Skip to main content

Posts

Showing posts from September 12, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TANZANIA NA DRC CONGO WAFUNGUA UKURASA MPYA WA USHIRIKIANO KWENYE MADINI*

▪️Waziri Mavunde na Waziri Kabamba wakubaliana msingi wa ushirikiano, ▪️Ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia na Rais Tshisekedi ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, ▪️Ushirikiano walenga kurahisisha usafirishaji na biashara ya madini, ▪️Wakubaliana kuweka mikakati ya pamoja kuimarisha ufuatiliaji wa uzalishaji wa madini (traceability), *TIANJIN, CHINA* Pembezoni mwa Mkutano wa Madini wa China uliofanyika Jijini Tianjin, Waziri wa Madini *Mhe. Anthony Mavunde* amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), *Mheshimiwa Louis Watum Kabamba* yaliyolenga kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano kwenye sekta ya madini. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika tarehe 11 Septemba, 2026 Waziri Mavunde na mwenzake Mhe. Kabamba walijadiliana kwa kina namna ya kuendeleza sekta ya madini baina ya Nchi zao na hatimaye kuweka msingi ambao utakuwa ni mwanzo wa kuimarisha ushirikiano utakaoleta tija kwa pande zote mbili. "Leo tumekutana hapa si kwa...

KAMPUNI YA BIMA BUMACO YAWAFIKIA WANANCHI WA TANGA

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Kampuni ya bima ya BUMACO imewataka wateja wake kuhakikisha wanauhisha bima zao mara tu zinapoisha muda wake ili kuweza kupata msaada wa haraka pale wanapopata changamoto. Wito huo umetolewa na Afisa Masoko wa kampuni hiyo Mkoa wa Tanga Hosea Urasa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa changamoto inaweza kutokea wakati wowote ule hivyo ni vyema wadau wao ikiwemo wamiliki wa vyombo vya moto na nyumba wakawa tayari muda wote. Urasa amesema kwasasa mwitiko ni mkubwa Kwa wakazi wa Tanga tofauti na awali katika kukata bima na hii imechagizwa na elimu wanayoitoa kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwa na bima na hasa ukataji wa bima za moto. "Watu wa Tanga ni waelewa wanachohitji ni kupatiwa elimu tu,hata baada ya lile janga la moto lililotokea stendi ya daladala baada ya kutoa elimu muitikio umeongezeka zaidi," alisema urasa Aidha Urasa ameongeza kuwa BUMACO wanatoa bima za maisha,mali, vyombo vya moto (magari,piki...

WATOTO WAINUA SAUTI: “VIBOKO SHULENI, NDOA ZA UTOTONI VIKOME”

WATOTO nchini wametaka Serikali kuimarisha utekelezaji wa sheria na sera zinazolinda haki zao, wakisisitiza kukomeshwa kwa vitendo vya ukatili ikiwemo kupigwa viboko shuleni na ndoa za utotoni, wakieleza kuwa hali hizo zinaweza kuathiri elimu, ustawi na mustakabali wao. Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 11, 2026, na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watoto, Daniel Magembe, kwa niaba ya watoto nchini, katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya watoto. Magembe amesema pamoja na kuwepo kwa taratibu zinazodhibiti matumizi ya viboko shuleni, bado baadhi ya walimu wanaendelea kutumia adhabu hiyo kwa kiwango kikubwa, wakiamini kuwa ndiyo njia sahihi ya kurekebisha tabia za wanafunzi. Amesema matumizi ya viboko yanaweza kuwafanya baadhi ya wanafunzi kuishi kwa hofu, kupoteza kujiamini na kushindwa kushiriki kikamilifu katika masomo, hivyo Serikali na wadau wanapaswa kutafuta njia mbadala za kujenga nidhamu bila kumuweka mtoto katika mazingira ya ukatili. “Tuna...