Skip to main content

Posts

Showing posts from July 23, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

UWT YAMUHIMIZA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MARIA NYERERE SHOPPING MALL

 NA: MWANDISHI WETU, DAR Mkandarasi anayetekeleza mradi wa Maduka ya Biashara ya Maria Nyerere (Maria Nyerere Shopping Mall) ulio chini Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), amehimizwa kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, Julai 22, 2026, Jijini Dar es Salaam, katika ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa, kukagua uhai wa Chama na miradi ya Jumuiya hiyo. Chatanda amesema, ipo haja ya mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi, huku akimshauri kuongeza wakandarasi wengine ili kumsaidia baadhi ya kazi na kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo. "Mradi unakwenda vizuri, isipokuwa kwa mwenendo unavyokwenda na kwa muda tuliokubaliana huenda asikamilishe kwa wakati. Mkandarasi tunachomuhitaji aukamilishe mradi kwa mujibu wa tulivyokubaliana na kama kuna maeneo yeye hana uwezo wa kufanya, akabidhi kwa wakandarasi wengine (sub contractors) ili kazi ikamilike kwa...

KAMATI YA UTEKELEZAJI UWT TAIFA YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO STAMICO

 NA: MWANDISHI WETU, KISARAWE Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), imefaya ziara ya mafunzo katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Julai 21, 2026, wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda. Katika ziara hiyo, Wajumbe wa Kamati hiyo, walitembelea kiwanda cha Rafiki Briquettes, kinachochakata makaa ya mawe kuwa nishati safi ya kupikia ambayo ni rafiki wa afya na utunzaji mazingira. Katika ziara hiyo, Chatanda amesema, wanawake wana mchango mkubwa katika kufanikisha kampeni ya nishati safi ya kupikia kutokana na ukweli kuwa kazi hiyo inafanywa kwa kiwango kikubwa na wanawake. "Tunamuunga mkono Rais wetu, Dk. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni ya kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza afya na mazingira. Sisi UWT tunahimiza jamii itumie nishati safi," amesema Chatanda. Aidha, amesema UWT wapo tayari kuwa mabalozi na kushirikiana na STAMICO katika kutoa elimu kwa wanaw...

WIZARA YAJIPANGA KIKAMILIFU KUELEKEA TAMASHA LA NNE LA UTAMADUNI LA KITAIFA 2026.

 Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imefanya kikao cha maandalizi kwa lengo la kupitia na kuratibu hatua mbalimbali za utekelezaji kuelekea Tamasha la Nne la Utamaduni la Kitaifa, litakalofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti 2026. Kikao hicho kimefanyika leo, Julai 23, 2026, katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, jijini Dar es Salaam, kikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda. Akiongoza kikao hicho, Bw. Ntonda amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na maandalizi madhubuti ili kuhakikisha Tamasha la Nne la Utamaduni la Kitaifa linafanyika kwa mafanikio na kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuenzi utamaduni wa Tanzania. Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na watendaji wa Wizara kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji, ikiwemo uratibu wa shughuli za tamasha, maandalizi, pamoja na mikakati ya kuhakikisha tamasha hilo linafanyika kwa ufanisi.

UCHAGUZI CCM TANGA:MWANAFA AMPIGIA DEBE USTADH RAJAB

📍Awaonya wajumbe wasifanye ushabiki wa Messi na Ronaldo Na Mashaka Mhando, Muheza  MBUNGE wa Jimbo la Muheza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma 'MwanaFA', amewataka wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo kutopepesa macho wala kubabaika linapokuja suala la kumchagua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwakani. MwanaFA ametoa kauli hiyo Leo Julai 23 wakati akizungumza na Wana-CCM wa kata za Kwakifua na Tingeni, ambapo ametumia jukwaa hilo kumpigia debe zito Mwenyekiti wa sasa wa mkoa huo, Ustadh Rajab Abdallah, akieleza kuwa rekodi ya kazi zake za kukijenga chama haijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote nchini. *Rekodi Zilizompa Kiki Ustadh Rajab* Akijenga hoja ya kwanini wajumbe hawapaswi kufanya makosa, Mhe. Mwinjuma aliwataka wanachama hao kutaja mwenyekiti yeyote nchini aliyewahi kujenga nyumba za watumishi wa chama kila wilaya, ambapo wajumbe walijibu "hakuna." "Hebu n...

RC TABORA AONYA WANAOKWAMISHA MIRADI

 Na Allan Kitwe, Tabora WAKURUGENZI wa Halmashauri zote Mkoani Tabora wametakiwa kuchukua hatua stahiki kwa Mkandarasi au Mtaalamu yeyote atakayebainika kukwamisha utekelezaji miradi ya maendeleo inayogharamiwa na serikali katika maeneo yao. Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Chacha kupitia kwa Katibu Tawala (RAS) Dkt John Mboya alipokuwa akiongea na Wakuu wa Disivison na Vitengo, Watendaji na Madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Tabora. Ameeleza kuwa serikali ya Awamu ya Sita imeleta fedha nyingi sana katika Mkoa huo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa soko kuu na stendi mpya ya kisasa Mjini Tabora, miradi hii ni muhimu sana. ‘Miradi yote inayotekelezwa hapa Tabora tunataka itekelezwe kwa weledi na ufanisi mkubwa, na thamani ya fedha ionekane kwa kila mradi, katika hili mkandarasi au msimamizi yeyote atakayezembea, atakiona cha moto', ameeleza. RC amesisitiza kuwa wanataka kwenda na kasi ya viwango katika suala zima la utekelezaji ...

GHANA SHARES LOCAL CONTENT SUCCESS STORY AT FIFTH LOCAL CONTENT COMPLIANCE FORUM

 MWANZA Ghana has shared its experience and key strategies behind the successful implementation of local content policies in the mining sector, highlighting strong legislation, stakeholder collaboration, value addition and incentives as critical factors in increasing local participation. Speaking during the Fifth Local Content Compliance Forum (LCCF 2026) in Mwanza, the Deputy Chief Executive Officer (Policy, Planning, Mineral Titles and Local Content) at the Minerals Commission of Ghana, Victoria Awuni, said Ghana's success had been driven by the establishment of clear laws, regulations and policies aimed at ensuring greater participation of local businesses in the mining value chain. Awuni said Ghana had developed policies, including a 2030 policy framework, to ensure that mining operators increasingly contribute to the country's economic development by adding value to minerals before they are exported. She noted that, although only a few mining companies were currently under...

MASAUNI: MUUNGANO SI JAMBO LA KUCHEZEWA, WATANZANIA WAUTUNZE

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema, kati ya jambo ambalo halipaswi kuchezewa ni Muungano ambao unatakiwa kulindwa na kila mmoja maana ndio alama kubwa ya Tanzania. Mhe. Masauni ameyasema hayo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya Julai 22, 2026 akieleza kufurahishwa na shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Pwani zinazofanyika ambazo zinaunganisha na Zanzibar ikiwemo bandari. "Fursa ya Muungano inatakiwa kusaidia pande zote bara na Zanzibar na katika hili itakuwa inasaidia zaidi kwenye sekta ya utalii kwani mtalii anapokuja Zanzibar anaunganisha na Bagamoyo kwenye hifadhi ya Saadani," amesema. Kadhalika amewataka vijana kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii katika kipindi hiki cha utandawazi kutokana na kuwepo kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya vijana. Amewataka kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo ambayo yatakuwa na faida kwao hususani kujifunza mbinu ...

TUME YA MADINI YAJIPANGA KUONGEZA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI*

_Dkt. Numbi atoa somo kutoka Ghana kuhusu usimamizi wa ushirikishwaji wa wazawa katika Sekta ya Madini_ 📍MWANZA Tume ya Madini imejipanga kuimarisha usimamizi wa ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini kwa kuhakikisha watoa huduma na wazalishaji wa bidhaa wanakidhi vigezo na viwango vya ubora vinavyohitajika, hatua inayolenga kuongeza mchango wa sekta hiyo katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Hayo yamesemwa leo, Julai 23, 2026, jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Dkt. Theresia Numbi, kwenye Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF 2026), linalowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo. Dkt. Numbi amesema Tume itaendelea kuboresha usimamizi wa eneo la ushirikishwaji wa Watanzania ili kuhakikisha wananchi wanapata fursa zaidi za kushiriki katika shughuli za uchimbaji wa madini, utoaji wa huduma, uzalishaji wa bidhaa na maeneo mengine ya mnyororo wa thamani wa Sekta ya Mad...