Skip to main content

Posts

Showing posts from July 17, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Lema Atoa Maneno Mazito Dhidi ya Mbowe

 Anaandika Godbless Lema kwenda kwa Mbowe. Kwako Mh Freeman Mbowe. Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu. Tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya ulipokuwa Mkti wetu. Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku mwenyekiti wetu, Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na Chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania. Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbali mbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ...

Zaidi ya vyuo 20 vya kimataifa kutua Dar

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Elimu Nje ya nchi Global Education Link inatarajia kuwakutanisha wanafunzi wa Tanzania na vyuo vikuu zaidi ya 20 kutoka nchi mbalimbali duniani  katika maonyesho jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi watapata fursa ya kujua fursa za kusomea kozi mbalimbali kwenye vyuo hivyo Global Education Link imesema wanafunzi watakaotaka kusoma nje ya nchi watapata udahili wa papo hapo. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel,  wakati akizungumza kuhusu maonyesho hayo. Alisema kwenye maonyesho hayo yatakayofanyika siku ya Jumanne Julai 22 kutakuwa na vyuo vikuu kutoka mataifa mbalimbali vikiwemo kutoka nchi za Cyprus, India China Malaysia, Uingereza, Canada, Marekani, Australia,  Uturuki , Mauritius  na Dubai Alisema baadhi ya vyuo vikuu vitakavyoshiriki kwenye maonyesho hayo vitatoa ufadhili wa kuanzia asilimia 20 hadi 80 wakati vingine vitatoa ufadhili wa moja kwa moja. Mollel alisema kw...

Maboresho bandari ya Tanga, yaanza kulipa

* Fedha zilizotolewa na serikali zarudi Na Mwandishi Wetu, Tanga FEDHA zilizotolewa na serikali kiasi cha shilingi bilioni 429.1 kwa ajili ya uwekezaji katika bandari ya Tanga, fedha hizo zimerudi na kubaki salio la shilingi bilioni 56.7. Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Leo Julai 10, Meneja wa bandari ya Tanga Mhandisi Maosud Mrisha alisema kuwa kwa kipindi cha miezi 24 taasisi mbili za serikali za TPA na Mamlaka ya mapato nchini TRA, wameweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 484.8. "Ile fedha iliyotolewa na serikali kiasi cha shilingi bilioni 429.1 imesharudishwa na taasisi mbili za TPA na TRA kwa miezi 24 na chenji pembeni imebaki," alisema Mhandisi Mrisha na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huo. Akifafanua kuhusu makusanyo hayo alisema kwamba TPA  imeendelea kuvunja rekodi ya mapato kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali na kupelekea ongezeko la shilingi bilioni 30 ya mapato ambayo waliwekewa lengo la kukusanya kiasi cha shil...

Serikali Yaanzisha Mpango Maalum Kuwawezesha Wanawake na Vijana Katika Uchimbaji Endelevu wa Madini

_Lengo ni Kuchochea Maendeleo, Usalama na Utunzaji wa Mazingira kwa Vizazi Vijavyo_ 📍*Singida, Julai 17, 2025* Serikali kupitia Tume ya Madini imezindua mpango maalum wa “Uchimbaji Bora na Endelevu kwa Kizazi Kijacho”, unaolenga kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchimbaji madini nchini. Mpango huu unatoa fursa ya kuanzisha vikundi, kupata mikopo, pamoja na leseni za uchimbaji kwa lengo la kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Akizungumza katika mafunzo kwa wachimbaji wadogo yaliyofanyika katika vijiji vya Utaho A na Isalanda, Kata ya Kituntu na Puma mkoani Singida, Mjiolojia kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Mutagwa, amebainisha kuwa mpango huo pia unalenga kuhakikisha kuwa shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa usalama na kuzingatia utunzaji wa mazingira. “Uchimbaji salama ni msingi wa maendeleo. Tunawafundisha wachimbaji si tu kuhusu mbinu bora za uchimbaji, bali pia umuhimu wa kulipa kodi ya serikali k...