Skip to main content

Posts

Showing posts from March 26, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

HESLB yatilia mkazo PPP kutanua wigo wa ufadhili wa wanafunzi

Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga Elimu ni gharama. Elimu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji fedha ili kuyakamilisha ili kupata utulivu wa kujifunza darasani. Serikali inasimamia na kutekeleza kikamilifu Sera ya Elimumsingi Bila Ada ambapo hutumia fedha nyingi kuwezesha upatikanaji wa mahitaji muhimu shuleni ili shughuli za ufundishaji na ujifunzaji ziweze kufanyika vizuri na kuwapunguzia mzigo wazazi na walezi gharama za kusomesha watoto wao. Kupitia Sera ya Elimumsingi Bila Ada, fedha zinawafikia walengwa ipasavyo. Serikali hutuma fedha moja kwa moja katika akaunti za benki za shule ili zigharimie masuala mbalimbali ya kuendesha shule kama vile shughuli za utawala, taaluma, mitihani, ukarabati, michezo na mahitaji mengine kadha wa kadha. Sambamba na hilo, serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatoa ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma Stashahada kwa kozi za kipaumbele, Shahada ya kwanza na kuendelea katika kozi mbalimbali ili kwa pamoja vijana wa Kitanzan...

Mwera na Tungamaa waitika ziara Katibu UVCCM Pangani

Na: Mwandishi Wetu, Pangani Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Pangani, Nasri Mkalipa, amepata mapokezi makubwa katika ziara yake Kata za Mwera na Tungamaa Machi 26, 2026, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya ujenzi wa Chama wilayani humo. Katika ziara hiyo, Mkalipa amewaleza vijana hao namna serikali inavyotekeleza miradi ya maendeleo inayogusa maisha na vijana na wananchi. "Serikali ya CCM ni ya vitendo si maneno, ikiahidi inatekeleza. Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ziwasaidie katika kuinua hali zao za kiuchumi. Vijana na wananchi wa  Pangani tusilale, tuwe sehemu ya wanufaika wa fedha hizo," amesema Mkalipa. Sambamba na hilo, Mkalipa amesema uhai wa Chama unategemea sana vijana, hivyo ni vyema vijana wakafanya juhudi kuongeza idadi ya wanachama kwani nguvu ya Chama ni wanachama wake. Katika ziara hiyo, vijana wamemshukuru Mkalipa kuwatembelea na kusikiliza changamoto zao huku wakiahidi kujitoa kwa ajil...

Fanyeni Kazi Kwa Bidii, Upendo na Ushirikiano Kuboresha Utoaji Huduma Kwa Wananchi - Prof. Shemdoe

Na OWM – TAMISEMI, Dodoma  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM– TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka watumishi wa OWM- TAMISEMI kufanya kazi kwa bidii, upendo, ushirikiano, pamoja na ubunifu katika utendaji wao ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Prof. Shemdoe ametoa wito huo jana Machi 26, 2026 wakati  akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa OWM– TAMISEMI uliofanyika  Jijini Dodoma. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa baraza hilo litumike kama jukwaa muhimu la kuimarisha mshikamano miongoni mwa watumishi na kuleta ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi. “Baraza hili lina nafasi kubwa ya kukuza upendo na ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zetu za kila siku,” amesema Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kushughulikia masuala ya msingi mahali pa kazi, ikiwa ni p...

Tanzania na Urusi Kuimarisha Ushirikiano Katika Teknolojia za Kisasa Ili Kukuza Diplomasia ya Uchumi

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), ameshiriki katika hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Taasisi ya Innopraktika kutoka nchini Urusi yenye muunganiko wa makampuni zaidi ya 142 ya Teknolojia (High Tech companies) na Kampuni ya Gen Z Corporation Limited ya Tanzania.  Hafla hiyo imefanyika tarehe 25 Machi, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Dar es Salaam.  Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Kombo amesema Tanzania na Shirikisho la Urusi zimejizatiti kuimarisha ushirikiano katika teknolojia za kisasa, hatua inayolenga kukuza diplomasia ya uchumi kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili.  Aidha Mhe. Waziri Kombo amesema hati hiyo ya makubaliano imekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera yake Mpya ya Mambo ya Nje, inayolenga kukuza diplomasia ya uchumi, huku ikisisitiza umuhimu wa teknolojia na ubunifu kama vichocheo vya maendeleo end...

Mhandisi Magesa Anogesha Mahafali Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma

 Na Mwandishi wetu GMTV Musoma KATIKA kipindi hiki ambacho fursa za elimu zinazidi kuongezeka nchini,Vijana wametakiwa kuzingatia kuchagua kozi wanazozipenda ili kuongeza uwezekano wa kufanikiwa kitaaluma na katika ajira huku wakisisitizwa kuwa na nidhamu ambayo itawasaidia kufikia Malengo yao. Akizungumza katika hafla ya mahafali ya kidato Cha sita katika shule ya secondari ya Ufundi ya Musoma iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani mara,Mhandisi mwandanizi wa Tanroads mkoa wa Mwanza Eng, Magesa Mwita,amesema kuwa wanafunzi wengi wanaokosa mafanikio hufanya hivyo kwa sababu ya kusoma kozi zisizoendana na vipaji na shauku zao.  Amesema hali hiyo husababisha kushuka kwa ari ya kazi na kufanya iwe vigumu kwa wahitimu kuendelea kukua katika taaluma zao. “Ni bora ukasoma kozi unayoipenda hata kama ni katika chuo usichokipenda, kuliko kusoma kozi usiyoipenda katika chuo unachokipenda,” alisisitiza. Aidha, amebainisha kuwa pamoja na uchaguzi sahihi wa kozi, bidii ni jambo lisiloweza ku...