Skip to main content

Posts

Showing posts from July 19, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Kuzindua Uboreshaji Wa Daftari La Kudumu La Wapiga Kura

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 20, 2024 anazindua uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, katika uwanja wa Kawawa, mkoani Kigoma. Uzinduzi huo unaashiria kuanza kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchini nzima. Mikoa ambayo inaanza uboreshaji wa daftari hilo leo Julai 20, 2024 hadi  Julai 26, 2024 ni Kigoma, Katavi na Tabora na baadaye mikoa mingine itafuata. KauliMbinu ya uboreshaji ni: Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora.

Jamhuri ya Indonesia Kuendelea Kuwekeza Tanzania

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo, ameeleza kuwa  Jamhuri ya Indonesia itaendelea kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali.  Mhe. Nyongo amesema hayo, Julai 19, 2024, wakati Mhe.alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe. Pahala Mansury, ambaye alifika nchini kuzungumza juu ya mashirikiano na Tanzania, miongoni mwa hayo ilikuwa ni kuikaribisha Tanzania kwenye Kongamano la Biashara kati ya Indonesia na nchi za Afrika (Indonesia - Africa Forum) linalitegema kufanyika 1-3 Septemba, 2024 nchini Indonesia Mhe. Nyongo amethibitisha Tanzania  kushiriki katika kongamano hilo na wamejadili  masuala ya uwekezaji wa Indonesia katika sekta mbalimbali nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kilimo, nishati safi, mitandao, viwanda, na miundombinu. Mhe. Nyongo aliongeza kuwa kampuni moja kutoka Indonesia ipo tayari kutekeleza mradi mkubwa wa uzalishaji wa mbolea inayotokana na gesi hapa nchini, mradi ambao utakuw...

Shilingi Bilioni 83.1 Zatumika Katika Utekelezaji wa Mradi wa Uendelevu-SRWSS

Mratibu wa Mradi wa Uendelevu wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSS) kutoka TAMISEMI  Hayo yamesemwa na Seleman Yondo, wakati wa kikao Kazi kilichofanyika Mkoani Morogoro ambapo amesema mradi huo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 umepokea jumla ya Tsh. 83.1Bil kwa ajili ya utekelezaji wake huku eneo la Afya ikitumia shilingi Bil. 54.39 na ujenzi wa miundombinu ya Elimu ikitumia shilingi Bil. 28.73 Amesema mradi unatekelezwa katika mikoa yote 25 ya Tanzania bara na Halmashauri 137, huku akiweka bayana kuwa Manispaa, miji na majiji sio sehemu ya mradi huu.  kikao kazi hicho kimewahusisha waganga Wakuu wa Mikoa na Maafisa Afya wa Mikoa yote Tanzania Bara lengo likiwa ni kujitathmini juu ya utekelezaji wa Mradi huo. Amesema mpaka sasa mradi wa SRWSS umefikia vituo vya kutolea huduma za Afya 2,727 na shule za Msingi 1,842, kwa mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 838 na shule 566 vimepokea fedha za utekelezaji. Kwa upande wake Mwakilishi ...

Mbunge Mathayo Awashauri Bodaboda Musoma Kufanya Kazi Kwa Ushirikiano

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Mhe. Vedastus Mathayo ametoa wito na kushauri bodaboda wanafanya shughuli zao maeneo ya utoaji wa huduma za afya Manispaa ya Musoma Kufanya Kazi kwa ushirikiano Mhe Mathayo ameyasema  hayo alipokuwa akizungumza na bodaboda wanaopaki kwenye hospital ya manispaa Musoma katika ziara yake ya mtaa kwa mtaa. Amesema ameshangaa kusikia Bodaboda hao wanapopeleka abiria kwenye hospital ya rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kwangwa wanazuiliwa kupaki na kuondoka na abiria huku wote wanatoa huduma kwa jamii hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na kupendana Mathayo amesema sio vyema kubaguana kwa kuwa shughuli yao ni moja na yule anayepaki hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anaweza kupaki hospital ya manispaa ya Musoma. " Nimesikia hii changamoto ni jambo la kuzungumzika na kazi ikafanyika kwa kushirikiana kwa kuwa wote mnafanya kazi kwa wananchi wetu. Nimempigia simu mganga mfawidhi pale hospital ya Kumbukumbu ya Mw...

Waziri Mkuu Atoa Wito Kwa Taasisi Za Dini Kuendelea Kushirikiana na Serikali

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za dini nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa mchango kwenye maendeleo ya taifa.  Amesema kuwa taasisi za dini zina uwezo mkubwa wa kutoa huduma imara za kiroho na kugusa maisha ya watu katika jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kisiasa. Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Julai 19, 2024) kwenye Kilele cha Mkutano wa  Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (CPCT), uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Biblia Miyuji jijini Dodoma. “Tuna kila sababu ya kuyashukuru Makanisa kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi kwa ujumla, yamekuwa sehemu ya suluhisho katika changamoto za kijamii kama vile umaskini, elimu duni, na matatizo ya kiafya” “Nitumie fursa hii kusisitiza taasisi za dini kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali na kuendelea kuiishi kwa vitendo kaulimbiu yenu ya Palipo na Umoja, Bwana huamuru baraka! Bwana huamuru baraka, palipo na Um...