Skip to main content

Posts

Showing posts from October 1, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Nchimbi Awasili Mtwara Kuendelea Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za Dkt Samia

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel  John Nchimbi leo Alhamisi Oktoba 2,2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Mtwara kwa ajili ya kuanza ziara ya mikutano yake ya hadhara ya kampeni, kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani mkoani Mtwara baada ya kuhitimisha mkoa wa Dar es Salaam. 

Wasira: Wanaohubiri Kufuta Stakabadhi Ghalani Wanataka Kurudisha Wizi Kwa Wakulima

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kusimamia na kusisitiza mfumo wa stakabadhi kwa wakulima na kwamba chama chochote kitakachokuja na sera ya kuufuta kinataka kuleta wizi na dhuluma kwa wakulima. Hayo yameelezwa leo Oktoba 1, 2025 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipozungumza na wana CCM Mkoa wa Mtwara  akiwa katika ziara ya kuwanadi na kuwaombea kura wagombea waliosimamishwa na Chama kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka. "Wapo watu wanapinga stakabadhi ghalani bila kujua, mimi najua, miaka ile nikiwa waziri wa kilimo mimi nilikuja hapa mkulima wa korosho alikuwa analipwa sh. 300 tena siyo kwa kipimo cha kisasa, analipwa sh. 300 kwa kitu kinaitwa kangomba, mnakajua kangomba?. "Ni kipo ambacho ni zaidi ya kilo na wanalipwa 300, katikati yuko mtu mwingine anayenunua kwa kangomba halafu anaenda kwa mwenye pesa yeye anamuuzia sh. 500 hana mkorosho hata mmoja lakini yeye anapata sh. 200 mwenye mkorosho aliyenunua salfa analipwa 300. "Taj...

Mct na Uwezo Tanzania Kushirikiana Kuimarisha Uandishi wa Habari za Elimu

  Dar es Salaam Ernest Sungura, Katibu Mtendaji wa MCT (Kulia), na Baraka Mgohamwende, Mkurugenzi Mtendaji wa UWEZO Tanzania, wakisaini makubaliano ya kushirikiana katika kuwawezesha waandishi wa habari kuandika habari za elimu kwa weledi, kwa kutumia ushahidi na kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, Oktoba 1, 2025, jijini Dar es Salaam.  Habari bora za elimu zina mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii. Kwa kuzingatia hilo, makubaliano haya yanaweka mkazo katika uandishi jumuishi kwa kuhakikisha sauti za wasichana, makundi yaliyotengwa, na wanafunzi walioko katika mazingira hatarishi zinatambuliwa na kupewa nafasi katika vyombo vya habari. Wanaoshuhudia ni; Greyson Mgoi, Mkuu wa Mawasiliano wa Uwezo Tanzania, na Josephat Mwanzi, Meneja wa Programu wa MCT.

Dkt Samia Kupokelewa Butiama Kwa Heshima za Mila za Kizanaki

  Mlezi wa familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kiongozi wa ukoo wa Burito Nyerere, Chifu Japhet Wanzagi, amemkaribisha mgombea wa nafasi ya Urais  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitis chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutembelea ukoo wa Burito Nyerere na familia ya Baba wa Taifa huko Mwitongo,  Butiama mkoani Mara. Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa Mwalimu Nyerere,Leo Oktoba Mosi mwaka 2025, Chifu Wanzagi amesema kuwa  Dkt. Samia Suluhu Hassan atapokelewa kwa heshima kubwa kama kiongozi wa machifu hapa nchini, kwa kuzingatia mila na desturi za Wazanaki. Kwa Mujibu wa Chifu Wanzagi Baada ya mapokezi hayo,Dkt Samia atatembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa  kwa ajili ya kuzuru kaburi na kuzungumza na wanafamilia, kabla ya kuanza Kampeni zake rasmi mkoani Mara kwa ajili ya kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi.

Balozi Nchimbi Afunga Kazi Dar es Salaam Kwa Kuomba Kura za Ccm

  Picha za matukio mbalimbali za Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia na kuwanadi baadhi ya Wagombea Ubunge wa mkoa wa Dar es Salaam, akiwemo Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni,Ndugu Abbas Tarimba pamoja na Madiwani,kwenye mkutano wake wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Biafra,leo Oktoba 01, 2025. Dkt. Nchimbi anahitimisha kampeni zake leo kwa mkoa wa Dar es Salaam akifikisha mkoa wa 15 tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar na kuelekea mikoa mingine kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maelfu ya wananchi wafurika katika mkutano wa mgombea urais wa CCM mjini Moshi

Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi na Wanachama wa CCM wa Moshi Mjini katika muendelezo wa kampeni za  Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho Mkoani Kilimanjaro tarehe 01 Octoba, 2025