Skip to main content

Posts

Showing posts from March 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Vikundi vya mawasiliano vya Majeshi ya SADC kujengewa uwezo

Vikundi vya Mawasiliano vya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) vimekutana ili kujenga uwezo na uelewa wa pamoja katika fani ya mawasiliano leo tarehe 02 Machi 2025, Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo mjini Unguja, Zanzibar.  Akifungua Mkutano huo kwa niaba ya  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Amri Salim Mwami amesema Mkutano huo utawajengea uwezo wa utendaji washiriki, na kusisitiza kuwa mawasiliano yanahitaji vifaa bora na mafunzo ili kuongeza weledi katika utendaji.  Meja Jenerali Mwami aliongeza kuwa nia ya Mkutano huo ni kuwa na muongozo mmoja ili kuwepo na uelewa wa pamoja kwa majeshi ya SADC. Aidha,  mshiriki kutoka nchini Botswana Brigedia Jenerali Meshack Mosime  amesema mkutano huo umekuwa na manufaa makubwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya na kwa mshiriki mmoja mmoja hasa katika fani ya mawasiliano, lakini pia wamepata fursa ya kutalii na kuona uzuri wa Tanzania ...

Waziri Mkuu: Elimisheni Wananchi Masuala ya Ardhi

*Asisitiza amani na kuishi kindugu WAZIRI MKUU Dkt Mwigulu Nchemba amewaomba Wabunge wa Mbulu na uongozi wa wilaya hiyo waendelee kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuendeleza amani na kuishi kindugu. Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Machi 2, 2026) wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye hospitali ya Lutheran ya Haydom, wilayani Mbulu, mkoani Manyara mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la afya ya mama na mtoto. “Nimepata taarifa ya kuwepo kwa mizozo kule Yaeda Chini. Waheshimiwa Wabunge wa majimbo haya mawili na viongozi wa Halmashauri kaeni na wananchi muwaelimishe kuwa ardhi haiongezeki. Kaeni na wananchi muwaeleze kuwa suluhisho ni kupanga matumizi bora ya ardhi.” “Endeleeni kuwaelimisha wananchi kuwa hata wakipigana ardhi haiongezeki. Hata mkiwaondoa kabila fulani, bado ardhi haiongezeki kwa sababu watu wanaendelea kuzaa.” Akizungumzia kuhusu ujenzi wa jengo hilo, Waziri Mkuu amesifu kazi nzuri iliyofanywa na akamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fe...

Waziri Mkuu Akagua Ujenzi wa Barabara ya Mbulu – Garbabi (Km 25)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amekagua mradi wa ujenzi wa barabara kipande cha Mbulu – Garbabi (km 25), ambacho ni sehemu ya barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 389) inayojengwa kwa kiwango cha lami. Mradi huo unaotekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) unalenga kuboresha mawasiliano ya barabara, kuimarisha usafirishaji wa watu na bidhaa, na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo husika. Hadi sasa, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 41.7, ambapo jumla ya shilingi bilioni 36.3 zitatumika kukamilisha ujenzi. Mpaka sasa malipo ya shilingi bilioni 12.5 tayari yameshafanyika.

Mtaalamu Sayansi, Usalama wa Mtandao atinga Tume

*DAR ES SAALAM:*  TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Machi 2, 2026 imekutana na Mtaalamu wa Uchunguzi wa Kisayansi na Usalama wa Mtandao, Yusuph Kileo. Mkutano huo wa Tume na Mchunguzi huyo umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wataalamu, watu wa kawaida, viongozi wa sasa na wastaafu. Katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa. Hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi imeiongezea Tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29...

Moi Yaanika Mafanikio Makubwa Kwa Taasisi hiyo Chini ya Rais Samia

 DODOMA  SERIKALI kupitia Taasisi ya Tiba ya Mifupa na ubongo (MOI) katika kipindi cha mwaka 2025 imefanikiwa kuanzisha huduma mpya 9 za kibobezi ikiwemo huduma ya upasuaji wa ubongo kwa kutumia akili unde ambazo hapo awali ziliwalazimu wagonjwa kuzifuata nje ya Tanzania. Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na ubongo (MOI) Mhe. Balozi, Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani alizowahidi Watanzani. Balozi,Dkt. Mpoki amezitaja huduma zingine zikiwemo huduma za Upasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu,Huduma ya kuchukua sampuli za vipimo kwa njia ya matundu,Huduma ya kuweka tiba simenti kwenye pingili za mgongo zilizovunjika,Huduma ya tiba ya maumivu (Pain clinic). Huduma ya upasuaji rekebishi wa viungo vilivyopooza,Huduma ya upasuaji wa uvimbe na ubongo kwa kutumia teknolojia ya fluorescein, Kuanza kwa wodi mpya za kisasa za premier kwa ajili ya wagonjwa maalum ...

Bawacha Walitaka Jeshi la Polisi Mkoani Mara Kutozuia Kongamano la Wanawake

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano ;Musoma. Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema mkoa wa Mara na wanawake wa Chama walitaka Jeshi la Polisi kutozuia Kongamano la Wanawake linalotarajia kufanyika Machi 8,2026 Duniani kote. Akiongea kwa niaba ya wanawake wa Chadema Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Veronica Sando amesema haoni sababu ya Jeshi hilo kutoa tamko la kuzuia Kongamano hilo kupitia vyombo vya habari kwani wanawake wa Chadema wamejiandaa kusherekea siku hiyo. "Siku hiyo ni siku ya wanawake Duniani kote kwa nini Kamanda wa Polisi azuie kama anazuia basi azuie pia kwa wanawake wa taasisi nyingine vikiwemo na vyama vya kisiasa sisi ni akina mama na tarehe 8  Machi,2026 tunaungana na wanawake Duniani kote kufikisha jumbe zetu, kupewa kauli kwa mdomo na kutakiwa kufika kituo Cha Polisi kwa maelezo ya mdomo hii siyo haki ni uonevu,mbona hata madhehebu ya dini wanaadhimisha kwa umoja wao wasituvuruge", amesema Veronica. Ameongeza kuwa sababu aliyoielezea s...