Skip to main content

Posts

Showing posts from July 10, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wananchi Sengerema Wampongeza Mbunge Hamis Tabasamu

Wananchi wa Jimbo la Serengema Mkoani Mwanza wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Tabasam kwa kufanikisha ujenzi wa shule 24 za sekondari kwa kipindi cha miaka minne ambapo awali kulikuwa na sekondari  sita tu kipindi cha mbunge aliyemaliza muda wake wa miaka 15 akiwa katika jimbo hilo. Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Hamis Tabasam kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa shule za sekondari  mpya tatu katika eneo la Igalagalilo, Chamabanda na Kasomeko ili kunusuru wanafunzi kutembelea umbali wa kilometa 16 kwenda shule za jirani.

Mativila Afurahishwa na Viwango vya Ujenzi wa Barabara za Lami Dodoma

Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amefurahishwa na viwango vya ujenzi wa miradi ya barabara za lami zinazosimamiwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Dodoma. Mhandisi Mativila ameyasema hayo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kukagua uimara wa barabara zinazosimamiwa na TARURA ambapo alitembelea miradi ipatayo nane. Alisema barabara zote hizo zimejengwa kwa fedha za tozo na mfuko wa maendeleo wa barabara ambazo hutolewa na serikali kwaajili ya kuboresha miundombinu ya barabara hususani maeneo ya mijini. “Nimefurahishwa na viwango vya barabara hizi ambazo zinasimamiwa na TARURA pamoja na makandarasi waliojenga barabara mkoani Dodoma, wamefanya kazi nzuri barabara zote zipo kwenye viwango vizuri hata wakazi wanaoishi jirani na barabara hizi unaona wanavyofurahia barabara hizi", alisema. Aliongeza kusema kwamba anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Sul...

Serikali Yawaagiza Wakuu wa Mikoa Kuwakamata Waganga wa Jadi Wanaofanya Ramli Chonganishi

Na Angela Sebastian-Muleba IKIWA zimepita siku 24 tangu yalilipotokea mauaji ya kikatili kwa mtoto mwenye ualbino marehemu Noela Asimwe Novart ( 2.5) katika kijiji cha Bulamula kata Kamachumu Wilayani Muleba mkoani Kagera, Waziri  wa nchi ofisi ya Waziri mkuu kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu Deogratias Ndejembi amewaagiza wakuu wa mikoa yote hapa nchini kufanya operesheni maalum nchi nzima. "Nawaagiza wakuu wa mikoa nchi nzima kufanya operesheni maalum ya kuwakamata waganga wa tiba asilia na tiba mbadala wanaojishughulisha na ramli chonganishi wasio na vibali  na kuwafikisha katika vyombo vya sheria,watu wenye ualbino wana haki ya kuishi kama mimi na wewe hivyo ukatili dhidi yao kwasababu ya tamaa havina nafasi "Ndejembi  Ametoa agizo hilo  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga ukatili kwa watu wenye ualbino uliofanyika katika kata ya Kamachumu Wilayani Muleba mkoani hapa . Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbiino Taifa (TASI) Alfre...

Jackline Mzindakaya Akabidhi Magodoro 30 Shule ya Elimu Maalumu Sumbawanga

Jackline Mzindakaya amekabidhi Msaada wa amekabidhi magodoro 30 katika Shule ya elimu maalumu Malangali na kumaliza changamoto ya watoto kulala chini shuleni hapo huko katika Manislaa ya Sumbawanga ikiwa ni kuunga juhudi za serikali katika kuboresha elimu na utoaji wa elimu bure. Amesema msaada huo ni kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Amesema ametoa msaada kwa utashi na upendo kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa hasa katika kusaidia kundi hilo lenye mahitaji maalumu. Jackline Mzindakaya ni binti wa aliyekuwa Mwanasiasa mkongwe nchini Mbunge wa Jimbo la Kwela wilayani Sumbawanga kwa miaka 45 Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya.

Makamu wa Rais Ataka Msukumo Utolewe Kwa Vijiji na Vitongoji Visivyo na Umeme

Makamu wa Rais, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango ambaye yupo katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo  mkoani Kigoma, ameiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa inatoa msukumo wa upatikanaji  umeme  kwa vijiji na vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo. Dkt Mpango ameyasema hayo Julai 9, 2024, wakati akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali mkoani Kigoma ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani humo. Akiwa katika Kata ya Kalinzi na Mnanila Jimbo la Buhigwe, Dkt. Mpango alisema kuwa, changamoto za umeme kwa sasa zinashughulikiwa vizuri ambapo  ameipongeza Wizara ya Nishati na watendaji kwa ujumla kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Sekta ya Nishati. Akijibu hoja mbalimbali wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, aliwaagiza TANESCO na REA kuhakikisha vijiji 5 vilivyokosa umeme kwenye Kata ya Kalinzi vinapatiwa umeme kwa kuanza na vijiji 3 ambavyo wakandarasi wako kwenye eneo la m...

Bilioni 34 Kujenga Kituo Cha Kisasa Cha Biashara Manyovu Kigoma

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 34 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha  (One Stop Boarder Post- OSBP) katika eneo la Manyovu ambapo ni mpaka wa nchi ya Tanzania na Burundi ili kuwezesha Mkoa wa Kigoma kufanya biashara na nchi jirani. Bashungwa ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Mnanira, Manyovu katika ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Kigoma. “Wizara ya Ujenzi tayari tupo katika hatua ya kumtafuta Mkandarasi wa kujenga kituo cha kisasa ndani ya nchi yetu ya Tanzania, bilioni 34 zimeshatengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi huo”, ameeleza Bashungwa. Bashungwa amefafanua kuwa Kituo hicho kitakuwa cha kisasa na kikikamilika kitasaida kuboresha biashara na kuwezesha Mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara kwa nchi yetu na nchi za jirani za Burundi na DRC Congo. Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Wizara ya Ujenzi itashirikian...