Na Angela Sebastian ;Bukoba Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhan Kido amewataka viongozi na,watumishi na wataalam wa mkoa huo kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi,weledi,uadilifu na kuzingatia taratibu zote za manunuzi na utaratibu wa mikataba ya inayohusu miradi husika ili raslimali za Umma zitumike kwa ufanisi. Kanali Kido ametoa maagizo hayo wakati wa warsha maalum iliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Kagera ya kuwajengea uwezo wadau kutoka sekta mbalimbali mkoani humo, juu ya usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo amesema katika miradi yote inapaswa kuzingatiwa ubora,muda wa utekelezaji,matumizi sahii ya fedha za Umma na kuhakikisha sheria zinafuatwa kikamilifu. Aidha amewataka wadau wanaohusika na usimamizi na utekelezaji wa miradi ya mbalimbali ya ujenzi kuhakikisha wanafanya upimaji wa vifaa wanavyotumia katika ujenzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, sambam...
Marato tv - Sauti ya Jamii