Na Mwandishi wetu, Dodoma Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imewezesha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Famamu Muhimbili (MOI) kutoa huduma bora za ubingwa bobezi kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa ikiwemo CT SCAN mbili, MRI, mbili Angio Suite, Ultrasound na X-Ray za kisasa. Hayo yemesemwa leo Septemba 8, 2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini MOI Dkt Marina Njelekela wakati akifungua kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo. "Hili ni jambo la kujivunia na kuishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita, niwaombe tuendelee kuvitunza na kuvithamini vifaa hivi ili viendelee kuwanufaisha wananchi", alisisitiza Dkt Njelekela Akieleza zaidi Dkt Njelekela amesema Menejimenti ya Taasisi hiyo iendelee kuwakumbusha watumishi kufuata misingi ya maadili katika kuhudumia wananchi kwa kufanya kazi kwa bidii kama wanavyofanya sasa. "Ninafurahi kwamba MOI...