Skip to main content

Posts

Showing posts from March 29, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mbunge wa Ilala Ashiriki Katika Changizo la Kanisa La Wasabato Magomeni

 Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ameshiriki kwenye Ibada ya changizo maalum la maendeleo ya Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni. Mhe Zungu ambaye pia ni naibu Spika wa Bunge la jamhuri  ya Muungano Tanzania alitumia nafasi hii kuwapongeza  na kuwaomba waumini wa Kanisa la Wasabato waendelee kuliombea Taifa letu pamoja na Rais  Mhe.Dkt .  Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza Vema Taifa letu. Amewaomba pia kuombea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu uweze kufanyika kwa amani.

Ncaa Yang’ara Tuzo za Ubora za Prst 2024

Kampeni ya ‘Merry & Wild: Ngorongoro Awaits’ Yavunja Rekodi* Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kung’ara katika ulingo wa mawasiliano na uhusiano wa umma baada ya kushinda Tuzo ya Ubora ya Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania (PRST) kwa mwaka 2024 kupitia kampeni yake bunifu ya “Merry & Wild: Ngorongoro Awaits.” Kampeni hiyo, iliyolenga kuhamasisha utalii wa ndani wakati wa msimu wa mwisho wa mwaka, imeweka historia kwa kuwavutia watalii wa ndani kwa wingi zaidi ya wageni kutoka nje kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa NCAA. Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 4 Desemba 2024 hadi 4 Januari 2025, jumla ya watalii wa ndani 44,386 walitembelea Hifadhi ya Ngorongoro, ikilinganishwa na 35,837 kwa kipindi kama hicho mwaka uliopita (2023/24). Hii ni ongezeko la watalii 8,549, sawa na asilimia 24%, ongezeko ambalo linadhihirisha mafanikio makubwa ya kampeni hiyo ya kimkakati. Kampeni hii ilijikita katika kuonyesha vivutio vya kipekee vya Ngorongoro kwa kutumia mbinu shirik...

Mbunge wa Itilima Njalu Silanga Amkosha Mzee Wasira

Mbunge wa Jimbo la Itilima Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga, amemweleza Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Steven Wasira kuwa Wilaya ya Itilima imeimarisha zaidi huduma za kijamii kwa wananchi, kutokana na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha nyingi za maendeleo kwa kila sekta.  Mh Njalu ameyasema hayo alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nkoma wilayani humo, katika mapokezi ya Makamu M/kiti CCM Bara, Stephen Wassira.  "Itilima tumejenga kilomita 700 za barabara na tubusasamle (na zaidi) baada ya kuletewa fedha na Serikali ya Awamu ya Tano na ya Awamu ya Sita ya Mama Samia. Tunaishukuru sana Serikali kwa kuwajali wananchi wa Itilima,tumejenga shule za sekondari 12 katika jimbo letu," amesema Mbunge Njalu. "Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetuletea fedha kwa ajili ya kujenga kituo cha kupoza umeme Mkoa wa Simiyu. Zamani tulikuwa na upungufu wa shule, lakini kwa sasa tumejenga shule za madirisha ya vioo. Tunajengewa pia mra...

Waziri Mkuu Akagua Viwanja Vitakavyotumika Chan Agosti 2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 29, 2025 amefanya ukaguzi wa viwanja vitakavyotumiwa kufanyia mazoezi na timu zitakazo shiriki michuano ya CHAN Agosti 2025 na AFCON 2027 kwa Ushirikiano na nchi za Kenya na Uganda. Baada ya ukaguzi huo Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kufanya tathmini ya kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya mazoezi vitakavyotumika kwenye michuano hiyo. Ametoa maelekezo hayo leo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata ambaye ndiyo wakandarasi  wa mradi huo. Amesema ni vyema sasa ufuatiliaji wa karibu wa kila hatua za ujenzi na ukarabati ukafanyika  ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa vifaa vyote ambavyo Mkurugenzi huyo amesema tayari  vimenunuliwa na viko Stoo. "Ndani ya siku tatu hizi fanyeni tathmini mkutane na Mkandarasi na tembeleeni stoo na ...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Asisitiza Umahiri na Ubunifu Kwa Mawakili wa Serikali

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amewataka Mawakili wa Serikali kuzingatia umahiri,weledi, ubunifu na ubora pindi wanapotekeleza majukumu yao. Mhe.Johari ametoa maelekezo hayo wakati akifunga mafunzo kwa Mawakili wa Serikali tarehe 28 Machi, 2025 Jijini Arusha.  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali yalilenga kuwakumbusha na kuwajengea uwezo Mawakili hao katika masuala mbalimbali ya kisheria ikiwemo usalama, Uzalendo na kulinda maslahi ya taifa, Uandishi wa Sheria, Ushauri wa Kisheria, utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, Utambuzi wa vihatarishi na namna ya kudhibiti na Wajibu wa Wakili wa Serikali katika Usimamizi wa Mikataba. “Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo Mawakili wetu wa Serikali katika maeneo mbalimbali ya kisheria ili Mawakili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.” Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewataka Mawakili wa Serikali kuyatumia mafun...