Skip to main content

Posts

Showing posts from April 23, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Yaongeza Nguvu Kwa Wachimbaji Wadogo, Yasisitiza Usalama Migodini

Wakaguzi wakuu wa migodi watakiwa kupewa fursa zaidi kuimarisha usalama na utunzaji wa mazingira 📍KAHAMA Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuwawezesha Wakaguzi Wakuu wa Migodi pamoja na wachimbaji wadogo nchini ili kuimarisha usalama kazini, kulinda mazingira na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Wito huo umetolewa leo Aprili 23, 2026 wilayani Kahama, mkoani Shinyanga na Mkurugenzi wa Huduma za Leseni wa Tume ya Madini, Mhandisi Aziza Swedi, alipokuwa akifungua mafunzo kwa mameneja na Wakaguzi Wakuu wa Migodi ya uchimbaji mdogo kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo. Mafunzo hayo yanawakutanisha washiriki kutoka mikoa ya kimadini ya Kahama, Mbogwe na Shinyanga yakilenga kuimarisha uelewa wa kitaalam, usimamizi bora wa migodi, uzingatiaji wa sheria na kanuni pamoja na kukuza uchimbaji salama na endelevu. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mhandisi Swedi amesema Wakaguzi Wakuu wa Migodi wanapaswa kupewa ushiri...

Prof. Shemdoe Amshukuru Mhe. Rais Kutoa Fedha za Kutekeleza Miradi Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa

Na OWM - TAMISEMI, Arusha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia fedha nyingi kupelekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imepeleka tabasamu kwa wananchi kwa kuboresha utoaji wa huduma za kijamii. Prof. Shemdoe ametoa pongezi hizo Aprili 22, 2026 jijini Arusha kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika tarehe 22 hadi 23 Aprili, 2026 jijini humo. “Mhe. Waziri Mkuu, nichukue fursa hii kumshukuru sana Mhe. Rais kwa kuleta fedha nyingi  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zimetekeleza miradi mingi ya kimkakati, nakushukuru nawe pia kwani ukiwa Waziri wa Fedha uliwezesha upatikanaji wa fedha zote zilizoridhiwa na Mhe. Rais,” amesisitiza Mhe. Prof. Sh...

Government Steps Up Support for Small-Scale Miners, Stresses Mine Safety

📍KAHAMA, Shinyanga Region The Government has reaffirmed its commitment to empowering small-scale miners and strengthening the role of Chief Inspectors of Mines as part of broader efforts to enhance workplace safety, environmental protection and the mining sector’s contribution to national economic growth. The call was made today in Kahama District, Shinyanga Region, by the Director of Licensing at the Mining Commission, Engineer Aziza Swedi, while officiating the opening of a training programme for mine managers and Chief Inspectors of Mines drawn from small-scale mining operations. She represented the Executive Secretary of the Mining Commission, Engineer Ramadhani Lwamo. The training brings together participants from key mining areas of Kahama, Mbogwe and Shinyanga, with the aim of strengthening technical capacity, improving mine management practices, enhancing compliance with laws and regulations, and promoting safe and sustainable mining operations. Speaking during the opening ses...

Dhamira ya Serikali Yadhihirika; Lango Mamire Laanza Kupokea Watalii - Tarangire

Na. Jacob Kasiri - Tarangire. Dhamira ya serikali ya kukuza utalii na kufikisha watalii milioni nane (08) ifikapo 2030 sasa inaonekana kwa vitendo, baada ya lango la Mamire lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Tarangire kukamilika na leo Aprili 23, 2026, lango hilo limepokea mgeni mmoja kutoka Taifa la Australia. Hatua hii inafungua ukurasa mpya wa kiuchumi kwa jamii zinazozunguka hifadhi hiyo huku ikichagiza katika kukuza mapato, ajira na kuibua fursa za utalii wa kiutamaduni kwa mkoa wa Manyara hasa katika mji wa Babati. Akikata (permit) kibali cha kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa Tarangire kupitia katika lango hilo jipya, Bi. Cindy Snart alisema kuwa amefurahishwa na hatua ya TANAPA kufungua lango hilo, na hii itawarahisishia na kuwapunguzia watalii wengi mwendo kwa kutokea Babati mjini hadi lango la Mamire ambalo ni kilometa 21 tu. Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Tarangire Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George aliwasihi na kuwahimiza wenye Makapuni ya utalii na usafiris...

Mhandisi Seff Akagua Ujenzi wa Barabara za Uwanja wa Afcon Arusha

#Ataka kazi zikamilike ifikapo Mei 2027 Arusha Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara zinazoingia katika uwanja utakaotumika kwa mashindano ya AFCON jijini Arusha. Mhandisi Seff amesema kwamba ziara hiyo imelenga kujionea hatua za utekelezaji wa mradi wa barabara zenye urefu wa kilomita 21.4 ambapo kazi tayari zimeanza katika sehemu ya barabara ya Essuri. Amesema serikali imejipanga kuhakikisha miundombinu hiyo inakamilika kwa wakati na kuongeza kuwa maeneo ambayo bado hayajaanza yanasubiri kukamilisha taratibu za fidia kwa wananchi watakaoathiriwa na mradi huo huku mkakati ukiwa ni kuendelea kuzungumza nao ili kutoa ushirikiano na kuruhusu kazi ziendelee bila vikwazo. “Lengo la Serikali ni kuhakikisha barabara hizi zinakamilika ifikapo Mei mwaka 2027 ili ziwe tayari kabla ya mashindano ya AFCON,” amesema Mhandisi Seff. Aidha, amesema mradi huo unatekelezwa kwa utaratibu wa Sanifu...