Skip to main content

Posts

Showing posts from September 20, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MBEGU, MAGONJWA NA TABIANCHI: TCB NA TARI ZATAFUTA MAJIBU

 MWANZA.  Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika tafiti za zao la pamba, kwa lengo la kupata suluhisho za kisayansi na kiteknolojia zitakazosaidia kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima. Makubaliano hayo yamefikiwa katika kikao kati ya Menejimenti ya TCB na TARI kilichofanyika Septemba 18, 2026 katika Ofisi za Bodi ya Pamba Tanzania, Makao Makuu jijini Mwanza. Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Mhandisi Godwin Makori, amesema utafiti unapaswa kuelekezwa zaidi katika changamoto zinazowakabili wakulima, huku matokeo yake yakifikishwa kwa wakati kwa mtumiaji wa mwisho. “Moyo wa maendeleo ya nchi ni utafiti, lakini thamani ya utafiti inaonekana pale matokeo yake yanapomfikia mtumiaji wa mwisho na kutatua changamoto aliyonayo,” amesema Mhandisi Makori. Amesema maeneo yanayohitaji kupewa kipaumbele katika tafiti za pamba ni pamoja na afya ya udongo, mbegu, magonjwa ya mimea, maba...

DKT. MWIGULU AWASILI ROMA, ITALIA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Roma, Italia, leo, Septemba 20, 2026, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health), utakaofanyika Septemba 21–23, 2026, katika Makao Makuu ya FAO. Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Leonardo da Vinci (Fiumicino), Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

MHE. PAUL MAKONDA AHITIMISHA ZIARA HISPANIA KWA KUKUTANA NA WACHEZAJI WA FC BARCELONA

Hili si tukio la kawaida, bali ni hatua kubwa inayoiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa! Mheshimiwa Makonda amepenya hadi katikati ya Bara la Ulaya na kukutana na wachezaji wa klabu maarufu duniani ya FC Barcelona, nyota waliowahi kufanya maajabu makubwa katika soka la dunia. Akihitimisha ziara yake ya kihistoria, Mheshimiwa Makonda alipata nafasi ya kubadilishana mawazo na wachezaji hao, huku akiwaalika mmoja mmoja kuja kutembelea Tanzania na kujionea uzuri, utamaduni na vivutio vya kipekee vya nchi yetu. Huu ni mwanzo wa ukurasa mpya katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na FC Barcelona. Dunia sasa inaelekeza macho yake Tanzania na makubwa zaidi yanakuja! 🇹🇿 Ikizingatiwa Tanzania ni Mweneji wa AFCON 2027.

REA YAHIMIZA WANANCHI SIMIYU KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME NA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

  *REA YAHIMIZA WANANCHI SIMIYU KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME NA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA* 📌*Kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kurahisisha upatikanaji wa umeme* 📌*Wananchi wahamasikia kutumia Nishati safi ya kupikia* 📌*Maswa, Simiyu* Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea na kampeni ya utoaji elimu na uhamasishaji kwa wananchi kuhusu miradi ya nishati vijijini, ikiwemo matumizi ya umeme na nishati safi ya kupikia katika Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu. REA imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na huduma ya umeme mara baada ya miundombinu ya umeme kufikishwa katika maeneo yao, ili kutumia fursa zinazotokana na upatikanaji wa nishati hiyo katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Aidha, wananchi wamepewa elimu kuhusu kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kinachowawezesha wananchi kupata huduma ya umeme kwa urahisi, pamoja na namna ya kutumia nishati hiyo kwa usalama na ufanisi. vilevile, REA imewahamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati zinazochang...