WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo yote nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo karibu na makazi yao. Ameyasema hayo leo (Jumapili, Mei 18, 2025) wakati akizungumza na wananchi katika Eneo la Hungumalwa wilayani Kwimba, Mwanza baada ya kuzindua mradi wa maji Hungumalwa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza. Mradi huo wa maji wa Hungumalwa ulianza kutekelezwa tarehe Machi 08, 2022 na ulikamilika Agosti 15, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amewasisitiza wananchi kuendelea kuiamini na kushirikiana na Serikali ambayo imedhamiria kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao. Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na ya elimu, maji, afya na ujenzi wa barabara. ”Tutaendelea kusimamia maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na tutaendelea kutekeleza ilani kwa vitendo. Kwenye elimu tunaendelea kuk...
Marato tv - Sauti ya Jamii