Skip to main content

Posts

Showing posts from February 27, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Akiwasalimia Watangulizi Wake Katika Mazishi ya Kardinali Pengo

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 28, 2026 anaungana na waombolezaji kushiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo inayofanyika katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria - Pugu Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anaongoza waombolezaji katika mazishi.

Makamu wa Rais Awasili Eneo Atakalozikwa Kardinali Pengo

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria - Pugu Jijini Dar es Salaam, ambapo anaungana na waombolezaji kushiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Tarehe 28 Februari 2026.

Rock Block Mine Generates Sh400 Million In Government Revenue, Creates 122 Jobs

📍Rombo, February 28, 2026 The Rock Block mine in Rombo District, Kilimanjaro Region, is fast emerging as a catalyst for transformation in Tanzania’s building materials sub-sector, having generated 122 jobs and contributed more than Sh400 million to government revenue within three years of operation. Acting Kilimanjaro Resident Mines Officer, Engineer Abel Madaha, said in an exclusive interview in Rombo that the extraction and carving of rock for building materials form part of the government’s broader strategy to regulate, develop and add value to industrial and building material resources. He noted that the mine has continued to boost public revenue through fees, royalties and various taxes remitted to institutions, including the Tanzania Revenue Authority (TRA) and the Rombo District Council, thereby stimulating economic growth in Rombo and the Kilimanjaro Region at large. According to Engineer Madaha, the rocks extracted in Holili originated from ancient lava flows from Mount Kilim...

Ra yaendea na uhamasishaji ya miradi ya nishati vijijini Mara

  📌 *Wananchi wahamasika kujiunga na huduma ya umeme* . 📌 *Wananchi waunga mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia* . 📍 *Mara*  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na ziara ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Mara. Uhamasishaji umehusisha utoaji wa elimu kwa wananachi namna ya kufanya maombi ya kujiunga na huduma ya umeme huku lengo kuu likiwa ni  kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.  Aidha, Wakala umefanya Kampeni zinahusisha utoaji wa elimu kuhusu umuhimu na faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utunzaji wa afya, mazingira pamoja na usawa wa kijinsia.  Aidha, Wakala umetoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi bora  ya umeme hususani katika shughuli za uzalishaji ikiwemo shughuli za biashara, kilimo, na shughuli za nyumbani. Vile vile, Wakala umetoa elimu kuhusu taratibu r...

Ziara ya Waziri Mkuu Yaibua Madudu Arusha

*DC atoa siku tatu watoto wa bweni warejeshwe makwao ZIARA ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba jijini Arusha imewazindua watendaji na kujikuta wakibaini ujenzi wa shule ya ghorofa usio na vibali na watoto kulazwa katika bweni wakati ujenzi ukiendelea kwenye ghorofa hizo. Hayo yamebainika leo (Ijumaa, Februari 27, 2026) wakati Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude na Kamati ya Usalama ya Wilaya walipofanya ziara kwenye shule ya Nariva Hill na kufanya ukaguzi katika madarasa, mabweni, jikoni na eneo wanalojenga ghorofa juu ya bweni lililokuwa linatumika. Katika ziara hiyo shuleni hapo ambayo ilikuwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, viongozi hao walibaini kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi wa kike wanaolala katika bweni la muda ilhali hawana vyoo wala mabafu kwenye ghorofa yao. Pia walibaini baadhi ya watoto wanalala wawiliwawili kwenye kitanda kimoja. “Yale mabweni sikuona standards za Wizara ya Elimu, kuanzia leo natoa muda wa siku tatu tu kwa sababu hawa watoto wana kwao; kw...

Dkt. Mwigulu Ashiriki Ibada ya Kuaga Mwili wa Kardinali Pengo

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 27, 2026 ameshiriki ibada ya kuaga mwili wa Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliongoza waombolezaji katika tukio hilo.