📍 Asema nadhiri aliyoweka ilitokana na watoto kusoma umbali mrefu 📍 Asema alipokosa fedha serikali alianzisha msalagambo kusaka marafiki zake kutimiza nadhiri yake 📍 Awashukuru CRDB Benki, Karimjee Foundation kumsaidia kujenga madarasa mawili na vyoo 📍 CRBD yaungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumpongeza MwanaFA kwa kazi nzuri anayofanya Muheza 📍 Mtendaji wa Kijiji Ataka umbali waliokuwa wakisoma watoto wa Kijiji cha Misufini 📍 Wazazi Misufini Wasema hawakukosea kumchagua MwanaFA kuwa mbunge, wamtaja pia Rais Na Mwandishi Wetu, Magoroto NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA, alisema alijiapiza na kuweka nadhiri ya kujenga shule ya msingi katika Kijiji cha Misufini kilichopo kata ya Magoroto kilichokuwa kikikabiliwa na changamoto lukuki. Sambamba na nadhiri hiyo, MwanaFA hakutegemea kama wananchi wa Kijiji hicho wangekichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa walikabiliwa na changamoto nyingi. Alisema Kijiji ...
Marato tv - Sauti ya Jamii