Skip to main content

Posts

Showing posts from October 4, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Nchimbi Aendelea Kusaka Kura za Ccm Tabora,Leo Kuunguruma Sikonge na Kaliua.

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi bado yupo mkoani Tabora ambako anaendelea na kampeni za kunadi sera za chama hicho pamoja na kuelekea kuelekea Uchagzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu. Dk.Nchimbi katika kampeni hizo anaendelea kuipeperusha bendera ya chama hicho akinadi sera na kuwanadi katika maeneo yote anayopita akiwemo Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni hizo, Dkt. Nchimbi leo Oktoba 05, 2025 atafanya mikutano ambayo itaanza na mkutano Sikonge Uwanja wa TASAF na kisha atamaliza mkutano wake mkuu utakaofanyika Kaliua kwenye Viwanja vya Konane.

Madaktari bingwa wa Tanzania waanza kambi maalumu Anjouan kuokoa maisha

  Na Mwandishi Wetu Visiwa vya Anjouan, Comoro vimeendelea kushuhudia mshikamano wa kidugu kati ya Tanzania na Comoro kupitia ujio wa madaktari bingwa wa Kitanzania kwa ajili ya kambi ya matibabu ya kibingwa. Jana, msafara wa kwanza wa madaktari bingwa kutoka Tanzania ulipokelewa rasmi na Gavana wa kisiwa cha Anjouan, Dkt. Youssef Zaidou, katika ofisi yake iliyopo jengo la DAR-NADJAH. Baada ya mapokezi hayo, madaktari walielekea Hospitali za Bambao, Hombo na Pomon ambako wanatarajiwa kutoa huduma kwa kipindi cha wiki moja, kuanzia tarehe 4 hadi 11 Oktoba 2025. Leo, mapokezi ya msafara wa pili wa madaktari bingwa kutoka Tanzania yamefanyika hapa Anjouan yakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Said Yakubu, pamoja, mwakilishi wa Gavana, Dkt. Samir Mohamed. Katika mapokezi haya, pia walihudhuria viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro. Msafara huu wa pili umeongozwa na Mwenyekiti wa Tiba Utalii Taifa, Dkt. Peter Kisenge, akifuatana na Mratibu wa Tiba Utalii kutoka Wizara ya ...

Democratic Party (Dp) Yaahidi Kusamia Rasilimali Na Kufuta Kikokotoo

>Ameahidi kusimamia rasilimali za nchi >Kuheshimisha utu na thamani ya mwanamke. >Kuboresha Mishahara kuongeza ufanisi wa uwajibikaji. >Kurudisha ujamaa >Kufuata ndoto na nyayo za Rais wa awamu ya tano. Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma Mgombea  wa Urais kupitia Chama Cha Democratic (DP) Abdul Juma Mluya amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atasimamia rasilimali zilizopo kunufaisha wazawa na kuondoa kikokotoo kwa watumishi wa serikali. Ameyasema hayo Septemba 30 akiwa ziarani mkoani Mara wakati akinadi sera zake na kuwaomba wananchi wa mkoa huu kumchagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amesema huduma zinazotolewa  hazikidhi haja za wananchi wa Tanzania kutokana na uwajibikaji mbovu wa viongozi kwa kuhujumu fedha za Umma. Amesema endapo wananchi watamchagua hakutakuwa na tozo za janjajanja ataboresha huduma za Afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kutosha katika vituo vya afya nchini kote, huduma bora kwa aki...

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Uapisho Rais wa Malawi

⬛Rais Mutharika awahakikishia wananchi kuwa Serikali yake itawaletea maendeleo ⬛Awasisitiza viongozi kushirikiana na kuwatumikia Wamalawi WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 04, 2025 amemwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais Mteule wa Malawi, Peter Mutharika uliofanyika katika uwanja wa Kamuzu, Blantyre nchini humo. Mheshimiwa Rais Mutharika wa Chama cha Democratic Progressive (DPP) alimshinda mpinzani wake Rais Mstaafu Lazarus Chakwera wa The Malawi Congress Party (MCP) kwa asilimia 56.8. Mutharika aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo kati ya mwaka 2014 hadi 2020 alipoangushwa na Mheshimiwa Chakwera, hivyo Mheshimiwa Rais Mutharika anarudi tena katika kiti hicho cha Urais baada ya miaka mitano. Akizungumza baada ya kuapishwa Mheshimiwa Rais Mutharika amesema nchi ya Malawi ni kwa ajili ya Wamalawi wote, hivyo amewataka viongozi wajitokeze na washirikiane katika kuwatumikia watu na si matumbo yao, watoto wao au marafiki zao. “Sote tunahitaji mabadiliko...

Dkt.Nchimbi Awasalimia Wananchi wa Jimbo la Manonga,Amuombea Kura Dkt.Samia

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia Wananchi wa Kata ya Ziba,Jimbo la Manonga,wakati akielekea  kwenye mkutano wake wa jioni katika kata ya Ndala jimbo la Nzega Vijijini mkoani Tabora leo Oktoba 4, 2025. Baada ya kuwasalimia wananchi hao,Dkt.Nchimbi aliwaomba pia kumpigia kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,Dkt.Samia Suluhu Hassan,aidha alimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Manonga,Ndugu Abubakari Alli Omari pamoja na Madiwani. Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 18 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Oktoba 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Dkt.Nchimbi Ndani ya Jimbo la Bukene,Tabora

Picha mbalimbali za mkutano wa kampeni wa Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi uliofanyika kata ya Itobo katika Jimbo la Bukene, mkoani Tabora leo Oktoba 4, 2025.

Dkt Samia Awaomba Kura Wananchi wa Babati

Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa akizungumza na Wananchi na Wanachama wa CCM wa Babati katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho Mkoani Manyara tarehe 04 Octoba, 2025.