Skip to main content

Posts

Showing posts from June 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MwanaFA aitaka UVCCM iwaunge mkono vijana wenye kesho nyingi kuliko jana

📍Asema anaheshimu mchango aliopewa na vijana kwa ajili ya fomu 📍 UVCCM wampa fedha za kuchukua fomu, wamuahidi kumuunga mkono Na Mwandishi Wetu, Muheza NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA awewataka vijana kuwa makini katika upigaji wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhakikisha wanachagua wagombea wenye kesho nyingi kwa ajili ya kusaidia kuleta maendeleo wilayani Muheza. Akizungumza kwenye Kambi ya vijana iliyofanyika shule ya sekondari Chief Mang'enya, MwanaFA ambaye pia ni mbunge wa Muheza alisema kuelekea upigaji wa kura za maoni ni vizuri vijana wakawaunga mkono wagombea wataoivusha CCM  katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba. "Kundi hili kama Kila kitu kitakaa sawa na rehema ya mungu, lina kesho nyingi kuliko jana, linatakiwa kuunga mkono vijana wenzao wenye kesho nyingi kuliko kuunga mkono wenye jana nyingi kuliko kesho chache na wana jana nyingi ambazo hawakujali mambo yetu," alisema. Alisema amefurahi k...

Kamishna Kuji,Awapiga Msasa Maafisa na Askari Uhifadhi Tanapa Kuelekea Msimu Mpya wa Utalii

Na. Edmund Salaho/Kitulo Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji leo tarehe 24 Juni, 2025 amefanya kikao kikazi na Maafisa na Askari wa Hifadhi ya Taifa Kitulo iliyopo mkoani, Njombe. Katika kikao kazi hicho Kamishna Kuji amewataka Maafisa na Askari kujipanga vilivyo katika kufanya kazi hasa katika msimu huu mpya wa utalii ambao unakwenda kuanza mwezi Julai 2025 ili kuhakikisha mapato ya Serikali yanakusanywa kikamilifu. “Ni fahari kubwa kwetu TANAPA kushiriki kuchangia katika ujenzi wa Taifa letu kupitia uratibu na usimamizi wa shughuli za utalii katika hifadhi za Taifa na maeneo ya Malikale yaliyokasimiwa kwa TANAPA. Mafanikio hayo ni matunda ya kila mmoja wetu katika kuhifadhi maliasili hizi tulizokabidhiwa kuzitunza kwa niaba ya Watanzania. Mpaka siku ya jana 23.06.2025 Shirika limeweza kukusanya shilingi billioni 480 ikiwa imesalia shilingi 20 kufikisha nusu trillioni” alisema Kamishna Kuji. ““Bodi ya Wadhamini ya Shirika imenituma niwahakikishie ushirikiano wa kutosha “ful...

Edwin Soko asema Serikali kujitokeza na kujibu ongezeko la deni la Taifa ni ukomavu wa kiuongozi

" Mheshimiwa spika Serikali haikopi Kwa ajili ya kulipa mishahara au posho bali inakopa kwa ajili ya kufanya maendeleo, hivyo kasi ya  kukopa inaendana na Kasi ya maendeleo Nchini"  Hayo yamesemwa na  Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba Bungeni Leo Juni 24, 2025 alipokuwa anatoa ufafanuzi juu ya kuongezeka kwa deni la Taifa lililofika Trlioni 107.7. Waziri Nchemba katika kutoa msisitizo wake mbele ya wabunge juu ya nia chanya  ya Serikali ya kukopa alieleza kwa kutolea mfano wa trilioni 27 za ujenzi wa reli ya mwendo kasi (SGR) Kwa uelekeo wa Mwanza na Kigoma kwa kusema maendeleo kama hayo hayawezi kusubiri miaka arobaini ndipo yakamilike bali mpango sahihi ni kukopa na kujenga kwa muda mfupi na kukusanya faida na kulipa deni. Nchemba pia alisisitiza kuwa, ukopaji mwingine  pia ulifanyika kwenye ujenzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, ambapo Kwa sasa watanzania wengi wananufaika na chuo hicho, ikiwemo Utekelezaji wa dhamira ya sera ya elimu ya kuboresha miundombinu ya kujifu...

Balozi Nchimbi Awasili Arusha

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akipokewa na viongozi wa chama na serikali, wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndugu Dadi Musa Matoroka (kulia pichani) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paul Makonda, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kisongo Arusha. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha mjini, Dkt. Wilfred Soileli na Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha mjini, Timothy Sanga. Katibu Mkuu Balozi Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Wanawake Arusha 2025, litakalofanyika jijini humo, siku ya Jumanne, tarehe 24 Juni 2025.

Balozi Nchimbi: Maoni Yoyote Kuhusu Amani ya Tanzania Hayatapuuzwa

_Awahakikishia viongozi wa dini, taasisi za kijamii na kimila_ _Awapongeza wanawake kusimamia amani_ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa maoni yoyote yanayolenga kuhakikisha Tanzania inaendelea kudumisha amani na utulivu, hayajawahi kupuuzwa na hayatapuuzwa. Aidha, Balozi Nchimbi amemwelezea Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ni kiongozi mwanamke ambaye uongozi wake, umeongeza heshima kubwa kwa wanawake na Tanzania, akiendeleza safari iliyoanzishwa na viongozi wengine wanawake jasiri, tangu wakati wa kudai uhuru na kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia. Balozi Dkt. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akifungua Jukwaa la Wanawake wa Arusha 2025, lililowakutanisha wanawake katika kujadili maada ya ‘Safari ya Mwanamke Arusha 2025’, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), jijini Arusha, Jumanne, tarehe 24 Juni 2025. “Hivyo ndivyo wanawake wanalitazama taifa letu ...

Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Mitambo 10 ya Uchorongaji Kwa Wachimbaji Wadogo

✅️ *Asisitiza dhamira ya Serikali kuwainua wachimbaji wadogo kiuchumi* ✅️ *Mitambo Yagharimu shilingi bilioni 12.41* ✅️ *STAMICO yasaini mkataba wa ushirikiano na VETA* 📍 *Dodoma,* Katika mwendelezo hatua za Serikali kuendelea ya kuimarisha sekta ya wachimbaji wadogo nchini, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amezindua rasmi mitambo 10 ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo yenye thamani ya shilingi bilioni 12.41 iliyonunuliwa na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) sambamba na vitendea kazi vya Shirika hilo kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Shirika. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo Juni 24, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa madini, wachimbaji pamoja na wananchi. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuwawezesha wa...

Majaliwa Azindua Mitambo Ya Shilingi Bilioni 12.4 Kwa Ajili ya Wachimbaji Wadogo

  _▪️Ni kwa ajili ya uchorongaji na utafiti wa madini._ _▪️Asema ni mwendelezo wa juhudi za Rais Dkt. Samia kuboresha shughuli za wachimbaji wadogo_▪️ _▪️Atoa wito kwa wachimbaji wadogo kuuza madini ndani ya nchi_▪️   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mitambo kumi ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini yenye thamani wa shilingi bilioni 12.41 kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambayo itapunguza changamoto za wachimbaji wadogo ya kufanya uchimbaji bila kuwa na taarifa za kijiolojia. Akizungumza baada ya uzinduzi huo uliofanyika leo Jumanne (Juni 24, 2025) kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha shughuli za wachimbaji wadogo wa madini na kuwawezesha kuongeza uzalishaji. “Oktoba 2023 Rais Dkt. Samia, alizindua mitambo mitano ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Kutokana na wingi wa wachimbaji wadogo nchini na mwitikio chanya wa wachim...

Chuo Kikuu Mzumbe, GEL kushirikiana fursa za elimu ya juu

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Mzumbe cha mkoani Morogoro  na Wakala wa Elimu Nje ya Nchi (Global Education Link), wamesaini Mkataba wa Ushirikiano (MoU) kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa fursa za elimu nje ya nchi. Mkataba huo ulisainiwa jana katika ofisi za GEL jijini Dar es Salaam baina ya Mkurugenzi Mkuu wa GEL Abdulmalik Mollel na Makamu Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Mzumbe, Profesa William Mwegoha. Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa GEL, Mollel alisema lengo la makubaliano hayo  ni kuongeza ufahamu kwa wanafunzi na wahadhiri wa chuo hicho kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kimataifa. Alisema GEL imetengeneza mfumo kidijitali wanaoutumia kufuatilia na kupata taarifa mbalimbali za vyuo vikuu nje ya nchi pamoja na kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi wanaowapeleka nje ya nchi. Alisema GEL imekuwa ikiwaambia wanafunzi wanaokwenda nje ya nchi mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya safari, wakati wa safari na hata baada y...