Skip to main content

Posts

Showing posts from May 12, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mshumaa wa upendo na matumaini wawashwa ALMC Kwa Wagonjwa Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Arusha Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) chini ya menejimenti ya Taasisi ya Moyo ya  Jakaya Kikwete (JKCI) wamekuwa wadhamini wakuu wa Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika jijini Arusha, yakihusisha shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na utoaji wa huduma za matibabu bure kwa wananchi. Maadhimisho hayo, ambayo hufanyika kila tarehe 15 Mei kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa huduma za uuguzi duniani Florence Nightingale, yaliwakutanisha wauguzi kutoka maeneo mbalimbali nchini katika viunga vya Hospitali ya ALMC. Kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho hayo, wauguzi pamoja na madaktari bingwa walitoa huduma za matibabu bure kwa wakazi wa jiji la Arusha kupitia vituo maalum vilivyowekwa katika Hospitali ya ALMC na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC). Zaidi ya wananchi 1,400 walipata huduma mbalimbali za uchunguzi wa afya hususan magonjwa yasiyoambukiza, huku wauguzi 600 nao wakinufaika na huduma hizo, na ku...

Naibu waziri Mmuya Awasili Zimbabwe Kushiriki Mkutano wa Sita wa masuala ya Maafa

NA, MWANDISHIWI WETU – MASVINGO – ZIMBABWE Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya (Mb), amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Sita (6) wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi unaofanyika Masvingo, Zimbabwe kuanzia tarehe 11 haadi 14 Mei, 2026. Mara baada ya kuwasili, Mhe. Mmuya amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Balozi Suzan S. Kaganda na kuipongeza Tanzania kushiriki katika mkutano huo unaolenga kujadili maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa programu za kikanda na masuala ya kimkakati katika utekelezaji wa afua mbalimbali katika Usimamizi wa maafa kwa nchi za SADC. Masuala mengine yaliyoelezwa na Mheshimiwa Balozi Suzani ni  pamoja na Tanzania kuendelea kuzitangaza fursa zilizopo ikiwemo sekta ya utalii, uchukuzi...

Rais Samia arejea Nchini kutoka Uganda

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amerejea nchini baada ya kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Jijini Kampala, tarehe 12 Mei, 2026. Akiwa nchini Uganda mh Rais Samia Suluhu Hassan, amehudhuria sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, zilizofanyika jijini Kampala, Uganda. Rais Museveni ameapishwa kuiongoza Uganda kwa muhula mwingine baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 15 Januari, 2026. Ushiriki wa Rais Dkt. Samia ni kielelezo cha kuendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Uganda, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda, kwa maslahi ya pamoja ya wananchi wa pande zote mbili. Tanzania na Uganda ni washirika wa karibu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiendelea kuimarisha ushirikiano katika nyanja za diplomasia, biashara, uwekezaji, nishati, uchukuzi, miundombinu, kili...

Wizara ya Maliasili na Utalii Mguu sawa Kudhibiti wanyama wakali na waharibifu

Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuimarisha mikakati ya kudhibiti migogoro kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu nchini kupitia hatua mbalimbali za uhifadhi na ushirikishwaji wa wananchi. Hayo yamejadiliwa katika semina maalum iliyotolewa kwa wabunge jijini Dodoma leo Mei 12, 2026 ikiongozwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu. Mikakati iliyojadiliwa ni pamoja na kuimarisha Jeshi la Uhifadhi, matumizi ya teknolojia za kisasa, doria, matumizi ya ndege nyuki, visukuma mawimbi na vilipuzi vyenye pilipili kufukuza tembo, kujenga  vituo vya askari, vizimba vya mamba na viboko, mabwawa ya maji pamoja na kutumia uzio wa umeme katika maeneo yenye changamoto pamoja na utoaji wa elimu ya uhifadhi kwa wananchi, kuboresha matumizi ya ardhi vijijini na kuimarisha mfumo wa kifuta machozi kupitia mfumo wa kidigitali wa PAIS. Pia, Semina hiyo ilijadili mpango wa ujenzi wa Makumbusho ya Marais Wastaafu katika eneo la Mtumba jijini...

Serikali Yatoa Bilioni 2.59 Kuimarisha Mtandao wa Barabara Butiama

  NAIBU Waziri Ofisi ya waziri Mkuu tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Festo Dugange ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuwekeza kwa kasi katika kuboresha miundombinu ya barabara katika Jimbo la Butiama, ambapo jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 5.33 zimetengwa katika miaka miwili ya fedha kwa ajili ya matengenezo, ukarabati na ujenzi wa barabara, madaraja na makalvati. Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Butiama Mheshimiwa Dkt. Wilson Charles Mahera, leo Mei 12,2026 Bungeni Jijini Dodoma, aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itaanza na kukamilisha utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa Barabara katika Jimbo la Butiama. Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe. Festo Dugange amesema Serikali imejipanga kuhakikisha mtandao wa barabara wa wilaya ya Butiama wenye urefu wa kilomita 596.62 unaboreshwa ili kuongeza ufanisi wa shughuli za kiuchumi na kijamii. “Wilaya ya Butiama ina mtandao wa barabara wa kilomita 596.62 unaohudumiwa na TARURA. Serikali imekuwa ikiten...

Mbunge wa Tabora Mjini Ampongeza Mganga Mfadhili Hospitali ya Rufaa Kitete kwa Uboreshaji wa Huduma za Afya

MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini, Mhe. Hawa Mwaifunga, amempongeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete), Dkt. Joackim Eyembe, kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuboresha huduma za afya kupitia matumizi ya mapato ya ndani ya hospitali hiyo. Akichangia bajeti ya Wizara ya Afya leo Mei 12, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mwaifunga amesema uongozi wa hospitali hiyo umefanikiwa kuboresha miundombinu mbalimbali, ikiwemo ukarabati wa baadhi ya wodi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa, hatua inayochangia kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi. Aidha, amesema hospitali hiyo imeanzisha kituo cha mazoezi (GYM) ndani ya hospitali, hatua inayolenga kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ya mwili ili kupunguza magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari na magonjwa ya moyo. “Jitihada hizi zinaonyesha dhamira ya kweli ya kuboresha afya za wananchi na kuimarisha mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza,” amesema Mhe. Mwaifunga.

Viongozi wa Afrika na Ufaransa Wajadili Uwekezaji na Maendeleo

_▪️Dkt. Mwigulu asisitiza matumizi sahihi ya rasilimali ili kujenga uchumi wa Afrika_ _▪️Rais Macron atangaza uwekezaji wa dola bilioni 27 Barani Afrika_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 12, 2026 ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa (Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and Growth Summit) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo umewakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa sekta binafsi, wadau wa maendeleo pamoja na wawekezaji kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, teknolojia, nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu pamoja na viwanda.   Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mkutano huo umekuwa wa manufaa kwa Bara la Afrika na Ufaransa kwa pamoja kwani majadiliano yamegusa namna ya kuzifanya pande hizo mbili ziweze kunufaika na ushirikiano huo. Amesema rasilimali zinazopatikana b...