Skip to main content

Posts

Showing posts from March 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Prof Janabi yumo Kinyang'anyiro Cha Boss wa Who Kanda ya Afrika

 Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kupokea majina ya wagombea watano wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kwa Kanda ya Afrika akiwemo pia Prof. Mohamed Janabi ambaye anaiwakilisha Tanzania. Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya WHO Machi 14, 2025 inaeleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Duniani Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amepokea majina ya wagombea watano kutoka nchi wanachama wa WHO Kanda ya Afrika. Prof Janabi atachuana na Dkt N'da Konan Michel Yao kutoka Côte d'Ivoire, Dkt. Dramé Mohammed Lamine kutoka Guinea, Dkt. Boureima Hama Sambo kutoka Niger pamoja na Prof. Mijiyawa Moustafa kutoka Togo. WHO itaendesha tena uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika hivi karibuni kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika hilo kilichotokea Novemba 27, 2024.

Hoja ya Waziri Mkuu Majaliwa Kuhusu Veta "Imenyoka" Sana!

  George Michael Uledi! GAZETI la Mwananchi la March 16,2025 limebeba kichwa cha habari "Wasomi na VETA Mjadala Mkali"!Pia Jana mtandao wa Jamii Forum ulikuwa na mada kama hiyo kuhusu kauli ya Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa! Kwanza kabisa napenda kumpongeza Mh Waziri Mkuu kwa kutoa kauli ya kishujaa sana japo imekuwa "NGUMU kumeza" kwa "wasomi" wetu!Ukweli unabaki kuwa tatizo la ajira sio la Tanzania tu bali lipo Kenya, Uganda,Malawi Afrika Kusini na hata Marekani pia! Takwimu zinaonyesha kuwa sekta binafsi ndio mwajiri Mkuu Nchini Tanzania kwa sasa kuliko sekta ya Umma na "trend" hii itaendelea hivyo hivyo kwa miaka mingi ijayo!Sekta binafsi hasa katika "ubunifu" ndio itakuwa inazalisha ajira nyingi zaidi kuanzia sasa na kuendelea! Juzi nilikuwa nawaona Vijana wa (NETO) waalimu WASIO na AJIRA wakilumbana na Serikali ili iwapatie ajira!Je,vipi kuhusu makundi mengine yakija na madai kama hayo?Nikawa nawaza kwamba Serikali Ina uwezo kwa k...

Makamu wa Kwanza wa Rais Wa Zanzibar Hajui Itifaki Safari za Viongozi-Mbeto

   Mbeto amshangaa OMO kushindwa kuingia Angola  Na Mwandishi Maalum, Zanzibar  Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo CCM Zanz. Kamati maalum ya NEC Zanzibar imemshangaa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, kutojua itifaki za safari za viongozi na kujikuta akikwama kuingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Angola.  Pia idara hiyo imesema endapo Othman hajui hata utaratibu wa safari za nje , kushindwa kuujulisha ubalozi ,ni wazi hana uwezo wa kuwa Rais wa Zanzibar . Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Nec na Katibu wa Kamati Maalum ya Nec zanzibar ,Khmis Mbeto Khamis , aliyesema kiongozi huyo amelitia aibu Taifa akiwa ughaibuni  Mbeto alisema kutokana na wadhifa wake wa Makamo wa Kwanza wa Rais SMZ, alitakiwa kuaga kazini , kutoa taarifa Wizara ya Mambo ya Nje na kujulisha Ubolozi wa Tanzania Angola.  Aliongeza kusema taratibu hizo humfanya kiongozi wa Serikali kuanza kuandaliwa taribu za kiitifaki ,kiusalama na za ...

Balozi Nchimbi Achangisha Sh. 950 Milioni Kwa Matibabu ya Wagonjwa wa Mguu Kifundo

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amefanikisha uchangishaji wa shilingi milioni 950 kwa ajili ya matibabu ya watoto wapatao 400 wanaougua ugonjwa wa mguu kifundo. Kiasi hicho cha fedha kimepatikana kupitia ahadi za wadau mbalimbali walioshiriki hafla ya futari maalum kwa harambee hiyo, iliyofanyika Machi 14, 2025, katika Ukumbi wa Super Dome, Dar es Salaam. Harambee hiyo ililenga kukusanya shilingi milioni 600 kwa ajili ya matibabu hayo. Akifungua hafla hiyo kama mgeni rasmi, Balozi Nchimbi alisema tukio hilo ni sehemu ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameleta mafanikio makubwa katika sekta ya afya. “Siku chache zilizopita, Rais Dkt. Samia alitangazwa mshindi wa tuzo ya kimataifa kwa juhudi zake za kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto, na kuwa Rais wa kwanza barani Afrika kupata nishani hiyo,” alisema Balozi Nchimbi. “Shughuli yetu ya leo ni ishara ya k...

Kwa Kweli Ruangwa Hatuna Deni na Rais Dkt Samia-majaliwa

  Mbunge wa Jimbo la Ruangwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wakazi wa Wilaya ya Ruangwa hawana deni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa aliyoifanya wilayani humo. Amesema Rais Dkt. Samia ametoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta za kilimo, afya, elimu, miundombinu na nyinginezo. Ameyasema hayo leo (Jumamosi, 15 Machi 2025) wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wanakijiji wa kijiji cha Narungombe, Wilayani Ruangwa. "Rais Dkt. Samia amewezesha kupatikana kwa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo nchini ikiwemo kwenye wilaya yetu ya Ruangwa, Tunaachaje kumuunga mkono kwa kazi kubwa aliyoifanya." Amesema Wana-Ruangwa wanatoa shukrani za dhati kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyotoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo. "Wilaya yetu ilikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji kutokana na kuwa na chumvi nyingi chini in...

Mbunge Muhongo Kuanza Harambee Awamu Nyingine Ujenzi za Shule za Sekondari Jimbo la Musoma Vijijini

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amepanga kuanza kuendesha harambee awamu nyingine kuchangia ujenzi wa shule za sekondari. Awamu hii harambee hizo zitaanza kuanzia machi 25 hadi 27,2025 kwenye vijiji 3 vilivyoanza ujenzi wa shule. Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya mbunge iliyotolewa leo machi 15,2025 imeeleza harambee ya kwanza itafanyika Nyabakangara sekondari Kijijini Nyambono tarehe 25 machi 2025 kuanzia saa 8 mchana Harambee ya pili itafanyika Kataryo sekondari Kijijini Kataryo  tarehe 26 machi 2025 kuanzia saa 8 mchana na kumalizia Musanja sekondari Kijijini Musanja tarehe 27 machi 2025 kuanzia saa 8 mchana. Taarifa hiyo imeeleza lengo la Musoma Vijijini  ni kila Kijiji kiwe na shule za msingi za kutosha na kila Kijiji kiwe na sekondari moja na zipo sekondari mpya zitakazofunguliwa mwaka huu wa 2025 "Sekondari 3 zinazojengwa na serikali za vijiji vya Butata, Kasoma na Kurwaki na znazojengwa na wanavijiji 3 katika vi...

Wasira Azungumza na Wana Ccm Wilaya ya Mbozi

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Kanisani Vwawa Wilaya Mbozi mkoani Songwe akiwa katika ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025

Zaidi ya leseni 4,000 kutolewa Mbogwe

  - *Maeneo bado ni mengi watanzania waitwa* - *Fursa ujenzi wa mitambo, ununuzi wa dhahabu* - *Nyang’wale kinara ukusanyaji maduhuli ZAIDI ya leseni 4,000 zipo katika utaratibu wa kutolewa katika maeneo manne ya Mkoa wa Kimadini Mbogwe mkoani Geita, huku wazawa na wawekezaji kutoka nje wakitakiwa kuchangamkia fursa zilizopo mkoani humo. Akizungumza katika mahojiano, Afisa Madini Mkazi wa Mbogwe, Mhandisi Jeremiah Hango amesema maeneo yaliyotengwa ni Nyamikonze ambapo leseni 81 ziliweza kugawiwa kwa wachimbaji wadogo, kuna eneo la Mwamakiliga leseni 27 zilitengwa. “Maeneo mengine ni Bukombe kijijini leseni 140 na sasa hivi mchakato wa Kigosi ambapo takribani leseni 4,000 zimeweza kutengwa,”amesema Mhandisi Hango Amesema, zoezi la ugawaji bado  linaendelea na kwamba fursa zilizopo zikitumiwa vizuri serikali itaweza kukusanya kiasi kikubwa cha maduhuli. “Nawakumbusha wamiliki wa leseni ambao wameshikilia leseni katika mkoa wetu wa kimadini Mbogwe wazifanyie kazi leseni hizo, nyi...