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira. Aidha, Waziri aliwataka wahamasishe eli...

Mbunge Mavunde Akabidhi Jengo la Kupumzikia Wananchi Hospital ya Rufaa ya Dodoma

  ▪️RC Senyamule ampongeza kwa jengo na uanzishwaji wa ujenzi wa uzio ▪️Rais Samia apongezwa kwa maboresho makubwa ya huduma ya Afya ▪️Wananchi wamshukuru Mbunge Mavunde kwa utatuzi wa changamoto ya muda mrefu. Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amekabidhi jengo la kupumzikia wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambalo litasaidia kutatua changamoto ya wananchi wengi ambao hawakuwa na eneo lenye staha la kupumzika wakati wakiwa wanawahudumia wagonjwa wao. Hafla hiyo ya kukabidhi jengo hilo imeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary S. Senyamule leo tarehe 25.06.2025. “Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan amefanya kazi kubwa ya maboresho ya vifaa na huduma ya Afya kwenye Hospitali hii ya Rufaa Dodoma. Kazi iliyofanywa na Mbunge Mavunde ni ya kuigwa mfano kwa kuwa ameunga mkono jitihada za Mh. Rais kwenye maboresho ya huduma za Afya. Jengo hili litasaidia sana  kuwafanya wananchi wa Dodoma na nje ya Dodoma kukaa kwenye mazingira mazuri na nadhifu,hivyo ...