Skip to main content

Posts

Showing posts from February 23, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ppra Yatoa Mafunzo ya Mfumo wa Nest Kwa Makundi Maalum Wilayani Musoma

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Ziwa, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, hii leo imeendesha mafunzo maalumu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na makundi maalumu kuhusu namna ya kujiunga na Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (NeST) na fursa zinazopatikana kupitia mfumo huo katika ununuzi wa umma. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu ambao ni raia wa Tanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika zabuni za Serikali kupitia mfumo wa NeST, sambamba na utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 na Kanuni zake za mwaka 2024 zinazozitaka taasisi nunuzi kutenga asilimia 30 ya thamani ya ununuzi wao wa mwaka kwa makundi maalumu. Kupitia mfumo wa NeST, makundi maalumu yatapata fursa ya kushiriki katika zabuni mbalimbali za Serikali ikiwemo huduma za ujenzi, usafi wa mazingira, ulinzi na usalama kazini pamoja na huduma zinazohitaji ujuzi, teknolojia na uzoefu, fursa hizi zina...

Sakata la Zungu Edwin Soko asema hisia zilitawala kuliko ufahamu wa sekta ya Anga

Hivi karibuni, mjadala umeibuka kufuatia kauli nzito zilizotolewa na mwandishi wa habari Kelvin Raphael (Zungu) kuhusu utendaji wa Air Tanzania Company Limited (ATCL). Kauli hizo zimezua mjadala mpana miongoni mwa wananchi, wadau wa sekta ya usafiri wa anga, pamoja na mamlaka za serikali, zikigusa masuala ya uwajibikaji, usalama wa wasafiri na taswira ya uwekezaji wa Taifa. Haki ya kusema na uhuru wa maoni Kama mwandishi wa habari na raia, Zungu ana haki ya kikatiba ya kutoa maoni yake kuhusu masuala ya umma. Uhuru wa kujieleza ni msingi muhimu wa demokrasia, kwani unasaidia kuibua changamoto, kuhimiza uwajibikaji na kuleta maboresho katika taasisi za umma na binafsi.  Waandishi wa habari wana jukumu muhimu la kuwa sauti ya jamii, kuuliza maswali magumu, na kuhakikisha uwazi katika utendaji wa taasisi. Umuhimu wa kusema kwa hekima kulinda maslahi ya Taifa Pamoja na haki hiyo, ni muhimu kwa kila mwenye sauti ya ushawishi, hasa mwandishi wa habari, kutumia hekima na uwajibikaji katik...

Kanali Kido Aagiza Tanroads na Tarura Mkoa wa Kagera Kutoa Ajira Kwa Vijana na Wanawake

 Na Angela Sebastian ;Bukoba  Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali Yahya Ramadhan Kido amewaagiza wakala wa barabara Tanzania (Tanroads) na wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) mkoani humo,kuzingatia na kutoa kipaumbele katika masuala ya ajira kwa vijana na wanawake wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea na inayotarajiwa kutekelezwa. Ametoa agizo hilo leo wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara cha kwanza tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huo, kilichofanyika leo mjini Bukoba. "Sasa nawaelekeza Tanroads na Tarura kuwahusisha kwa wingi jinsia ya kike katika fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na vipaumbele kuajiri kundi la vijana kwani hii ndiyo nguvu kazi ya Taifa, tunayoitegemea hivyo sitegemei kuona mnaleta watu kutoka nje ya mkoa ambapo suala hili lilileta malalamiko kwa wananchi tunaowahudumia"ameagiza Kido. Pia amewataka Tanroads na Tarura kuzingatia usimamizi mathubuti wa rasilimali fedha kwa maana asilimia ya kazi lazima ionekane thamani yake,u...

Waziri Mkuu Azindua Shule ya Sekondari Sinya

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 23, 2026 amezindua Shule ya Sekondari Sinya iliyopo katika Kata ya Sinya, Kijiji cha Leremeta, Wilaya ya Longido mkoani Arusha. Ujenzi wa shule hiyo umegharimu shilingi bilioni 1.2  kutoka Serikali Kuu, SEQUIP, TASAF na Mapato ya Ndani ya Halmashauri, pamoja na mchango wa wananchi wa shilingi milioni 34. Shule hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza upatikanaji wa elimu ya sekondari, kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule zilizopo na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa jamii ya Sinya na maeneo jirani. Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Dkt. Mwigulu amewataka wanafunzi katika shule hiyo wasome kwa bidii ili waweze kunufaika na fursa za elimu ambazo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziweka kwa watoto wa kitanzania ikiwemo proramu ya ufadhili wa masomo ya ‘Samia Scholarship’.

Mbunge Devotha Atoa Milioni Moja za Matibabu ya Mtoto Mwenye Uvimbe Kichwani Karagwe

Na Angela Sebastian; Bukoba  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Devotha Daniel, ametoa msaada wa shilingi milioni moja  kwa mtoto Grecseous Raphael mwenye umri wa miezi minne mkazi wa Kata ya Kihanga, Wilaya ya Karagwe, anayesumbuliwa na uvimbe kichwani, ili kumwezesha kufikishwa Hospitali ya Kanda ya Bugando kwa ajili ya upasuaji. Mbali na msaada huo wa fedha,  Devotha pia ameahidi kugharamia bima ya afya kwa familia nzima ya mtoto huyo, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na ulinzi wa matibabu. Hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya  Devotha katika kuwatumikia wananchi kwa vitendo, kuwagusa wenye mahitaji maalum, na kuendelea kuleta matumaini mapya kwa jamii. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Devotha amesema Kuwa  alipata taarifa za mtoto huyo kupitia matangazo ya kituo cha redio ya jamii cha Fadeco Radio, ambapo mama...

Dkt. Mwigulu Akagua Maendeleo Mradi wa Maji Sinya

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 23, 2026 amekagua maendeleo ya Mradi wa Majisafi wa Sinya–Namanga unaotekelezwa eneo la Sinya, Longido mkoani Arusha. Mradi huo unaotarajiwa kuongeza uzalishaji wa maji hadi lita 4,100,000 kwa siku, unatekelezwa na mkandarasi M/s. Zongii Contractors Co. LTD kwa gharama ya Shilingi bilioni 13.5 ambazo zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Mradi huo unategemea kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Namanga na Sinya kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maji ambayo chanzo cha sasa cha Mto Simba hakitoshelezi.  Maji yatakayo toka katika mradi huo ambao hadi kufikia Januari 2026 ulikuwa umefikia asilimia 24.7 yatakidhi mahitaji ya wananchi na mifugo.