Skip to main content

Posts

Showing posts from November 7, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais mteule Donald Trump amemteua mwenyekiti-mwenza wa timu yake ya kampeni, Susie Wiles, kuwa White House Chief of Staff wa Marekani

 Rais mteule Donald Trump amemteua mwenyekiti-mwenza wa timu yake ya kampeni, Susie Wiles, kuwa White House Chief of Staff wa Marekani. Anakua mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo. Nafasi ya WH Chief of Staff ni moja ya nafasi zenye ushawishi mkubwa katika utawala wa Marekani, ambapo mhusika huyu hutumika kama mshauri mkuu wa rais na kuhakikisha utendaji wa Ikulu unafanyika kwa ufanisi. Haya ni baadhi ya majukumu ya nafasi hii: 1. Ratiba na Mipangilio: Anasimamia ratiba ya kila siku ya rais, akihakikisha kuwa mikutano na majukumu yote yanazingatia malengo ya utawala. 2. Mshauri na Mlinda Mlango: Akiwa mshauri wa karibu zaidi wa rais, anahusika na kuchuja taarifa na watu wanaofika kwa rais ili kuhakikisha muda na nishati ya rais vinatumika vyema. 3. Mkurugenzi ya Sera na Watumishi: Anasimamia washauri wakuu na watumishi wa Ikulu, akihakikisha kuwa wote wanashirikiana katika kufanikisha ajenda na sera za rais. 4. Kujenga Mahusiano Muhimu: Akitumika kama kiunganishi kati ya ...

Ccm Misungwi yajizatiti kuyavunja makundi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

    Chama chamapinduzi(CCM)wilaya misungwi mkoani mwanza kimewataka viongozi na wanachama wake kuyavunja makundi yaliyoibuka wakati wa mchakato wa kura za maoni za wenyeviti wa vitongoji,vijiji na mitaa pamoja na wajumbe wa serikali za mitaa na vijiji. Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Emmanuel Masangwa ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi na watendaji pamoja na wanachama wa chama hicho katika kata ya misasi. Masangwa amesema kuwa kuvunjwa kwa makundi hayo ni muhimu katika kukiwezesha chama hicho kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba 27 mwaka huu. ‘’Uchaguzi wa ndani wa chama chamapinduzi tumemaliza kufanya uchaguzi wetu,kwa hiyo tunaendelea kukiunganisha chama na kuendelea kuwaambia wanachama ambao hawakupata kura za kutosha waendelee kukiunga mkono CCM pamoja na viongozi ambao wameaminiwa ili kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa novemba 27’’alisema Masangwa na kuongeza kuwa ‘Kuwepo makundi wakati wa ucha...

Mtambi awataka Wananchi mkoa wa mara kuchangamkia fursa chuo cha Mjnuat

 Shomari    Binda-Butiama     MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi  amewataka wananchi wa mkoa huo  kuchangamkia fursa za uwekezaji chuo kikuu  cha kilimo cha  Mwalimu Nyerere  ( MJNUAT)      Fursa zilizotajwa ni  pamoja na ujenzi wa  miundombinu  dmbalimbali ikiwemo ya   huduma kwenye  mazingira ya chuo.   Hayo ameyasema   katika Wilaya ya Butiama     baada ya serikalik uwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu cha Mwalimu  Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT ).    Akizungumza baada  kushuhudia utiaji saini   wa mkataba wa ujenzi  wa miundombinu d mtambuka wenye   thamani ya shilingi bilioni 9 katika  chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) na mkandarasi Shandong Hi-Speed Dejian Group Co. Ltd na Mshauri  mwelekezi Epitome...

Waziri Mkuu aonesha vitendo katika kudhibiti matumizi ya kuni

*Azuru Makutupora JKT, Msalato Sekondari na Gereza la Isanga WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwenye taasisi zenye watu zaidi ya 100. Waziri Mkuu ametembelea kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Makutupora (834 KJ), shule ya Sekondari Msalato na Gereza la Isanga ili kuona utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuwa taasisi zote za Serikali na binafsi zinazotumia nishati ya kuni kuandaa chakula cha watu zaidi ya 100 kwa siku zisitishe matumizi ya kuni na mkaa kuwekeza katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo Desemba 31, 2024.  Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Dodoma na wa taasisi zote tatu kwa nyakati tofauti, Waziri Mkuu aliwaeleza viongozi hao kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishatoa maelekezo na yeye anapita kuangalia kama wamebadilisha mifumo inayotumika kwenye taasisi hizo. “Nishati safi ya kupikia ni ubunifu wa Rais wetu ambaye amebobea...

Wataalam Nirc waaswa kuzingatia sheria ya manunuzi

WATAALAM Tume Ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), wamekumbushwa kuzingatia sheria na kanuni mpya za manunuzi katika usimamizi wa miradi na utekelezaji wa manunuzi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, wakati wa mafunzo ya siku tano ya Sheria Mpya ya Manunuzi ya Umma Namba 10 ya Mwaka 2023 na Kanuni za mwaka 2024,iliyowahusisha  Afisa Masuuli, Wajumbe wa Bodi ya Zabuni na Wahandisi wa Mikoa. “Wakati mwingine sisi watumushi wa serikali tunakuwa sababu ya wakandarasi kuisababishia hasara serikali”, ameongeza Mndolwa Mndolwa amesema lengo la kutoa elimu hiyo juu ya sheria mpya ni kuhakikisha wataalamu hao wanazingatia sheria na  taratibu sahihi ili kuepusha hasara za manunuzi kwa serikali. “Ndani ya kazi ya umma hakuna nia njema kuna utaratibu, niwaombe sana tufuate taratibu tusimamie kazi zetu, hii sheria ambayo mnakumbushwa mjione ninyi ni watendaji wakuu katika mikoa yenu," alisema Mndolwa.  Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wataalamu w...

Rais Mwinyi:Smz kujenga kiwanja kipya cha mpira kwa Afcon2027

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameendelea na ziara ya kikazi nchini China ambapo leo amekutana na kampuni mbalimb ali zinazolenga kuwekeza Zanzibar.  Katika mwendelezo wa ziara hiyo Rais Dk. Mwinyi pia, amekutana na uongozi wa kampuni maarufu na yenye uzoefu wa miaka mingi, China Railway Construction Engineering Group (CRJE), yenye makao makuu Beijing, China katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Westin, Shanghai, China. Katika mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kujenga Mji wa Kiserikali ambapo Serikali na taasisi zake zitawekwa sehemu moja ili kuboresha ufanisi na utendaji serikalini pamoja na kurahisisha huduma kwa wananchi. Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali pia ina mpango wa kujenga kiwanja cha mpira wa miguu cha kimataifa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027. Mkutano huo umekutanisha Benki na taasisi za fedha, wakiwemo wenyeji CR...

Rais Samia apeleka neema Tabora

*📌Aidhinisha Bilioni 19 kusambaza umeme vitongojini* *📌Kaya 5,940 kutoka katika Vitongoji 180 kunufaika* Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 19 wa kusambaza umeme katika vitongoji 180 utakaonufaisha Kaya 5,940 Mkoani Tabora. Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Robert Dulle Novemba 07, 2024 Mkoani Tabora mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Paul Chacha wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya Sinotec Company Ltd kutoka nchini China. “Napenda kuwafahamisha wananchi wa Tabora kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta. Samia Suluhu Hassan ameridhia kiasi cha shilingi 19,057,015,682.55 kitumike kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 180 mkoani hapa na leo hii tupo hapa kumtambulisha mkandarasi anayetekeleza mradi huu,” alibainisha Mhandisi Dulle. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Chacha alimuelekeza Mkandarasi kuhakikisha anakamalisha ka...