Skip to main content

Posts

Showing posts from April 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Ashiriki Maadhimisho Ya Kumbukumbu ya Miaka 53 ya Kifo Cha Karume

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Aprili 7, 2025 ameshiriki Maadhimisho ya  Kumbukumbu ya Miaka 53 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume kwenye Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua  Zanzibar. Viongozi wengine aliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Stephen Wasira, Mjane wa Hayati Karume, Mama Futuma Karume, Watoto ya Hayati Karume, Amani Abedi Karume na Balozi, Ali Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein.

Waziri Mavunde atoa siku 30 Mgodi wa Magambazi kuthibiti uwezo wa kuendeleza mgodi huo

  📍 *Handeni, Tanga* Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ametoa muda wa siku 30 kwa Kampuni PMM Tanzania Limited inayoendesha na kumiliki Mgodi wa Kati wa Dhahabu wa Magambazi, uliopo katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga, kuwasilisha taarifa za kifedha na kiufundi ili kuthibitisha uwezo wake wa kuendesha mgodi huo kwa viwango vinavyohitajika kisheria. Waziri Mavunde ametoa agizo hilo leo Aprili 6, 2025, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nyasa, Kata ya Kang’ata, Wilaya ya Handeni, ambapo alizungumza na wananchi wanaozunguka mradi huo. Amesema kuwa baada ya kusikiliza pande zote za Kampuni ya PMM ma CANACO zinazohusika katika mgodi huo, ameona ni muhimu kuchukua hatua ili kuhakikisha rasilimali hiyo inaleta manufaa kwa wananchi wa Nyasa, Handeni na taifa kwa ujumla. “Nimeagiza kuwa ndani ya siku 30, kampuni inayoliki huu mgodi, inatakiwa kuwasilisha taarifa za kifedha na kiufundi zinazoonesha uwezo wa kuendesha mgodi wa leseni ya kati, ...

Rais Samia Atimiza Ndoto ya Miaka 50 ya Taifa ya Kuwa na Umeme wa Uhakika Kutoka Bwawa La Mwalimu Nyerere

 _Rasmi mashine zote 9 za kuzalisha umeme Megawatts 2,115 zimekamilika, ndoto ya miaka 50 Rais Samia ameitimiza kwa miaka 4 tu kutoka kuukuta mradi ukiwa chini ya 33% hadi kuumaliza 100%._ Na Bwanku M Bwanku. Moja ya mradi mkubwa wa kimkakati uliokua ukitekelezwa kwenye nchi yetu ni mradi wa kufua umeme kwa kutumia njia ya maji maarufu kama Mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kwenye Mto Rufiji kule mkoani Pwani (Julius Nyerere Hydroelectric Power Project- JNHPP). Mradi huu ni wa 4 kwa ukubwa barani Afrika na umegharimu Trilioni 6.5 ukiwa na mashine 9 ambazo zote kwa pamoja zinazalisha Megawatts 2,115.  Kihistoria, mradi huu ulibuniwa na kuasisiwa mwaka 1975 takribani miaka 50 iliyopita na Rais wa Awamu ya kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuanza kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya 5 chini ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na sasa kukamilishwa kwa haraka na Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Nishati na N...

Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Mkunda awapa pongezi wanamichezo wa JWTZ

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Nchini Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kufanya vizuri katika michezo mbali mbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2025 . Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao  iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya Jeshi Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo leo hii wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpirawa magongo, na mpira wa kikapu. " Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi wa Kimataifa kupitia Meja Mohamed Kasui kwa kuchaguliwa kuwa wa kwanza kutoka Afrika tangu mwaka 1948 kuwa Rais wa Kamati ya Kikapu ya Kijeshi Duniani   jambo la kihistoria kwa Tanzania na Afrika". Aidha, amesema kuwa  Wanajeshi wamekuwa wakilitang...

Rais Mwinyi Awasili Uingereza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili Jijini London,  nchini Uingereza tarehe 6 Aprili 2025. Katika uwanja wa ndege wa London Heathrow, Rais Dkt.Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Mbelwa Kairuki. Rais Dkt.Mwinyi ataanza ziara yake ya kikazi nchini humo leo na kumaliza tarehe 9 Aprili 2025.

Dkt Biteko awapongeza walimu Al - Muntazir kwa kulea watoto wenye mahitaji maalum

  📌 Aguswa namna watoto hao wanavyofundishwa stadi za maisha 📌 Al Muntazir yahudumia zaidi ya wanafunzi  100 wenye mahitaji maalum Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewapongeza walimu na uongozi wa Shule ya Al Muntazir kwa kuwahudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa upendo mkubwa. Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Aprili 6, 2025 katika viwanja vya Shule ya Al Muntazir iliyopo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya matembezi ya Maadhimisho ya Siku ya Usonji Duniani iliyofanyika shuleni hapo kitaifa. Amesema mara baada ya Mungu kumuumba mwanadamu mtu mwingine anayeweza kumuumba mwanadamu kwa kumfundisha na kumkuuza kimaarifa na maadili ni mwalimu. “ Tumeona watoto hawa wanafanya kazi mbalimbali, wanafundishwa na wanaongozwa vizuri  niwapongeze walimu wote wa shule hii mnaofundisha watoto wenye mahitaji maalum pamoja na uongozi wa shule mmefanya kazi hii kwa watoto kwa ujuzi mlionao mmefanya wanaweza kuimba kuandika, kutengeneza sabun...