Na OWM - TAMISEMI, Lushoto Mawaziri saba (7) wa kisekta wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ambaye ni Mbunge wa Lushoto wamekutana wilayani Lushoto kujadili utatuzi wa changamoto na migogoro inayowakabili wananchi mkoani Tanga ikiwemo ya ardhi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoyatoa katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Tanga. Mwenyekiti wa kikao kazi hicho, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Asiatu Kijaji ameongoza kikao hicho cha viongozi hao na watalaam wa Wizara za Kisekta ambacho kitawasilisha mapendekezo ya utatuzi wa migogoro na changamoto hizo za wananchi kwa Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kabla ya kuhitimisha ziara yake mkoani Tanga, ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki. Katika kikao kazi hicho wananchi wenye changamoto mbalimbali wamepata fursa ya kuwasilisha malalamiko yao na kusi...
Marato tv - Sauti ya Jamii