Na Mwandishi Wetu NDOTO za vijana wa Tanzania wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi kwa mwaka wa masomo 2026/2027 zimeingia hatua muhimu baada ya Global Education Link kuwakutanisha wanafunzi hao pamoja na wazazi na walezi wao kwa ajili ya kuhakiki nyaraka na kukamilisha maandalizi ya safari. Kikao hicho kilichofanyika katika Makao Makuu ya Global Education Link, Dar es Salaam, kililenga kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa na nyaraka sahihi, taarifa za kutosha na maandalizi muhimu kabla ya kuondoka nchini kwenda kuanza masomo. Miongoni mwa mambo yaliyopitiwa katika kikao hicho ni pamoja na nyaraka za visa, barua za udahili, fomu za uthibitisho wa malazi, maandalizi ya safari pamoja na maelekezo ya namna ya kuishi na kusoma katika mazingira mapya nje ya Tanzania. Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, alisema lengo kuu la kikao hicho ni kuhakiki na kukamilisha nyaraka muhimu za wanafunzi, kujibu maswali ...
Marato tv - Sauti ya Jamii