Skip to main content

Posts

Showing posts from February 26, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

EWURA NA MISA Tan yaendelea kuwanoa wahariri na waandishi wa habari Nchini

Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari ambao ni wanachama wa MISA Tan toka Mikoa mbalimbali. Takribani waandishi wa habari hamsini (50) wamehudhuria warsha hiyo yenye kulenga kufanya tathimini ya kuwajengea uwezo kwenye kuifahamu EWURA na majukumu yake. Mafunzo hayo yalifunguliwa na mgeni rasmi Eng. Lorivii Long'idu ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa EWURA alisema kuwa, waandishi wa habari ni daraja la muhimu kwenye kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi juu ya haki zao kwenye huduma za nishati na maji. Naye Mwenyekiti wa Misa Tan Bwana Edwin Soko aliwataka waandishi wa habari kuandika habari za uwajibikaji ili kuwasaidia jamii kujua haki zao. Naye  Kaimu Meneja  Mawasiliano wa EWURA Bwana Wilfred Mwakalosi alisema kuwa, ni vyema waandishi wa habari wakajikita kwenye kuandika habari zenye kueleza haki za walaji kwa kina ili watamb...

Rais Samia Akutana na Balozi wa Singapore Ikulu Dar es Saalam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Singapore nchini Tanzania Mheshimiwa Douglas Foo, tarehe 27 Februari, 2026 Ikulu, Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha Uhusiano baina nchi hizi mbili haswa katika masuala ya teknolojia,elimu, afya na miundombinu.

Ziara ya Waziri Mkuu Arusha Yarejesha Tumaini Kwa Flora Mbeve

*Akabidhiwa sh. milioni 1.8 kulipa deni la kikoba MKAZI wa Arusha, Bi. Florah Mbeve amekabidhiwa sh. milioni 1.8 ili akalipe deni analodaiwa kwenye kikoba ambazo alikopa na kumpa mumewe kisha akatelekezwa na mwanaume huyo kwa madai kuwa anazaa watoto wa kike tu. Februari 24, mwaka huu, Bi. Florah aliwasilisha kero yake mbele ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo linapojengwa soko jipya la Kilombero wakati akiwa kwenye ziara ya siku tatu mkoani Arusha. Alisema alikuwa anauza vipande vya matikiti ili apate fedha za kujikimu na wanawe wanne na kiasi apeleke kwenye rejesho.  Bi. Florah alikabidhiwa fedha hizo taslimu jana (Alhamisi, Februari 26, 2026) na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude kwa niaba ya Waziri Mkuu ambaye aliahidi kumsaidia mama huyo. Akimkabidhi fedha hizo ofisini kwake mbele ya Mwenyekiti wa kikundi cha Jikomboe, Bw. Laurent Mwita Marwa, Mkuu huyo wa Wilaya ya Arusha alisema kuwa amemkabidhi kiasi hicho cha fedha kut...

Katibu Mkuu wa Umoja Wa Mabunge Duniani (Ipu) Awasili Nchini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Bw. Martin Chungong amewasili nchini usiku wa kuamkia leo Februari 27, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya kushiriki hafla ya  Uwekaji Saini Mkataba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) utakaofanyika Oktoba 2026 Jijini Arusha. Hafla hiyo ya uwekaji saini inafanyika leo Februari 27, 2026 katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam ambapo Bw. Chungong na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu wataweka saini mkataba huo.

Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Jnhpp Yakagua Maendeleo ya Bwawa la Julius Nyerere

📌Yasema mradi umesimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi 📌Yasisitiza ni kichocheo muhimu katika za fursa za kiuchumi na kijamii Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), tarehe 26 Februari 2026, imekagua maendeleo ya uzalishaji wa umeme katika mradi huo na kueleza kuridhishwa na usimamizi pamoja na utekelezaji wake, uliokidhi viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha iliyowekezwa na Serikali. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi , amesema kamati imefurahishwa na namna bwawa hilo linavyochochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji wa umeme unaosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini, hatua inayochangia kuimarika kwa upatikanaji wa nishati ya umeme. “Tumeridhishwa na jinsi mradi huu ulivyosimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Ukilinganisha na miradi mingine barani Afrika, mradi huu umejengwa kwa ubora wa hali ya juu na umeleta unafuu katika huduma ya umem...

Halmashauri Kuu ya Ccm Mbeya Yampatia Tuzo ya Heshima Dc Itunda

📍Yataja utendaji wake kama kiungo muhimu kwenye chama na serikali *NA MWANDISHI WETU, MBEYA* Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Vijijini, imemtunukia Tuzo maalum ya Heshima na Shukrani Mkuu wa Wilaya hiyo, *Mhe. Solomon Itunda*, kwa kutambua mchango wake mkubwa wa kuunganisha Serikali na Chama katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025. Tuzo hiyo imekabidhiwa jana tarehe 26 Februari 2026, wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya kilichopokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2025. Akisoma maelekezo ya Kamati ya Siasa mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Hakimu Mwalupimbi, amemuelezea DC Itunda kama "Kiungo" madhubuti ambaye amekuwa akipatikana wakati wote kushughulikia kero za wananchi na mahitaji ya Chama bila kujali muda. "DC Itunda umekuwa kiungo kikubwa baina ya Chama na Serikali. Iwe usiku wa manene, asubuhi au mchana, umekuwa ukipokea simu na ...