Skip to main content

Posts

Showing posts from April 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (Mif) Yakabidhi Sanitary Pads 350 Kwa Wasichana Walio Kwenye Mazingira Magumu

Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) leo tarehe 18 Aprili, 2025 imekabidhi Taulo za Kike (Sanitary Pads) 350 kwa Wasichana walio katika mazingira magumu nyakati za hedhi husababisha changamoto kubwa kwa wasichana kuhudhuria masomo yao. Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) Mhe. Sabra Ali Mohamed amekabidhi Taulo za kike (Sanitary Pads) 350 kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Zanzibar Ndugu Siti Abasi Ali, ili kuweza kugaiwa kwa Madawati ya Jinsia ambayo yapo kwenye masoko na bandari na Dahalia za Shule zilizopo Pemba.  Vilevile, Mhe. Sabra Ali Mohamed amekabidhi Taulo 150 kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) - Zanzibar ili kuweza kugaiwa kwa Shule za Mikoa yote ya Unguja. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za MIF zilizopo Mazizini - Unguja.

Tuwajengee Uwezo Wana-ccm Kujibu Hoja za Wapinzani -Sagini

📍JIMBONI BUTIAMA *Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini* ameeendelea na Ziara ya kusikiliza na Kutatua kero za wananchi Kata ya Buswahili ambapo amewataka wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kujibu hoja za wapinzani kwa kuwaonesha maendeleo yaliyofanywa na Rais, Mbunge na Diwani. Mbunge Sagini amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kuna watu watapita na kupinga kuwa viongozi waliopo madarakani hawajafanya maendeleo ili wapate nafasi ya kujinadi wao hata uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi pia, hivyo ndio muda wa kuwaaambia kilichofanyika kuanzia ngazi ya shina mpaka Taifa. "Hata uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi utashangaa kuona baadhi ya wananchama wanaotaka nafasi wanaanza kupinga na kubeza kazi zilizofanyika kipindi hiki kwa lengo la kupata nafasi muwaambie kuwa miradi ya mabilioni imeingia Kata ya Buswahili na utekelezaji umeonekana na vingine vimetekelezwa kwa pesa binafsi za mbunge muwaoneshe Barabara,...

Rpc Mara Atoa Angalizo Kwa Watumiaji wa Barabara Kuelekea Sikukuu ya Pasaka

Na Shomari Binda-Musoma  KAMANDA waPolisi mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Pius Lutumo ametoa angalizo kwa watumiaji wa barabara kuwa makini na waangalifu katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka. Akizungumza na GMTV kwa njia ya simu leo aprili 18,2025 kuelekea sikukuu hiyo amesema kila mtumiaji wa barabara wakiwemo madereva na watumiaji wengine kuongeza umakini ili kuepuka ajali. Amesema madereva wa magari,pikipiki na vyombo vingine vya moto wasitumie pombe wanapokuwa wanaendesha kwani ni kisababishi cha ajali. Kamanda Lutumo amesema jeshi la polisi limeimalisha ulinzi na litawachukulia hatua kali wale wote watakaokamatwa kwa kwenda kinyume na matumizi sahihi ya barabara. Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mara amewasisitiza madereva kuacha miemko na kuwajali watumiaji wengine wa barabara ili washerehekee sikukuu kwa amani. Amesema chanzo cha ajali nyingi imekuwa ni pamoja na uzembe na matumizi ya vileo na kupelekea vifo na ulemavu na kupoteza nguvu kazi ya ...

Shule Mpya nne Kufunguliwa Mwezi Huu Jimbo La Musoma Vijijini

Na Shomari Binda-GMTV SHEREHE za ufunguzi wa shule mpya 4 za sekondari zinatarajiwa kufanyika jimbo la Musoma Vijijini kuanzia aprili 24 hadi 29,2025 huku wanafunzi,walimu,wazazi na wadau wa elimu wakikaribishwa. Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amewakaribisha na kudai hilo ni tukio muhimu na kubwa kwa maendeleo ya elimu. Akizungumza na GMTV leo ijumaa aprili 18,2025 Muhongo amesema ratiba itaanzia Butata sekondari iliyopo Kijijini Butata Kata ya Bukima siku ya alhamisi aprili 24,2025 kuanzia saa 6:30 mchana mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka. Amesema ijumaa aprili 25 itakuwa ratiba ya sekondari ya Kumbukumbu ya David Massamba Kijijini Kurwaki Kata ya Mugango kuanzia saa 6:30 mchana Muhoji sekondari iliyopo Kijijini Muhoji Kata ya Bugwema itafunguliwa Jumatatu aprili 28 kuanzia saa 6:30 mchana huku Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi akiwa mgeni rasmi Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na mbunge huyo Nyamrandirira sekondari ya Amali ili...

Bilioni 13.46 kuleta Mageuzi ya Kilimo cha Umwagiliaji, Mangalali

 📍NIRC, Iringa  Tume ya taifa ya Umwagiliaji (NIRC), imefanya makabidhiano ya mradi wa ujenzi miundombinu ya Umwagiliaji, wenye thamani ya shilingi bilioni 13.46, katika kijiji cha Mangalali, kata ya Ulanda mkoani Iringa.  Mradi huo unalenga kuboresha kilimo kwa wakulima zaidi ya 500, ambao sasa wataweza kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa wingi na kwa tija. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Herry James ameipongeza serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa juhudi za utekelezaji wa miradi ya Umwagiliaji mkoani humo. Amesema, mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka 2025, utajumuisha ujenzi wa miundombinu muhimu kama mifereji ya zege yenye urefu wa kilomita 5.356, mfereji wa upili wa kilomita 1.812, barabara za mashambani za kilomita 7.170, pamoja na ofisi ya umwagiliaji ya mkoa na nyumba ya makazi ya meneja wa skimu.  “Mageuzi haya ya kilimo katika skimu hii ni kwa ajili ya vijana ambao ni nguvu kazi ya Tai...