Skip to main content

Posts

Showing posts from November 29, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Madaktari wa Tanzania Comoro waanza kambi kwa kishindo

Na Mwandishi Wetu, Comoro KAMBI Tiba ya Madaktari Bingwa kutoka Tanzania nchini Comoro imeanza kwa mwitikio mkubwa wa wananchi wa nchini humo ambapo mamia wamejitokeza kupata huduma mbali mbali zinazotolewa kwa ushirikiano na madakatari wazawa katika Kisiwa cha Ngazidja. Madaktari hao wa Tanzani wametoa huduma za uchunguzi na matibabu katika matatizo ya mifupa,figo na kibofu cha mkojo, mifupa, saratani, moyo na mengineyo ambapo takriban wagonjwa 417 wameandikishwa katika siku ya kwanza. Akizungumza katika kikao cha tathmini ya uendeshaji wa kambi hiyo inayoratibiwa Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Kaimu Mkuu wa Msafara, Dk Salehe Mwinchete alieleza kuwa ushirikiano waliopewa na madaktari wenyeji ni mkubwa na wananchi wa Comoro wamejitokeza kwa wingi na hilo limewatia moyo kuwa siku zinazofuata hali itakuwa bora zaidi. Naye Balozi wa Tanzania nchini Comoro aliwaaeleza madaktari hao kuwa Kambi Tiba hiyo imekuwa kivutio kikubwa na wananchi wen...

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yaendelea Kupungua Nchini

 Na. Aron Msigwa Songea, Ruvuma. Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amesema kiwango cha ushamiri wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini Tanzania kimepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003/2004 mpaka asilimia 4.4 mwaka 2022/23 kufuatia juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali na wadau wa Sekta binafsi.  Mhe. Mhagama ameyasema hayo leo Novemba 29,2024 mjini Songea, Ruvuma wakati akifungua kongamano la kitaifa la kisayansi na uzinduzi wa usambazaji wa ripoti ya utafiti wa viashiria na matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2022/23 ambapo amesema kiwango cha maambukizi pia kimepungua kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto kutoka asilimia 18 za mwaka 2010 hadi asilimia 8.1 mwaka 2023 hali inayoongeza usalama wa watoto. Leo tunazindua usambazaji wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI mwaka 2022 - 2023 katika Kongamano lililohusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini. Takwimu hizi zitasaidia makundi mbalimbali katika kupanga mipango ya maendeleo Amesema Mhe. Mhagama. Ameongeza...

Kambarage Wasira apongezwa Kufanikisha Ushindi wa Ccm

Baadhi ya wana CCM na wakereketwa wa chama hicho kata ya Nyasura wamempongeza kada wao Kambarage Wassira (Mmarekani)kwa kujitoa na kufanikisha ushindi mkubwa katika mtaa wa Zanzibar mjini Bunda mkoani Mara. Wakizungumza na GMTV baada ya kumalizika uchaguzi wa Serikali za mitaa,baadhi ya wananchi hao wamedai juhudi kubwa za kada huyo zimewezesha ushindi wa CCM katika mtaa huo Bunda mjini. Wamesema kulikuwa na figisu ambazo zilikuwa zikifanywa baadhi ya watu ndani na nje ya chama kwa kumpinga mgombea huyo mwana Mama Nyabaturi Ogola kitendo kilichomchukiza kada huyo na kuingilia kati kwa kupambana usiku na mchana hivyo kuwezesha ushindi huo wa CCM kwa kupata kura 586,huku Chadema ikipata kura 159 na NRA ikiambulia kura tatu Wananchi hao wamesema wanatambua mchango wa ndugu Kambarage Wassira katika ushindi huo na kwamba wanakiomba chama Chao kiangalia namba ya kutoa tuzo kwa makada wanaojitoa katika kukipigania chama wakati wa kutafuta dola.

Shule za Msingi 139 Mbinga Kupewa Kompyuta

Na Mwandishi Wetu, Ruvuma.  Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM), Mhe.Judith Kapinga ameahidi kutoa kompyuta 139 katika Shule za Msingi 139 zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini ili kuchochea kasi ya ukuaji wa Elimu katika wilaya hiyo. Mhe. Kapinga ametoa ahadi hiyo Novemba 28, 2024 wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Mbungani iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini. "Nitatoa kompyuta 139 ifikapo Januari 2025 ili zitumike katika Shule za Msingi 139 zilizopo Halmashauri ya Wilaya Mbinga Vijijini kwa lengo la kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo ya Elimu nchini."  Amesema Mhe. Kapinga Aidha, pamoja na kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Mbungani wilayani Mbinga, Mhe.Kapinga amechangia fedha ili kuongeza nguvu katika ujenzi wa nyumba hiyo. Akizungumza na Wazee wa Kijiji cha Kindimbajuu katika Halmashauri...

Mamlaka za Usafirishajj Majini Barani Africa Zatakiwa Kushirikiana Kutoa Huduma

  Na Lubango Mleka, Dar es Salaam.    Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri majini Barani Afrika zimetakiwa kushirikiana na kuungana ili kuimarisha usalama wa sekta ya usafirishaji majini na hivyo kuchochea maendeleo ya Uchumi katika nchi husika. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Novemba 29, 2024) wakati akifungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi na Usafirishaji Majini Barani Afrika unaofanyika kwa siku tatu, Jijini Dar es Salaam. Dkt. Biteko amewashauri washiriki kutumia mkutano huo kama fursa ya kubuni na kupanga mikakati mipya ya kuelekea katika mafanikio kupitia sekta hiyo ambapo amesisitiza kuwa ushirikiano miongoni mwa washiriki na kujadiliana juu ya kuwezesha masuala mbalimbali na sekta ya usafirishaji ndio suluhisho la changamoto mbalimbali zilizopo. “Kila mmoja wetu atumie fursa ya mkutano huu kujiwekea malengo yatakayo tuwezesha kufikia azma ya kuboresha usalama na kuima...

Rais Samia amesimama na Viongozi wengine kumkumbuka Ndugulile

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Viongozi wengine kwa ajili ya kumuombea aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Marehemu Dkt. Faustine Ndungulile aliyefariki dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu, wakati wa Kikao Kazi kilichofanyika Ikulu ndogo Arusha tarehe 29 Novemba, 2024.

Mamlaka za Usafirishaji Majini Barani Afrika Zatakiwa Kushirikiana Kuboresha Huduma

*📌 Dkt. Biteko afungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa 7 wa AAMA* *📌 Awataka washiriki kubuni mbinu za kukabili changamoto zilizopo* *📌 IMO yaahidi kuendeleza ushirikiano kukabiliana na changamoto Bahraini* *📌 Dar es Salaam yampongeza Rais Samia kuboresha Bandari, kupunguza msongamano* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri majini Barani Afrika zimetakiwa kushirikiana na kuungana ili kuimarisha usalama wa sekta ya usafirishaji majini na hivyo kuchochea maendeleo ya Uchumi katika nchi husika. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Novemba 29, 2024) wakati akifungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi na Usafirishaji Majini Barani Afrika unaofanyika kwa siku tatu, Jijini Dar es Salaam. Dkt. Biteko amewashauri washiriki kutumia mkutano huo kama fursa ya kubuni na kupanga mikakati mipya ya kuelekea katika mafanikio kupitia sekta hiyo ambapo amesisitiza k...