Shirika la Reli Tanzania linatarajia kuajiri wafanyakazi 2,460 katika mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kwa vipande viwili vya Kutoka Dar es Salaam mpaka Makutopora. Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya siku mbili ya bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR ) na MGR, kati ya Kigoma-Tabora na Tabora Mwanza iliyoanza Agosti 19, 2025. Ajira hizo ni mbali na zaidi ya ajira 115,000 ambazo tayari zinatokana na mkandarasi katika kipande cha kwanza mpaka cha sita. Katika ajira hizo 2,460 utekekezaji wake ni awamu ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 zaidi ya watumishi 500 wameshaajiriwa na mwaka huu wa fedha 2025/26 marajio ni kuajiri watumishi 272 na TRC itaendelea kuajiri kufikia watumishi 2,460. Wakati utekekezaji wa utoaji ajira rasmi za Shirika ukiendelea, jumla ya ajira 115,000 kutoka mkandarasi zimeshawanufaisha Watanzania 115,000 zikiwemo za vijana wa ...