Skip to main content

Posts

Showing posts from September 16, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Ahimiza Usimamizi wa Maadili Mema Kwa Jamii

Asema lengo ni kuepusha uovu na kuchochea maendeleo WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla wahakikishe wanasimamia na kuimarisha maadili mema kwa jamii ili kuepuka maovu na kuleta maendeleo endelevu kwa Watanzania. “Nitumie fursa hii kuendelea kutoa rai kwa wananchi, wazazi na viongozi wa dini kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wetu katika ngazi zote kwa kuzingatia maadili na tamaduni ya Taifa letu. Ni wajibu wetu kama wananchi” Amesema hayo leo (Jumatatu, Septemba 16, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Baraza la Maulid Kitaifa lililofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu, Mkoani Geita. Amesema kuwa viongozi wa dini wana jukumu la kutoa mwongozo na malezi ya kiroho kwa waumini kwa kuwa wana nguvu kubwa ya kuhamasisha maadili na tabia nzuri. “Wazazi, ninyi mna jukumu la msingi katika kulea watoto wenu kuanzia katika ngazi ya familia ili kujenga tabi...