Skip to main content

Posts

Showing posts from February 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Juhudi Za Kuboresha Ikolojia Hifadhi Ya Taifa Ziwa Manyara Zazaa Matunda, Wanyama Wazidi Kuongezeka

 Na. Happiness Sam - Manyara Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wamepongeza juhudi za Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara katika kuboresha ikolojia ya maeneo yake, hatua iliyochangia ongezeko la wanyama katika Hifadhi hiyo. CPA. Khadija Ramadhani ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi alitoa pongezi hizo leo februari 06, 2025 wakati wa ukaguzi wa maeneo hayo, ukaguzi uliyofanyika ndani ya hifadhi hiyo iliyopo mkoani Manyara. Akiwa katika ziara hiyo CPA. Khadija alisema, “Niwapongeze Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara kwa juhudi kubwa za kuboresha mazingira na ikolojia ya maeneo mbalimbali katika Hifadhi hii, hali iliyopelekea ongezeko la wanyama tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali”. Aidha aliongeza, “Leo tumeshuhudia Twiga, Pundamilia, Tembo na Swala wengi, niwapongeze kwa kazi nzuri ya kuendelea kuyalinda maeneo ya Hifadhi zetu na kuboresha maeneo y...

Dc Bariadi Akemea Vikali Vitendo Vya Kuchungia Mifugo Ndani Ya Hifadhi

Na Mwandishi wetu, Bariadi -Simiyu Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Simon Simalenga amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wafugaji wilayani humo kuchungia mifugo ndani ya Hifadhi hususani Pori la Akiba Maswa huku akisisitiza kuwa wilaya hiyo sio sehemu salama kwa watu wanaofanya ujangili na  wanaovunja sheria, kanuni na taratibu  zilizowekwa kwa ajili ya kulinda rasilimali za nchi. Akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari Februari 6, 2025 wilayani humo Mhe. Simalenga amesema vitendo hivyo vimekuwa vikileta athari kubwa kwa mazingira ya hifadhi, na pia kuhatarisha usalama wa wafugaji wanaoingia ndani ya hifadhi dhidi ya wanyamapori wakali pamoja na kuharibu mfumo ikolojia wa maeneo hayo. "Niwasihi sana wananchi wote walio ndani ya wilaya ya Bariadi, maeneo ya Pori la Akiba Maswa, maeneo ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti  Kwa kipande kinachoingia wilaya ya Bariadi Kata ya matongo sio maeneo ya kwenda kuchunga mifugo wala haifai kwenda kuingiza mifugo kwenye...

CBE kuanza kutoa PhD ya infomatiki za biashara

Na Mwandishi Wetu CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kinatarajia kuanzisha program ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Infomatiki ya Biashara ili kuleta mabadiliko ya uchumi wa kidijitali na teknolojia katika kufanya biashara za kidijitali kuendana na mabadiliko ya dunia. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kujadili mtaala  wa masomo hayo yaliyowashirkisha wataalamu wabobezi kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu. Wataalamu hao walikuwa wakipitia mtaala ambao umeandaliwa na chuo hicho na kutoa maoni yao ili baada ya hapo upelekwe kwa mdhibiti ambaye ni Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi  (NACTIVET) kwaajili ya kupewa ithibati na kuanza kutumika. Alisema kuanzishwa kwa shahada hiyo ni hatua muhimu yenye kuleta mabadiliko katika kuendeleza elimu ya juu, kukuza uvumbuzi wa kiteknolojia na kuchangia ajenda ya maendeleo ya taifa. Alisema CBE ambayo inakampasi...

Waziri Mkuu Amesema Tanzania Itaendelea Kujiimarisha Kiuchumi

_Ampongeza Rais Dkt. Samia kwa kuendeleza mahusiiano ya Kimataifa_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inajiimarisha katika kukuza uchumi wake kwa kutumia rasilimali zilizopo ili kuweza kumudu kutekeleza maeneo yote muhimu yakiwemo ya sekta ya afya, elimu na maji. Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Februari 6, 2025) wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, George Mwanisongole katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.”Tanzania itatumia vyanzo vya fedha na mapato vilivyowasilishwa Bungeni ili vipangiwe kazi ili kujazia maeneo yaliyopungua.” Mbunge huyo alitaka kujua Serikali inajipangaje na mabadiliko ya sera za nje ya nchi ya Marekani ambayo yanakwenda kuathiri utekelezaji wa sera za elimu, afya na uchumi hususan miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na USAID. ”Uwezo tunao, tunazo maliasili, tunazo rasilimali, kazi ambayo tunayo ni Watanzania kushirikiana kuhakikisha tunatumia maliasili na rasilimali tulizonazo kujenga uchumi wa ndani kuwezesha mip...

Takukuru Mara yabaini Dosari Kwenye Miradi 10 yenye Thamani ya Bilioni 7

Na Shomari Binda-Musoma  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) mkoa wa Mara imebaini dosari kwenye miradi 10 ya maendeleo yenye shamani ya shilingi bilioni 7,947,792,718.00 katika sekta za afya,elimu,barabara na maji. Dosari hizo zimebainika baada ya miradi hiyo kufuatiliwa kwa kufanyiwa ukaguzi ili kujua ubora wake na thamani ya fedha iliyotumika. Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara Sadiki Nombo wakati akitoa taarifa kwa umma mbele ya Waandishi wa Habari katika kipindi cha oktoba hadi disemba 2024. Moja ya mradi uliofatiliwa na kukutwa na dosari ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari Seka iliyopo Wilaya ya Musoma wenye thamani ya shilingi milioni 584,280,029 Katika mradi huo dosari zulizobainika ni kukosa vifaa madhubuti kwaajili ya kusafisha na kusaswazisha eneo la ujenzi pamoja na kukosa maji kwaajili ya shughuli za ujenzi. TAKUKURU katika ufatiliaji wake ilimshauri msimamizi wa mradi kufatilia utaratibu  wa kuomba kuunganishiwa maji kutok...