*Makaa ya Mawe, Vito na Dhahabu kichocheo cha uchumi mkoani Ruvuma* 🔺_Makusanyo maduhuli yafikia asilimia 98 kwa mwaka 2024/2025_ 📍*Ruvuma* MAKUSANYO ya maduhuli ya Serikali kupitia Sekta ya Madini katika Mkoa wa Ruvuma yatokanayo na mrabaha, tozo na ada mbalimbali kwa mwaka wa fedha ulioanza Julai 2024/2025 ni Shilingi Bilioni 32.5. Fedha hizo ni makusanyo ya mpaka tarehe 19 Mei, 2025 wakitarajiwa kuvuka lengo la fedha walilopangiwa la Shilingi Bilioni 33.15. Akizungumza na wanahabari wa Tume ya Madini, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi amesema, hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu Mkoa huo utakuwa umevuka lengo la zaidi ya asilimia 100 ya ukusanyaji mapato. Mhandisi Bikulamchi amesema kuwa mafanikio hayo yamepatikana kutokana na kushamiri kwa biashara ya makaa ya mawe ambayo kwa Mkoa wa Ruvuma yamebainika kuwa ni bora zaidi na yamekuwa yakiuzwa nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Bara la Asia na...
Marato tv - Sauti ya Jamii