Skip to main content

Posts

Showing posts from October 8, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhe. Esther Matiko azitembelea shule za sekondari Nkende na Rebu

  Mhe Esther Matiko Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara na Mkurugenzi wa taasisi ya Matiko Foundation ameendelea na ziara yake ndani ya Wilaya ya Tarime kwa kuzitembelea Shule za Sekondari Nkende na Rebu zinazopatikana ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime na kufanya mazungumzo na Walimu na Wanafunzi wa Shule hizo. Ikiwa ni utendaji wa majukumu yake ya kibunge, Mhe Esther Matiko amezungumza na Walimu hao na kupokea changamoto mbalimbali ambazo atakwenda kuziwasilisha bungeni kwa ajili ya kufanyiwa kazi na serikali kuu. Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkende Mwl Nchagwa Chacha amemueleza Mhe Esther Matiko changamoto kubwa inayoikabili Shule hiyo ni ukosefu wa Mabweni ya Wanafunzi, jambo lililopelekea Shule hiyo kuanzisha  mchakato wa ujenzi kwa kushirikiana na wazazi na wadau wengine wa elimu. Sambamba na changamoto hiyo Mwl Chacha hakusita kumpongeza Mhe Esther Matiko kwa kutimiza ahadi zake alizoahidi shuleni hapo ikiwa ni pamoja na utoaji wa Taulo za Kike kupitia taasisi ya Matiko...

Dkt.Biteko awasili mkoani Arusha

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili Mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Radiografia Afrika litakaloanza kesho Oktoba 9, 2024. Katika Uwanja wa Ndege wa Arusha, amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda.

Juliana Masaburi ampongeza Rais Dkt.Samia kwa uwekezaji wa zaidi ya shilingi billioni 400 katika bandari ya mtwara

  Mbunge wa Viti Maalum(Vijana Taifa) Mhe. Juliana Masaburi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji wa miundombinu ya zaidi ya shilingi Bilioni 400 katika Bandari ya Mtwara. Akizungumza wakati wa kutembelea bandari hiyo,Juliana amesema kuwa uwekezaji huo utachochea Maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Mtwara na Taifa kwa ujumla. Aidha Mhe. Juliana Masaburi amempongeza Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ndugu Fernand Nyati kwa kusimamia vyema Bandari ya Mtwara na kujipanga vyema kwa maandalizi ya kusafirisha Korosho kwa kupokea Meli zaidi ya 3 zenye makasha ya kusafirisha Korosho hizo. Katika ziara hiyo,Mhe.Juliana aliambatana baraza la umoja wa vijana wa chama chamapinduzi (UVCCM)Mkoa Mtwara ambapo Mwenyekiti wa umoja huo,Komredi Abuu Athumani amesema kuwa wameamua kumleta Mgeni, Mhe. Juliana Masaburi kutembelea Bandari ya Mtwara ili aone uwekezaji wa Serikali na Baraza la Vijana lipate la kujifunza kupitia Bandari hiyo. Mbunge Jul...

Makamu wa Rais ahimiza wananchi kujiandikisha katika daftari la makazi pamoja na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa

 Na MWANDISHI WETU Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amewataka wananchi wa Nzega Mkoani Tabora kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa taarifa za Mpiga kura na kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Dkt.Mpango pia amehimiza chaguzi hizo kudumisha amani na utulivu na Chama Cha Mapinduzi kutuma salama za ushindi wa kishindo katika uchaguzi Mkuu Mwakani. Akizungumza jana katika ziara yake mkoani Tabora Makamu wa Rais Dkt Mpango, amesisitiza umuhimu wa wananchi kuboresha taarifa zao katika daftari la Mpiga kura na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa huku akihimiza kudumishwa kwa amani na utulivu “ Niwasihi wananchi wa Nzega na Tabora kwa ujumla chagueni viongozi wasio wachumia tumbo, mnaye Bashe anafanya vizuri sana twende katika uchaguzi tukiwa wamoja na tubishane kwa hoja dumisheni amani na utulivu. “Tukampe Rais wetu Dkt. Samia zawadi katika chaguzi za serikali za mitaa kwa kazi kubwa aliyoifanya lakini pia tutumie uchaguzi huo CCM kutuma salamu kwa wale wenze...

Dr.Nchimbi afanya kufuru Itilima na kuifunga kabisa ofisi ya chadema wilaya

💠 Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima, Katibu na wanachama wao wahamia CCM. Zaidi ya viongozi pamoja na wanachama 60 wa chama cha Demokrasia na maendeleo(Chadema)wamekihama chama hicho na kujiunga na chama chamapinduzi(CCM) Viongozi na wanachama hao akiwemo Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, wamepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Luguru, wilayani Itilima. Ndugu Kilugala, akizungumza kwenye mkutano huo, amesema mbali na Chadema kuwatumia vibaya viongozi na wanachama wake, kisha kuwaacha ‘watupu’ wakiangaliana wenyewe kwa wenyewe, uongozi wa CCM na utendaji kazi wa serikali yake, chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, vyote vimemfanya arudi nyumbani. “Tulikuwa tunaenda Mwanza siku mbili kwa ubovu wa barabara, leo tunaenda na kurudi. Lazima tusem...

Watakaobainika Kugombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bila Kuwa na Sifa Kagera Kuchukuliwa Hatua

  Na Angela Sebastian-Bukoba  MKUU wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewatahadharisha watu wasio na sifa za kugombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa hususani wahamiaji haramu, kutodhubutu kuchukua fomu na wakibainika  watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria  Hajat Mwassa amebainisha  wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwakwe wakati akitoa taarifa kwa Umma juu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchi nzima  Novemba 27 mwaka huu. "Sisi mkoa wetu uko mpakani tunajua kabisa kuwa wapo watu ambao wameingia hapa nchini na wengine wamebaki bila kutoka hivyo wanaishi kinyume cha sheria na taratibu za nchi na  wangependa kuwa viongozi na wengine wanatumia mbinu mbalimbali ikwemo rushwa ili wachaguliwe kuwa viongozi wakijaribu kugombea tutawachukuli za kisheria" Pia amewatahadharisha wananchi wa Kagera kutochagua watu ambao si watanzania kwani uchaguzi huu ni kwa ajili ya watanzania pekee hivyo mwenye haki y...

Serikali Kujenga Bwawa la Mkomazi-Tanga Kwa ajili ya Kilimo Cha Umwagiliaji

Na Elizabeth Cornely WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema serikali inatarajia kujenga Bwawa la Mkomazi kwa ajili ya umwagiliaji linalotarajia kunufaisha wananchi zaidi ya 20,000 kutoka katika Kata zaidi ya saba na vijiji zaidi ya 28 mkoani Tanga. Kwa mujibu wa Bashe bwawa hilo la Mkomazi ni kati ya mabawa 14 yanayotarajiwa kujengwa mwaka wa fedha 2024/25 na linatarajia kugharimia Sh.bilioni 18. Bashe amesema ujenzi wa Bwawa hilo ilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, hivyo Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuitimiza kwa kutenga fedha za ujenzi wake. “Wananchi wa vijiji vya pembezoni mwa Bwawa la Mkomazi hatimaye mtashuhudia ndoto ya Hayati Julius Nyerere ya kutaka kujenga bwawa hilo la umwagiliaji, ambayo sasa inakwenda kutimizwa na Rais Samia,”alisema Bashe. Amesema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa mabomba mawili yenye urefu wa kilomita 16 na 29 ambayo yatakuwa yanasafirisha maji pande tofauti pamoja na ujenzi wa mifereji mikuu, mifereji ya matupio, uje...