Skip to main content

Posts

Showing posts from October 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MAOFISA 39 WA JESHI LA MAGEREZA WAPANDISHWA VYEO

Na. Wdrs Irine Nkana - DODOMA ‎Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP), Jeremiah Yoram Katungu, leo Oktoba 19, 2026, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, amewavalisha vyeo Maafisa 39 wa Jeshi la Magereza, wakiwemo Naibu Makamishna 17 na Makamishna Wasaidizi Waandamizi 22, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Msalato, jijini Dodoma. ‎Akizungumza katika hafla hiyo, CGP Katungu amemshukuru Rais kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza kwa kujaza nafasi za uongozi, kuboresha stahiki za watumishi na kutoa vibali vya ajira. Amesema kupandishwa vyeo kwa idadi hiyo ya Maafisa ni tukio la kihistoria, huku akiahidi kuwa Jeshi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi. ‎Amewataka Maafisa hao kutumia vyeo walivyopata kuongeza bidii na kusimamia majukumu ya Jeshi, ikiwemo kutoa hifadhi salama kwa wafungwa na mahabusu, kutekeleza programu za urekebu na kutoa ushauri wa kuzuia uhalifu katika jamii. ‎Kwa upande wake, Kamishna wa Sh...