Skip to main content

Posts

Showing posts from August 1, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kenya yathibitisha visa 314 vya Mpox maambukizi yakiongezeka

  Kenya imethibitisha jumla ya visa 314 vya ugonjwa wa Mpox kufikia Julai 31, 2025, ikiwa ni ongezeko kubwa la maambukizi mwaka mmoja tangu kisa cha kwanza kugunduliwa katika mpaka wa Taita-Taveta, Waziri wa Afya Aden Duale ametangaza. Mlipuko huo ulianza Julai 31, 2024, pale mtu aliyekuwa akisafiri kutoka Uganda kuelekea Rwanda kupitia Kenya alipogunduliwa kuwa na Mpox katika kituo cha mpaka cha Taita-Taveta. Tangu hapo, ugonjwa huo umesambaa hadi kaunti 22 licha ya juhudi kabambe za kudhibiti maambukizi zinazoendeshwa na Wizara ya Afya. Kaunti ya Mombasa inaongoza kwa kuwa na visa vingi zaidi vya Mpox, ikirekodi visa 146, ikifuatiwa na Busia (63), Nakuru (21), Kilifi (19), Nairobi (17), na Makueni (13). Taita-Taveta na Uasin Gishu zimeripoti visa vitano kila moja, huku Bungoma ikiwa na visa vinne. Kaunti za Kajiado, Kakamega na Kiambu kila moja imerekodi visa vitatu. Kaunti za Kericho na Machakos zimeripoti visa viwili kila moja, ilhali Migori, Kisii, Kirinyaga, Isiolo, Kitui, Na...

Vijana waliokopeshwa na TADB waingiza mamilioni

Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAKAMU wa Rais, Dk Phillip Mpango ameiagiza Wizara ya Uvuvi kuwawezesha vijana wanaofuga samaki kwa kutumia vizimba ili wapate mitaji mikubwa ya kuwawezesha kuyafikia masoko ya kimataifa. Pia ameiagiza Wizara hiyo kuweka mkakati kabambe wa kuwatangaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili wawe ushuhuda kwa vijana wengine wavutiwe na waweze kujiajiri. Dk Mpango alitoa maagizo hayo Leo Ijumaa  wakati alipotembelea maonesho ya wakulima maarufu kama nane nane mkoani Dodoma baada ya kusikia ushuhuda wa vijana wanaofuga samaki. Vijana hao  tisa wa kikundi cha VIJANA NGUVU KAZI MWANZA walikopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ili wafuge samaki kwa kutumia vizimba ambao walimweleza namna walivyofanikiwa. Baada ya kusikia maelezo ya vijana hao, Dk. Mpango alisema vijana hao wanapaswa kutangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama ushuhuda wa namna vijana wanavyoweza kujiajiri wenyewe. “Hawa vijana nataka niwaone kwenye vyombo vya habari mara k...