*_Aibua maeneo ya uwekezaji, ushirikiano zaidi na Tanzania_* WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Rais Mteule na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Biashara ya Afrika (Afreximbank), Dkt. George Elombi na kuainisha maeneo zaidi ya uwekezaji nchini Tanzania. Mheshimiwa Majaliwa amesema anaamini kuwa katika kipindi cha uongozi wa Dkt. Elombi, benki hiyo itaongeza kwa kiwango kikubwa mchango wake katika kusukuma mbele biashara, maendeleo ya viwanda na uwekezaji wa kimkakati barani Afrika ikiwemo Tanzania. “Tunapenda kukuhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kujitolea kikamilifu katika ushirikiano wake wa kimkakati na Afreximbank,” alisema. Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Majaliwa alihimiza umuhimu wa Afreximbank kukamilisha mpango wake wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha tiba nchini Tanzania (African Medical Centre of Excellence) ambacho kitakuwa na uwezo wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi na pia kupunguza utegemezi wa rufaa za nje ya...
Marato tv - Sauti ya Jamii