*Asema lengo ukuaji ufikie asilimia saba ifikapo mwaka 2030* MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema CCM inalenga kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia saba ifikapo mwaka 2030, huku ukichochea ongezeko la kipato na kuboresha maisha ya wananchi. Wasira amesema hayo leo (Agosti 21,2026) wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM mkoani Singida, akieleza kuwa ukuaji wa uchumi hautakuwa na maana iwapo hautaonekana katika maisha ya mtu mmoja mmoja kupitia ongezeko la kipato na fursa za kiuchumi. Amesema katika Ilani ya CCM, chama hicho kimeweka msisitizo wa kukuza uchumi jumuishi unaolenga kumwezesha kila Mtanzania kunufaika na ukuaji wa uchumi. “Katika Ilani yetu tumesema tunataka uchumi mkuu ambao kila siku mnasikia Tanzania uchumi wako unakuwa kwa asilimia 6.3. Lakini hii haitoshi. Tunataka uchumi huu usaidie maisha ya mtu mmoja mmoja,” amesema Wasira. Ameeleza kuwa CCM inalenga kuona mapato ya wananchi yanaongezek...
Marato tv - Sauti ya Jamii