Skip to main content

Posts

Showing posts from September 18, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tamasha la Utamaduni Lawakosha Wafanyabiashara Ruvuma

Na Elizabeth Zaya BAADHI ya wakazi wa Songea mkoani Ruvuma wamefurahia ujio wa Tamasha la Kitaifa la utamaduni mkoni Ruvuma kwa kuwapa fursa za kufanyabiashara na kujitangaza kupitia tamasha hilo. Kadhalika, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha utaratibu huo wa kuwa na tamasha la utamaduni kwa kuwa pamoja na kuwakumbusha kuenzi tamaduni zao lakini wanalitumia kujinufaisha kiuchumi. Tamasha la Utamaduni la Kitaifa linatarajiwa kufanyika kwa mara ya tatu mkoani Ruvuma kuanzia Septemba 20 mpaka 23 na mgeni rasmi kwenye kilele chake ni Rais Samia. Tito Mbilinyi, mkazi wa Songea mkoani Ruvuma, anasema matamanio yao kwa miaka mingi ilikuwa kuona tamaduni zao zinaendelezwa, hivyo wanampongeza Rais Samia kwa kuliona hilo na kuruhusu kufanyika. “Mimi namshukuru sana Rais Samia kwa kutuletea tamasha hili, tulilisubiri sana, kwa hiyo tumefarijika sana,"anasema Mbilinyi.   Sisi kama wafanyabiashara tunasema hivi, karibu mgeni, mwenyeji apone, kwa sababu hata mwenye nyumba ya ku...

Mradi wa Ujenzi wa Tawi Jipya la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Katika Wilaya ya Bukoba Wafikia Asilimia Kumi

Na Angela Sebastian-Bukoba UJENZI wa tawi  jipya la Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia mradi wa elimu ya juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaoendelea mkoani Kagera umefikia asilimia 10 tangu uanze mwezi Julai mwaka huu. Mradi huo unajengwa katika kata ya Karabagaine Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ambapo, mradi utawezesha huduma ya elimu ya juu kuwafikia watu wengi katika maeneo ambayo ni nje ya mkoa wa Dar es Salaam. Akiongea na waandishi wa habari katika eneo unapojengwa mradi huo Naibu Mratibu wa mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk.Liberato Haule amesema walikabidhi mradi kwa mkandarasi mwezi Mei na ujenzi ulianza rasmi mwezi Julai mwaka huu ambao unajumuisha madarasa,kambi za mihadhara,ofisi za walimu na mabweni kwa ajili ya wanafunzi. "Kwanini tumeamua kuanzisha miradi hii ya ujenzi huu ni kuhakikisha tunasogeza zaidi huduma ya chuo kikuu cha Dar es Salaam kwenye maeneo ambayo ni nje ya Dar es Salaam na ambapo hatujawahi k...

Serikali kukamilisha ujenzi wa bweni katika chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi Misungwi

Chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi(CDTTI)Misungwi kinahitaji kiasi cha shilingi billioni 1.9 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la wasichana litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 352 Mkuu wa chuo cha hicho CHARLES ACHUODHO amebainisha hayo wakati wa ziara ya waziri wa maendeleo ya Jamii,Jinsia,wanawake na makundi maalum DKT.DOROTHY GWAJIMA. Achuodho amesema kuwa bweni hilo liko kwenye hatua ya msingi ambapo ujenzi wake tayari umeigharimu kiasi  shilingi millioni mia tatu. Mradi wa ujenzi wa bweni hilo unatarajia kugharimu  kasi cha shilingi billioni 2.2 na kukamilika kwake kutaondoa adha ya wanafunzi wa chuo hicho  hususani wa kike kuishi mtaani. Waziri GWAJIMA amekagua maendeleo ya ujenzi wa bweni hilo na kusisitiza dhamira ya serikali ya kukamilisha ujenzi wake. Katika hatua nyingne dkt gwajma amewataka maafisa maendeleo ya Jamii nchini kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2025. Pia amewaasa maafisa...