*Ukosefu wa mawasiliano chanzo cha mgogoro wa wabia katika leseni 33* *Wachimbaji watakiwa kuweka mifumo ya wazi ya ushirikiano na mawasiliano* *Serikali yaonya leseni zisizoendelezwa kufutwa* 📍*Mwanza* Ukosefu wa Mawasiliano na taarifa sahihi miongoni mwa wamiliki wa leseni za uchimbaji madini unaweza kuchochea migogoro isiyo ya lazima na kudhoofisha shughuli za uchimbaji, hasa kwa wachimbaji wadogo. Hayo yamebainishwa leo Septemba 15, 2026 jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, wakati akiongoza kikao cha kutatua mgogoro uliowahusisha wachimbaji wadogo jijini humo. Dkt. Kiruswa amesema mgogoro huo umetokana kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa taarifa sahihi na mawasiliano baina ya wabia wanaomiliki kwa pamoja leseni 33, ambapo upande mmoja uliamini kuwa baadhi ya wabia wanafanya uzalishaji bila kumshirikisha na bila kumpatia stahiki zake, huku upande mwingine ukieleza kuwa katika leseni hizo bado haujaanza uzalishaji. Baada ya kusikiliza pande zote, Dkt. Kirus...
Marato tv - Sauti ya Jamii