*Na Mwandishi Wetu, Dodoma* MENEJIMENTI ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii Bw. Nkoba Mabula imekutana na kufanya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano na uongozi wa Benki ya NMB ukiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali Makao Makuu ya NMB Dodoma Bi. Vicky Bishubo. Mazungumzo hayo ya Kimkakati baina ya pande hizo mbili yamefanyika leo Julai 27, 2026 katika Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mtumba jijini Dodoma. Akizungumzia kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Mabula amesema kimekuwa na tija kubwa kwani Benki ya NMB ni wadau muhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii hususani katika kuimarisha maeneo yake makuu ya Utalii na Uhifadhi. “Ugeni huu wa wenzetu kutoka NMB unadhihirisha namna Wizara ya Maliasili na Utalii inavyozingatia umuhimu wa kukutana na wadau mbalimbali kama sehemu ya kujenga uhusiano wa karibu na pia kuimarisha utendaji kazi wa Wizara kwa wadau na wananchi kwa ujumla,” amesema Bw. Mabula. Naye Mkuu wa ...
Marato tv - Sauti ya Jamii