Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda katika Kesi ya kumwingilia kinyume na Maumbile Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine iliyokuwa ikimkabili. Uamuzi huo wa kesi namba 1883/2024 umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Erick Marley baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwa na ushahidi unaoweza kumtia hatiani Dkt.Nawanda Hakimu Mkazi Mfawidhi Marley amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri umeacha shaka katika maeneo mbalimbali ikiwemo Video Mjongeo(CCTV)zilizowasilishwa kutoonyesha sehemu wawili hao walikuwa kwenye gari wakitenda tukio hilo. Jamhuri kutowasilisha vipimo vya vinasaba(DNA)vilivyochukuliwa kwa wawili hao huku katika ushahidi wake Binti aliyedai kulawitiwa na Dkt.Nawanda akidai kufanyiwa ukatili huo kwenye gari nyeupe lakini gari hilo halikuwa nyeupe bali ya Silver. Aidha binti huyo alisema wakati anafanyiwa kitendo hicho,gari lilikuwa na vioo(Tinted)na nje haku...
Marato tv - Sauti ya Jamii