Skip to main content

Posts

Showing posts from April 6, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Massaburi atoa milioni 10 WRC,Asisitiza mshikamano na maendeleo ya kiroho Kivule

Na,George Marato-Dar es salaam MBUNGE wa Jimbo la Kivule, Ojambi Massaburi, ameonesha moyo wa kujitoa kwa jamii baada ya kuchangia shilingi milioni 10 katika Kanisa la The World of Reconciliation Church (WRC) wakati wa maadhimisho ya miaka 19 ya kanisa hilo yaliyofanyika Aprili 6, 2026, katika Kata ya Kivule. Maadhimisho hayo yaliyovutia maelfu ya waumini na wananchi, yalifanyika chini ya uongozi wa Prophet Suguye, ambapo mbali na ibada, pia yaligeuka kuwa jukwaa la kuimarisha mshikamano wa kijamii na kiroho. Akizungumza katika tukio hilo Leo April 6,2026, Massaburi ameeleza kuwa mchango huo ni sehemu ya kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na taasisi za dini katika kujenga maadili mema, kusaidia wahitaji na kuimarisha amani katika jamii. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Deus Clemence Sangu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), ambaye amesisitiza nafasi ya makanisa na taasisi za dini katika kukuza maadili, nidhamu na mshikamano wa kitaifa. Katika k...

Rais Dkt Samia ashiriki dua ya kumuombea Rais wa kwanza wa Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 Aprili 2026, katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day).

Tume ya Uchunguzi yaongezewa muda tena hadi Aprili 24

  Na Mwandishi Wetu *DODOMA* : MAMLAKA ya Uteuzi imeridhia maombi ya muda wa ziada kwa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hivyo imeiongezea tena muda wa siku ishirini na moja (21) na kuitaka ikamilishe kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026. Mamlaka hiyo imeeleza sababu za kuongeza muda huo kwa Tume ni pamoja na kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa. Sababu nyingine ni kuiwezesha Tume kukamilisha maandalizi ya Ripoti itakayowasilishwa kwa Rais na kutoa fursa kwa Tume kuandaa tafsiri ya Ripoti hiyo. Tume hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais kabla au ifikapo April 3,...

Waziri Mkuu ashiriki na watoto wenye mahitaji maalum asisitiza upendo na wajibu wa jamii

_▪︎ Asema hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma_ _▪︎ Aelekeza vituo vyote vitambuliwe na kuimarishwa_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma katika jamii, akisisitiza kuwa kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum si hisani bali ni wajibu wa pamoja wa jamii na Taifa kwa ujumla. Ameyasema hayo Aprili 6, 2026, alipojumuika na watoto wenye mahitaji maalum katika chakula cha pamoja kilichoandaliwa katika makazi yake ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Pasaka.  “Kufanya tukio la aina hii si hisani bali ni wajibu kama ambavyo hata maandiko matakatifu yanatutaka kufanya hivyo kuwahudumia wenye uhitaji,” amesema. Amesema Pasaka ni fursa ya kuenzi na kuendeleza matendo ya upendo, huruma na mshikamano kwa vitendo, huku akiwahimiza Watanzania kuendeleza maadili hayo katika maisha ya kila siku. “Leo tunapata fursa ya kutafakari kwa kina juu ya wajibu wetu wa kuendeleza matendo ya huruma, upendo na mshikamano katika jamii...

Mwakitinya akata utepe mashindano Aweso Vijana Cup

Na: Mwandishi Wetu, Pangani Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Mussa Mwakitinya, amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la "Aweso Vijana Cup," wilayani Pangani mkoani Tanga. Uzinduzi huo umefanyika Aprili 4, 2026, katika uwanja wa Kata ya Mwera. Katika hotuba yake fupi ya ufunguzi, Mwakitinya ameupongeza uongozi wa UVCCM wa wilayani humo kufuatilia uratibu mzuri wa mashindano hayo huku akisisitiza  umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu ili kukuza vipaji vyao. "Vijana wetu wana uwezo mkubwa, kupitia Aweso Vijana Cup tunafungua jukwaa la wao kuonyesha vipaji vyao na kujijengea mustakabali bora," amesema Mwakitinya. Sambamba na hilo, Mwakitinya amesema serikali ipo pamoja na wadau wote wa michezo ili kuhakikisha sekta ya michezo inakua na inachangia maendeleo ya nchi. Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tanga, Ramadhani Omary, amesema vijana ni wadau muh...

Waziri Mkuu Aagiza Hatua za haraka zichukuliwe kurejesha biashara soko la Simu 2000

_Asema Serikali itatoa kauli baada ya uchunguzi_ _Aagiza vibanda vipya vigawiwe kwa wafanyabiashara halisi_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza hatua za haraka kurejesha shughuli za biashara kufuatia ajali ya moto ulioteketeza Soko la Mawasiliano (Simu 2000) lililopo katika Kata ya Sinza, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Ameyasema hayo Aprili 6, 2026, alipofika kukagua madhara ya tukio hilo la moto lililotokea Aprili 4, 2026, ambapo takribani vibanda 500 vya wafanyabiashara wadogo viliteketea. Akizungumza na wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu tukio hilo na itatoa kauli rasmi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina ulioelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.  “Mheshimiwa Rais amepata taarifa ya jambo hili, anawapa pole sana na ameelekeza uchunguzi wa kina ufanyike ili tujue chanzo cha tatizo hili. Na kazi hiyo imekwisha kuanza ili tuweze kupata undani wa chanzo cha jambo...