Skip to main content

Posts

Showing posts from October 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kibunda cha Bilioni 426.5 kuwanufaisha wanafunzi 135,240 awamu ya kwanza

Na: Mwandishi Wetu, ARUSHA  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeidhinisha Shilingi Billioni 426.5 awamu ya kwanza kwa ajili ya wanafunzi wanufaika 135,240 ili kugharamia masomo yao. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, Oktoba 24, 2025, alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Ofisi ya HESLB Jijini Arusha. "Tunapenda kuutarifu Umma wa Tanzania kuwa HESLB imeidhinisha Bilioni 426.5 kwa ajili ya wanafunzi 135,240 kwa awamu ya kwanza," amesema Dkt. Kiwia. Katika hatua nyingine, Dkt. Kiwia amesisitiza kuwa katika fedha hizo, Shilingi Bilioni 152 zimegharamia wanafunzi 40,952 wa Shahada ya awali na 5,342 wa Stashahada. Aidha, waombaji mikopo wa Samia Skolashipu wapatao 615 wameidhinishiwa Shilingi Bilioni 3.3 huku Shilingi Bilioni 271.2 zikiidhinishwa kwa ajili ya wanafunzi 88,331 wanaendelea na masomo yao katika vyuo mbalimbali hapa nchini. Ikumbukwe kuwa Bodi ya Mikopo kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia k...

Watanzania Waombwa Kuliombea Taifa Kuelekea Uchaguzi Mkuu

 Taasisi ya TANZANIA JUMUISHI imetoa wito kwa watanzania juu ya kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani huku ikihimiza watanzania kufanya ibada ya kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika mwezi oktoba 29. Akisoma Tamko hilo mapema hii leo, oktoba 25, 2025, Innocent Gabriel Siriwa, Katibu wa Taasisi ya TANZANIA JUMUISHI (TAJU), Yenye lengo kuu la kuzitambua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini, ambapo amesema kwa nia nzuri na ya kizalendo imeona iitishe hafla hii ili kuhamasisha kuombea amani uchaguzi mkuu. Aidha, Innocent amesema kuwa jamii imekuwa ikisahau juu ya uwepo wa watu wenye ulemavu hivyo uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani kuelekea uchqguzi mkui ni wazi kuwa jamii inashindwa kujali uwepo wa idadi kubwa itakayoathirika ya kundi la watu walemavu. Hata hivyo, Taasisi hiyo ya TAJU kupitia Katibu wake ndugu Innocent Gabriel Siriwa imewaomba viongozi na wasimamizi wa uchaguzi wa mkuu wa mwezi oktoba kusimamia kwa weledi na haki ...

Dkt.Nchimbi Ahitimisha Mikutano Yake ya Kampeni,Ukerewe Jijini Mwanza

PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi  katika uwanja wa Gertrude Mongella Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza leo  Oktoba 25, 2025. Mkutano ndiyo wa mwisho kwa Dkt Nchimbi kabla ya uchaguzi mkuu Oktoba 29,2025.

Waziri Dkt. Stergomena Tax Atimiza Ahadi yake Kwa Kukabidhi Madawati 80 Shule ya Msingi Nyambitilwa Magu

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax,  tarehe 24 Oktoba 2025, amekabidhi madawati 80 ikiwa ni kutimiza ahadi yake  aliyowahi kuitoa kwa Shule ya Msingi Nyambitilwa, Wilaya Magu mkoani Mwanza. Katika makabidhiano hayo, Mhe. Dkt. Tax aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu, Bw. Mohamed Ramadhan. Akizungumza na Uongozi wa shule pamoja na hadhira ya Wanafunzi wa Shule ya Nyambitilwa, Mhe Dkt. Tax amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao na matarajio ya wazazi wao na Taifa kwa ujumla. Aidha, Waziri Tax ametoa wito kwa jamii na wadau wengine ikiwemo wana Magu kujenga utaratibu wa kurudisha kwa jamii kwa kutoa misaada hasa katika Sekta ya elimu ili kukabiliana na uhaba wa vifaa na miundombinu ya elimu mashuleni ikiwa ni pamoja na Wilayani Magu,      Kabla ya kuhitimisha tukio hilo la kukabidhi madawati hayo, Dkt Tax ametumia fursa hiyo kutoa rai na kuwataka Walimu na  Wa...