Skip to main content

Posts

Showing posts from June 26, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MIAKA 30 YA TRA: MAKUSANYO YAPAISHWA HADI TRILIONI 32, TANGA YAVUKA LENGO KWA KUKUSANYA BILIONI 495

 📍Wafanyabiashara wakiri kumalizika kwa uhasama wa 'Paka na Chui', taasisi za fedha zaahidi ushirikiano NA Mashaka Mhando, Tanga MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, ambapo makusanyo ya kodi yamepanda kutoka Shilingi Bilioni 531 mwaka 1996/1997 hadi kufikia Shilingi Trilioni 32 kwa mwaka uliopita. Hayo yamebainishwa leo wakati wa matembezi maalum ya hisani na mazoezi yaliyoanzia katika ofisi za TRA Mkoa wa Tanga hadi viwanja vya Usagara, yakiwa ni sehemu ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya mamlaka hiyo na maandalizi ya Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora. Akizungumza baada ya kuongoza matembezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, aliipongeza TRA kwa hatua kubwa iliyopigwa na kueleza kuwa Mkoa wa Tanga umefanya vizuri kwa kuvuka malengo ya makusanyo kwa asilimia 100. Balozi Batilda alieleza kuwa kukua kwa shughuli za Bandari ya Tanga, mipaka ya Horohoro, na wilayani kumeufan...

KARAMAGI AONGOZA KAMATI SIASA MKOA WA KAGERA KUKAGUA MIRADI

 Na Angela Sebastian ;Bukoba  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kagera,Nazir Karamagi, ameongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa huo kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ikiwa ni utaratibu wa chama hicho kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kuhakikisha miradi inanufaisha wananchi. Katika ziara hiyo, kamati ilitembelea mradi wa ghala la kuhifadhia dagaa uliopo katika Mwalo wa Rukojo, Kata ya Kaagya uliogharimi zaidi ya shilingi milioni 100 pia, ilikagua ujenzi wa shule ya msingi Kamagoba ambao umegharimu zaidi ya shl mil. 300 ambapo Karamagi amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi hicho cha pesa ili kufanikisha miradi hiyo yenye manufaa kwa jamii. Pia ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo sambamba na kutenga fedha ya mapato ya ndani kutekeleza miradi mbalimbali kwa ufanisi wa hari ya kulidhisha huku, akisisitiza umuhimu ...

WAFANYABIASHARA MKOANI TANGA WATAKIWA KUWA WAZALENDO KWA KODI KWA UAMINIFU.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amewataka wananchi wanaoanzisha kampuni binafsi kusajili ndani ya mkoa ili kuongeza mapato  ya mkoa Kwa mafunufaa ya mkoa na taifa Kwa ujumla . Hayo ameyasema alipokuwa  akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika uwanja wa usagara baada ya matembezi ya furaha ikiwa ni muendelezo wa shughuli  maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya mapato Tanzania TRA yaliyoanza tangu tarehe 22 Juni mwaka huu na  kilele chake ni tarehe 1 julai mwaka huu. Aidha Batilda alisema kuwa kufanya hivyo serikali ya mkoa itafikia malengo inayojiwekea Kila mwaka kwani mkoa wa Tanga una fursa nyingi ya kujipatia Kodi ikiwemo bandari,uvuvi,madini pamoja na mipakani. Sambamba na hayo aliwataka wafanya biashara wote kuweza kutoa risiti  na Kwa wale ambao wanapunguza gharama kwenye risiti waache mara moja tabia ya kuiibia serikali hivyo wafanya biashara hususanabwafanya biashara wa madini kuwa makini katika kuan...

HOSPITALI YA SHIFAA YAJA NA TUMAINI JIPYA WANAOSUMBULIWA NA KISUKARI

Na Mwandishi Wetu HOSPITALI ya Shifaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imeanzisha madarasa kwaajili ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa lishe bora na mtindo wa maisha ikiwa ni jitihada za kukabiliana na changamoto ya kisukari ambacho kimekuwa chanzo cha magonjwa mengi sugu. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Daktari bingwa mbobezi wa homoni na tezi wa Hospitali ya Shifaa ya Kinondoni, Dk Singla Mosha, wakati akizungumzia magonjwa sugu.  Alisema miongoni mwa maradhi wanayotibu ni kisukari na kwamba kitu cha muhimu ambacho wamekuwa wakitilia mkazo ni kutambua kuwa shida ya ugonjwa wa kisukari ndiyo msingi wa matatizo mengi ya kiafya. Alisema Katika matibabu ya sukari na magonjwa mengine sugu, eneo ambalo halijapewa nafasi yake ipasavyo na msisitizo wa kutosha ni suala la lishe na mtindo wa maisha. Alisema Shifaa imejikita sana katika kuonesha umuhimu wa lishe na mtindo wa maisha katika kukabiliana na changamoto hiyo ya kisukari ambacho ndicho chanzo cha matatizo mengi ya marad...

BEI ZA MAFUTA ZITAANZA KUSHUKA MWEZI JULAI – WAZIRI NDEJEMBI

 WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Watanzania wataanza kushuhudia kushuka kwa bei za mafuta kuanzia mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuanza kushuka kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia baada ya kusitishwa kwa mapigano ya Mashariki ya Kati. Akijibu mwongozo wa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu, Bungeni jijini Dodoma leo Juni 26, 2026, Ndejembi amesema Serikali imezielekeza EWURA, TPDC na PBPA kuhakikisha manufaa ya kushuka kwa bei duniani yanafika kwa walaji nchini. Amesema licha ya athari za vita kati ya Iran, Israel na Marekani zilizosababisha usumbufu katika usafirishaji wa mafuta kupitia Mlango wa Hormuz, Tanzania iliendelea kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta bila kukumbwa na uhaba. Ndejembi amesema hatua za haraka zilizochukuliwa na Serikali zilihakikisha mafuta yanapatikana katika maeneo yote ya nchi, huku Tanzania ikiendelea kuwa na bei nafuu zaidi ya mafuta ikilinganishwa na...

MAGARI YA SHULE YENYE TINTED HAYARUHUSIWI KUBEBA WANAFUNZI

Kutoka: Dawati la Habari Polisi Mwanza Katika mwendelezo wa ukaguzi wa magari ya shule hususan katika kipindi hiki cha likizo, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limeendelea na zoezi la ukaguzi likiwa na lengo la kuboresha huduma ya usafiri na kuimarisha usalama wa wanafunzi. Zoezi hilo lililozinduliwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Dcp Wilbrod Mutafungwa tarehe 18.06.2026 limeendelea leo, Juni 26, 2026, katika viwanja vya Shule ya Msingi Nyang’homango iliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, ambapo jumla ya magari 25 yamekaguliwa. Akizungumza na madereva pamoja na walezi wa wanafunzi wakiwemo ma-patron na ma-matron, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Misungwi, ASP Maris Isomba, amesema kuwa lengo kuu la ukaguzi huo ni kuhakikisha watoto wanakuwa salama wanapokwenda na kurudi kutoka shuleni. Aidha, ASP Isomba amekemea tabia ya baadhi ya wamiliki wa magari ya shule kuweka vioo vya giza (tinted). Amesema kitendo hicho ni kinyume cha sheria kwa magari ya usafiri wa umma na...

TANZANIA YATAMBULIWA ULIMWENGUNI KAMA MFANO WA KUIGWA KATIKA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE

 Na Mwandishi Wetu  Tanzania imeendelea kujijengea heshima katika jukwaa la kimataifa baada ya kutambuliwa kama mfano wa kuigwa katika kutetea haki za wanawake, ikiwemo wafanyakazi wa majumbani, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake katika Diplomasia ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika Geneva, Uswis. Utambuzi huo ulitolewa wakati wa Mjadala wa Haki za Binadamu kuhusu Haki za Wanawake uliofanyika pembeni mwa Kikao cha 62 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, kinachoendelea Geneva kuanzia tarehe 15 Juni hadi 7 Julai 2026. Kikao hicho kimewakutanisha wanadiplomasia, maafisa wa UN na wawakilishi wa asasi za kiraia kupitia maendeleo ya ahadi za kimataifa za haki za binadamu, huku mwaka huu mkazo ukiwa kwenye usawa wa kijinsia na ulinzi wa wafanyakazi walio katika mazingira hatarishi. Akizungumza kwa niaba ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Bi. Chidi King, Mkurugenzi wa Kitengo cha Jinsia, Usawa na Ushirikishwaji katika Sh...

WALALAZE: TRA, TUMEJIPANGA KUFANIKISHA MAKUSANYO YA KODI KWA MAENDELEO

 NA: MWANDISHI WETU, DODOMA  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo ni miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Fedha imejipanga kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 inafanikiwa kikamilifu katika utekelezaji wake. Hayo yameelezwa na Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Paul Walalaze, Juni 26, 2026, Jijini Dodoma. Walalaze amesema, bajeti nzima ni shilingi trilioni 62.33, ila TRA ina jukumu kuhakikisha inafanikisha makusanyo ya shilingi trilioni 36.99, ili mipango mizuri iliyowekwa na serikali katika kukuza maendeleo na ustawi wa wananchi ifanikiwe. "TRA inaendelea kusimamia mkakati wa utiifu wa hiari kupitia utoaji wa elimu kwa walipakodi kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na mlango kwa mlango. Kimsingi, wananchi wakielimishwa ipasavyo juu ya umuhimu wa kulipa kodi na namna kodi hizo zinavyoweza kuleta maendeleo, hawana shida wanalipa, na ndiyo maana TRA tumeimarisha sana elimu ya mlipakodi na matunda yake tumeyaona," amesema Walalaze. Aidha, W...