Skip to main content

Posts

Showing posts from September 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAITARA:JKT NI MUHIMU KUWAANDA VIJANA KUKABILIANA NA MAISHA

  Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini na mzazi wa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mwita Waitara, amelipongeza Jeshi hilo kwa kuendelea kuwajenga vijana katika misingi ya uzalendo, nidhamu, uwajibikaji na kujitegemea, akisema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa katika kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za maisha. Waitara ameyasema hayo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, Operesheni Linda Amani na vijana waliojitolea, iliyofanyika katika Kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mlandizi, mkoani Pwani, ambapo amesema vijana wanaomaliza mafunzo hayo wanapaswa kutumia ipasavyo maarifa na stadi walizopata ili kujiajiri, kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwa raia wema wenye mchango kwa Taifa. Aidha, Waitara amehimiza matumizi sahihi ya teknolojia ya Akili Bandia (AI) katika kuwaandaa vijana kwa mazingira ya sasa, akisema teknolojia hiyo inaweza kutumika kuwaongezea maarifa na stadi mbalimbali zitakazowasaidia kukabiliana na mahit...

OFISI ZINAZOTEMBEA ZA TRA ZINAVYORAHISISHA HUDUMA KWA WANANCHI

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatekeleza kwa vitendo mkakati wake wa kuwahudumia wananchi kwa kuhakikisha wanawapatia huduma bora na kwa urahisi kule walipo. Katika kutekeleza hilo, Februari 25, 2026, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Omar, akishirikiana na Kamishna Mkuu wa TRA, CPA Yusuph Mwenda, walizindua ofisi zinazotembea (mobile offices) Jijini Dar es Salaam ambazo ni magari yenye maofisa wa TRA na vifaa vya kazi, tayari kwa kuwahudumia wananchi. Kupitia ofisi hizo zinazotembea, maofisa hao wamekuwa wakiwafikia wateja na wananchi kwa kuwapa elimu na ushauri wa masuala ya kodi. Pia kufanya usajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN). Huduma nyingine ni kupata leseni za udereva, kutoa makadirio na namba za malipo ya kodi. Pia, wananchi wanapata elimu na ufafanuzi kuhusiana na mabadiliko ya sheria mbalimbali za kodi yaliyofanyika katika mwaka wa fedha 2026/2027. Kimsingi, ofisi hizo zimekuwa na manufaa kwani zinawafikia wananchi kule wal...

AWESO CUP 2026: JUKWA LA KUKUZA VIPAJI NA UWEKEZAJI PANGANI

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA  Michezo ni sekta muhimu inayotoa ajira kwa vijana wengi duniani. Kutokana na hilo, mipango madhubuti huwekwa ili kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia michezo na kuchangia maendeleo ya nchi. Tanzania si kisiwa. Kwa namna michezo ilivyobadili hali za maisha za watu wengi, hatuna budi kuipa msukuma sekta hiyo muhimu ili vijana wengi waweze kupata kipato. Mbunge wa Jimbo la Pangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameipa kipaumbele sekta ya michezo Jimboni kwake. Aidha, amedhamiria kutumia michezo kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara zinazopatikana wilayani Pangani ili wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wazitumie katika kukuza maendeleo. Kwa miaka mingi, Aweso amekuwa mfadhili wa mashindano mbalimbali ya michezo ili kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana. Mei 16, 2026, Aweso alikuwa Mgeni Rasmi wa fainali ya mashindano ya Aweso Vijana Cup, yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Ma...

KIKWETE, SASAKAWA WAZUNGUMZIA UCHUMI WA BULUU, USALAMA WA CHAKULA

 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amekutana na kufanya mazungumzo na Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Sasakawa Peace Foundation ya Japan, Bw. Masanori Kobayashi, katika ofisi yake ndogo iliyopo Masaki, Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalilenga kufuatilia utekelezaji wa masuala yaliyoibuliwa wakati wa ziara ya kikazi iliyofanywa na Dkt. Kikwete nchini Japan kuanzia tarehe 23 hadi 24 Julai 2025. Katika ziara hiyo, Dkt. Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri sita kutoka Afrika walioalikwa na Serikali ya Japan kupitia taasisi za Sasakawa Peace Foundation na Nippon Foundation. Viongozi hao walishiriki katika kutoa ushauri kuhusu namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Japan chini ya mwavuli wa Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD). Mkutano wa tisa wa TICAD ulifanyika baadaye jijini Yokohama, Japan, kuanzia tarehe 20 hadi 22 Agosti 2025. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Kikwete aliishukuru Serikali ya Jap...