Skip to main content

Posts

Showing posts from February 20, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Azindua Shule Mpya ya Sekondari ya Mbatakero

_▪️Asema Rais Dkt. Samia amewapa urithi watoto wa kitanzania wa kupata elimu_ _▪️Apongeza utekelezaji wa mradi huo kwa viwango_ Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la uzinduzi wa shule ya Sekondari ya Mbatakero iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambayo imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP Ujenzi wa Shule hiyo ambao umegharimu shilingi milioni 584 itasaidia kuondoa adha wanayopata wanafunzi wa eneo hilo ya kutembea umbali mrefu wa kwenda shule za jirani za sekondari za Roo na Longoi ambazo ziko umbali wa kilometa 9 kwa kila shule kutoka Kijiji cha Mbatakero na Pia itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule hizo. Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo ni matokeo ya maamuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha anaondoa changamoto kwa wananchi  “Kama mlivyosikia, Rais Dkt. Samia anapoelezewa kuna shida, anasema viongozi watatue changamoto...

Dereva wa Daladala, Mmiliki Kortini wakidaiwa kusababisha Kifo cha Askari na Majeruhi

*Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza*  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewafikisha mahakamani dereva wa gari la abiria T. 234 BUM aina ya Toyota Hiace pamoja na mmiliki wake, kufuatia ajali ya barabarani iliyosababisha kifo cha askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Nyamagana, Coplo Tumsifu Kileo, aliyekuwa akitekeleza majukumu yake, pamoja na kumjeruhi mtembea kwa miguu, Lucia Rweikiza. Washtakiwa hao ni Mohamed Rashid Mumba (40), mmiliki wa gari hilo na Alphonce Fredrick Kashozi (25), dereva wa gali hilo (daladala), ambao wamefikishwa leo Februari 20, 2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana na kusomewa mashtaka nane yanayowakabili. Akisoma shauri la jinai namba 3749 la mwaka 2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, Clement Tuji, Wakili wa Serikali, Stella Minja, alianza kwa kumsomea mshtakiwa wa kwanza, Mohamed Rashid Mumba, ambaye anakabiliwa na mashtaka matatu. Shtaka la kwanza ni kushindwa kutunza kumbukumbu za dereva wake, k...

Dkt. Nchemba Amjulia Hali Mhe. Ibrahim Shayo

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 20, 2026 amemjulia hali mbunge wa Moshi Mjini Mhe. Ibrahim Shayo ambaye amelazwa katika hospitali ya KCMC iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro. Mhe. Ibrahim alipata ajali Februari 18, 2026 katika eneo la Kirinjiko, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Zaidi ya wakazi 22,482 Misungwi kupata huduma ya maji safi, wamshukuru Rais Dkt Samia

Zaidi ya wakazi 22,482 wa Mji wa Misungwi wanatarajiwa kuanza kunufaika na mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ambao sasa umefikia hatua za majaribio. Mradi huo unahusisha ulazaji wa mtandao wa bomba kwa urefu wa KM 38, ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji (Lita 150,000 na Lita 90,000), ujenzi wa kituo cha kusukuma maji kinachojengwa pamoja na Kisima cha maji (Sump well - Lita 50,000) na ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji (domestic points). Mradi umetekelezwa na MWAUWASA kupitia Mkandarasi kampuni ya DATTI CONSTRUCTION LTD kwa fedha kutoka Wizara ya Maji kiasi cha TZS Milioni 888 na utanufaisha wakazi wa maeneo ya *Mbela B, C na D, Shule ya Sekondari Mbela, Mitanda, Mwambola, Ng'ombe, Iteja, Old Misungwi na Mwamanga.* Hatua ya majaribio inayoendelea kwa sasa inalenga kuhakikisha mifumo yote inafanya kazi kwa ufanisi kabla ya kuanza kutoa huduma rasmi kwa wananchi. Kukamilika kwa mradi huu kunaenda kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo na kufikisha asil...

Waziri Mkuu Atoa Siku Tano Kncu Ilipe Deni la Sh. Milioni 400

_Ni za wakulima wa kahawa AMCOS ya Mwika Kinyamvuo_ _Akagua ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Kilimanjaro ahakikishe Chama cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU) kinalipa kwa mkupuo mmoja sh. milioni 400 ambazo chama hicho kinadaiwa na wakulima. Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Februari 20, 2026) aliposimama kusalimia wananchi katika eneo la Chekereni ambapo mkazi wa eneo hilo, Bi. Glory Sam kutoka Chama cha Mwika Kinyamvuo AMCOS alieleza malalamiko yake mbele ya Waziri Mkuu akitaja kusikitishwa na KNCU kuuza kahawa yao msimu wa mwaka 2021/2022 lakini hadi sasa hawajalipwa. “Tuliuza kahawa yetu kwa zaidi ya shilingi milioni 600 lakini mpaka sasa tumelipwa shilingi milioni 200 pekee. Kwa kipindi chote hicho tumekuwa tukidai milioni 400 bila mafanikio.” Dkt. Mwigulu amemtaka Mrajis ahakikishe kuwa hadi kufikia tarehe 25 Februari, 2026 Bodi hiyo iwe imekaa kikao na iamue ni mali gani zi...

Chuo cha Uhasibu Arusha Chaweka Mikakati Katika Kuwainua Vijana Kiuchumi

 DODOMA. IMEELEZWA Kuwa Changamoto Kubwa inayowakabili vijana wengi Nchini Katika Safari ya Kujiajiri ni Ukosefu wa Elimu ya Fedha na Elimu ya Rasilimali watu. Kutokana na changamoto hiyo katika kipindi Cha siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Kimejikita Kuwaandaa Vijana kwa kuwapatia Elimu ya Fedha na Ujuzi wa Biashara ili Waweze Kujiajiri na Kujitegemea. Hayo yamebainishwa Leo February 20,2026 Jijini Dodoma na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) Prof.Eliamani Sedoyeka, wakati wa mkutano wake na wanadishi wa habari kuhusu siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni zamu ya taasisi. Amesema Kuwa Chuo Hicho Kimejikita Katika Kuwaandaa Vijana Kwa Kuwapatia Elimu ya Fedha na Ujuzi wa Biashara ili Waweze Kujiajiri na Kujitegemea. "Vijana wengi wana Ujuzi wa Kitaaluma na Kiufundi, lakini Wanakosa Maarifa ya namna ya Kuugeuza Ujuzi huo Kuwa Fursa ya Ajira na Chanzo Cha Kuajiri Wengine". Amesema Aidha Prof. Sedoyeka Amesema Chuo hicho Pamo...

Ujenzi wa Shule Kuanzia Sasa Uzingatie Madarasa 10

*Asema yatahitajika madarasa 39,000 kukidhi mtaala mpya *Akagua barabara ya Spencon - Mabogini -Kahe - Chekereni WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza watendaji wanaosimamia sekta ya elimu kuanzia sasa waanze kujenga shule zitakazokidhi mahitaji ya mtaala mpya wa elimu ifikapo mwaka 2028. “Tulikuwa na vikao hivi karibuni, niliagiza ujenzi wa shule za sekondari nchini kuanzia sasa hivi uzingatie kuna madarasa 10 na shule zinapoenda kujengwa pawe na eneo la kutosha kujenga yote 10 au tuamue kujenga madarasa matatu kwenye yale saba yaliyokuwepo,” amesema. Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Februari 20, 2026) wakati akizungumza na wananchi wa Mabogini mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Spencon - Mabogini - Kahe hadi Chekereni wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro. Alikuwa akijibu ombi la Mbunge wa Moshi Vijijini, Morris Makoi ambaye aliomba kata hiyo ipatiwe sekondari. Amesema mabadiliko ya mtaala wa elimu yanajumuisha miaka sita ya elimu ya msingi na miaka minne ya elimu ya sekond...