Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi waiomba tume ya ushindani (FCC) kuendelea kuthibiti na kutoa elimu ili kuepuka athari za matumizi ya bidhaa bandia. Hayo yamesemwa na wafanyabiashara wa soko kuu la Manispaa ya Musoma mara baada ya kufikiwa na maafisa wa Tume ya ushindani kupata elimu ya bidhaa bandia,mikataba ya mlaji (mikopo inayotolewa na taasisi za fedha)inayotoa vigezo na masharti vilivyoandaliwa na upande mmoja. Maafisa hao wa ukaguzi bidhaa bandia Mgasi Kalindimya na Thomas Maisory wamewaelimisha wafanyabiashara hao umuhimu wa kutambua bidhaa wanapofanya manunuzi au kuuza bidhaa zao kwa mtumiaji wa mwisho sambamba na vigezo na masharti ya mikopo kwa mlaji (mkopaji). Tume ya ushindani (FCC) inaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara mkoani hapa kuondokana na uuzaji wa bidhaa bandia zinazopelekea kuathiri afya kwa walaji. Akiongea na GMTV Jane Maginga mfanyabiashara wa soko kuu la Musoma mkazi wa Mwisenge amesema hivi sasa bid...
Marato tv - Sauti ya Jamii