Skip to main content

Posts

Showing posts from October 20, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

7th SADC Groundwater Conference to Explore Innovative Solutions

By Prosper Makene, Senior Journalist Dar es Salaam, Tanzania.  The 7th SADC Groundwater Conference is scheduled to take place from November 19 to 21, 2025, in Johannesburg, South Africa aims at strengthening sustainable groundwater management practices through regional collaboration and innovation. The conference’s theme: "Investing in Groundwater for Climate Action" with Sub-themes: Groundwater and Mitigation of Climate Change: Exploring how sustainable groundwater management can contribute to climate resilience, Adaptation Strategies for Groundwater Management: Discussing climate-smart groundwater infrastructure options and conjunctive surface and groundwater management. The conference of its kind will be held at Birchwood Hotel and OR Tambo Conference Center, Johannesburg. The 7th SADC Groundwater Conference is set to strengthen sustainable groundwater management practices through regional collaboration and innovation.  Key outcomes  Advancing Knowledge Sharing: Provid...

Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Saalam Tujitokeze Kwenye Mikutano Yote ya Dkt Samia-Msama

  Aliyekuwa mtia nia wa Ubunge Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Production, Alex Msama, ametoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kumpokea na kushiriki katika kampeni za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na mgombea urais kupitia chama hicho. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Msama amesema ujio wa Rais Samia katika jiji la Dar es Salaam ni tukio muhimu linaloonesha dhamira yake ya kukutana na wananchi na kuwasikiliza moja kwa moja kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Amefafanua kuwa Rais Samia amekuwa akipokelewa kwa shangwe na hamasa kubwa katika mikoa yote aliyoitembelea, hali inayoonyesha mapenzi makubwa ya wananchi kwake. “Rais wetu amezunguka katika mikoa mingi na kila alipofika amepokelewa kwa furaha kubwa. Sasa anakuja Dar es Salaam, hivyo ni jukumu letu wakazi wa jiji hili kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumuunga mkono katika kampeni zake ambazo zitafanyika ...

Glory Aahidi Kuboresha Huduma za Afya, Elimu, na Miundombinu ya Maji

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Glory Tausi Shayo, ameahidi kufanya mabadiliko makubwa katika sekta za afya, elimu, na miundombinu ikiwa atachaguliwa kuwa mbunge.  Akizungumza katika kampeni zake, Tausi amesisitiza kuwa atahakikisha wananchi wengi wanapata fursa ya kuwa na kadi za bima za afya ili kupunguza gharama za matibabu zinazowaumiza wananchi wengi. Katika kuendelea na ahadi hizo, Tausi pia amejizatiti kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayezuiliwa kupewa maiti yake hospitalini pale ambapo msiba utatokea. "Hatutaruhusu maiti zizuiliwe hospital, tutahakikisha mtu akipatwa na msiban basi anapewa maiti yake," alieleza. Aidha, mgombea huyo ameweka bayana ahadi ya kuondoa michango inayotozwa katika elimu bure, kwa lengo la kuhakikisha watoto wa familia maskini wanapata elimu bila vikwazo vyovyote. "Tutahakikisha kuwa elimu bure inatekelezwa kikamilifu," alisema. Tausi amezungumzia pia masuala ya ajira, akiahidi kuwa atahakikisha wana...

Rea Yaendelea Kutekeleza Kwa Vitendo Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia

📌 *Majiko banifu 4,836 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe*  📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 8,850 tu* . 📌 *Kila walaya kupata majiko 1,209*  📍 *NJOMBE*  Mkuu wa  Wilaya ya Ludewa Mhe. Olivanus Thomas akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo Oktoba 20,2025 amezindua rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa wilaya , Maafisa kutoka REA pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji vyake.  Mhe. Olivanus amesema , lengo la uzinduzi  wa mradi huu ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi. Mhe. Olivanus, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo lit...

Dkt Nchimbi - Dkt Samia Amepaisha Bajeti Sekta ya Uvuvi,Apewe Mitano Tena

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake ndani ya miaka minne ameleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Uvuvi kwa kuiongezea bajeti zaidi ya mara sita ili iweze kuwa na tija. Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Oktoba 20, 2025 wakati akiwahutubia  Wananchi kwenye mkutano wake wa kampeni za Urais katika jimbo la Kilwa Kaskazini, Mkoani Lindi, ambapo amenadi  Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025-30, Sera zake pamoja na kumuombea Kura Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani kwenye kanda hiyo ya kusini. "Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Uvuvi hasa kwa mkoa wa Lindi ni pamoja na kujengwa kwa Bandari ya Uvuvi iliyogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200" amesema Dkt Nchimbi. Katika hatua nyingine Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo pia kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini Ndugu Kinjeketile Ngombale MWIRU n...